Abdallah Twalipo na Tumainiel Kiwelu: Vita na Uganda 1978-79 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abdallah Twalipo na Tumainiel Kiwelu: Vita na Uganda 1978-79

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chifunanga, Jun 20, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wadau, natafuta info kuhusu hawa jamaa, nimesikia walikuwa makamanda kwenye vita ya 1978. Mwenye info zaidi atumwagie hapa.

  Abdallah Twalipo na Tumainiel Kiwelu
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,691
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Ongezea Mojar General Mayunga - Mti Mkavu
   
 3. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Katika pitapita yangu kutafuta info hizo, nimeona vitu viwili hapa vya kuongelea kwenye thread hii:

  1. Libya walikuwa upande wa Idd Amin wakati wa vita hii. Labda na sisi tumptezee Ghadafi kwa sababu alileta wajeshi wake wapigane na Tanzania.
  2. OAU ilikataa kuisupport Tanzania katika hii vita, walidai kuwa Wabongo (Nyerere) ni wakorofi na wanapenda kuingilia soverignity ya nchi nyingine kama Seychelles na Uganda na kuweka puppet leaders.....Kutoka na jambo hili, ilibidi Tanzania ilipie shughuli yote ya vita na peacekeeping process afterwards, peke yake bila kusaidiwa na nchi nyingine yoyote. Jambo hili liliipelekea Tanzania kuwa maskini sana, baada ya vita.....Sasa kitu cha kudiscuss ni kwamba, nimesikia kuwa Uganda ililipa deni lote la vita mwaka 2007!!....kunayeyote mwenye info kuhusu hayo malipo?
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,934
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  CHIFUNANGA......A man of the people, umeleta mada ambayo kweli inahitaji majibu na haiko-biased
  GREAT THINKER
   
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Avatar yako nimeipenda sana, inaonyesha ni jinsi gani serikali inamlea mkuu wa jeshi la polisi ambaye ameshindwa kuwadhibiti polisi wake wa barabarani wanaochukua rushwa mchana kweupee. Hii inasikitisha sana imekuwa donda sugu ambalo ni vigumu kupona, mimi binafsi nalazimika kupanga budget ya rushwa ktk mshahara wangu.

  Imekuwa vigumu kuwaepuka hawa polisi wanalazimisha makosa hata ambayo hayapo ili mradi utoe rushwa la sivyo watakucheleweshea shuhuli zako na huna pa kwenda kuwashtaki kwa vile ni mfumo umejengeka katika jeshi zima la polisi. Hapa nilipo nina namba za askari wote(kama 10 hivi) niliowahi kuwapa rushwa kutokana na tabia yao ya kunyan'ganya leseni na kukaa nayo hadi utakapompelekea rushwa anayotaka, Eee Mungu tuepushe na janga hili!!!
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,904
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 180
  Leutenant General Abdalla Twalipo(1974-1980) alikuwa CDF -Chief of Defence Forces(TPDF)
  na Brigadier General Tumainiel Kiwelu(1975-1980) alikuwa Chief of Staff(TPDF)
   
 7. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu, sasa hivi wako wapi, wanafanya nini......nimesikia Twalipo alishafariki.
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,339
  Likes Received: 1,694
  Trophy Points: 280
  Twalipo GENERAL ..alikuwa mkuu wa majeshi wakati wa vita vya kagera.....General Tumainiel Kiwelu alipelekwa mstari wa mbele mwanzoni mwa vita lakini baadaye ikaonekana ni bora aje awe msaidizi wa Twalipo kama chief of staff.....kwani alikuwa kati ya maafisa wa mwanzo kabisa jeshini kusoma Sundhurst....mabadiliko hayo yalipelekea Brigedia David Musuguri kupandishwa cheo na kupelekwa msatari wa mbele kama Mkuu wa mapambano...akisaidiwa na mabregadia ..Walden,Mwakalindile,Mwita Marwa,James ,Burton,Lupogo....
  Mara nyingi watu Kama kina General Twalipo na Kiwellu walifanya kazi kubwa sana kwenye central command unit dar es salaam wakishirikiana kwa karibu na Amiri jeshi mkuu[Julius nyerere] kutokana na nyazifa zao....
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,339
  Likes Received: 1,694
  Trophy Points: 280

  Ni kweli marafiki walituziria vita ile ili tuadhirike hasa kutokana na influence ya Tanzania kijeshi enzi ile kuwa juu sana ..kama ulivyosema ..Nyerere alikuwa akidhibiti nchi za Comoro,Seyshells na Re-Union...huko maafisa wa Tanzania kama Brigedia Ngwilizi na Iddi GANHU ...Walikuwa kama viongozi wa kijeshi ...chini wakiwa na viongozi wazawa walioripoti kwao na wao kwa Nyerere daily.....Uganda baada ya vita alipandishwa cheo akaachwa pale Brigedia Msuya ..kuwa mtawala wa Uganda....

  Maafisa wa kitanzania kama kina ALI MAHFOUDH walikuwa wakipigana Msumbiji ..baadaye wakapokewa na Brigedia Mwakalindile na baadaye Ngwilizi.....hiyo ni kuacha role ya watu kama Brigedia General Hashim Mbita..ambaye alikuwa alongoza kamati ya mstari wa mbele ...na maafisa waliokuwa wakiendesha makambi ya wapigania uhuru wa Angola,zimbabwe,Namibia,South afrika etc....in short vita ya uganda ni wazi Iddi Amini alichochewa ili tuadhirike..na kudumaza kasi ya ukombozi....influence ya Tanzania kwa ukanda huu ilikuwa kama ya marekani kwa sasa kwa dunia...tatizo hatukutafuta infulence ya kiuchumi
  .
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nilisoma kitabu kinaitwa WAR IN UGANDA kimeandikwa na Martha Honey na Tony Arvigan. kweli vijana wetu walifanya kazi kubwa saaaana ukukisoma hicho kitabu mpaka utapenda makamanda km akina Mwita Marwa, Silas Mayunga BR. Waden waganda walipomwona wakasema tumekodisha wajerumani jamaa alikuwa chotara. kuna siku wanajeshi wa bongo walishambuliwa ilikuwa karibu na mto wale soldiers wetu wakakimbilia ndani ya maji wakajifika for six hrs yaani pua tu zimechomoza wasikose hewa.

  Baada ya hapo wanajeshi wa nduli wakaondoka jamaa zetu ndo wakaibuka toka hapo yule kamanda wao wakamuita AMPHIBIA. Kulikuwa na mtu anaitwa Ben Msuya kanali huyo na yeye alikuwa frontline. ile vita bana haikuwa lelemama.

  Kuna mpiganaji mwingine akiitwa OYITE OJOK huyu alikuwa ni mganda alikuwa pilot mzuri sana wa ndege maskini alikufa kwa ajali ya helcopter kwa Uganda alikuwa ofisa kwenye jeshi la museveni.
   
 11. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  asanteni sana wadau kwa mchango wenu.....sijui huu GLORIOUS TANZANIA tumeipotezea wapi.....yaani Kuanzia RUKSA mpaka hapa tulipo sasa kuna FAULO moja imechezwa, si haba.
   
 12. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani tatizo ni kwamba, Nyerere alikuwa too far ahead of his time...kiasi kwamba waliomzunguka walikuwa hawamuelewi....kang'atuka yeye na falsafa zake zote.....watu wamekuja kuanza upya, na mambo ya ajabu.
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  imagine ndo NDULI angetuvamia leo under huyu sharobaro tuliyenaye si angekimbia nchi huyu?
   
 14. M

  Masuke JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,603
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kiwelu alijenga maeneo ya mbezi inn, nadhani bado anaishi hapo.
   
 16. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mnakumbuka mizinga ya BM-Katyushya. Walikuwa nayo waganda. Hawakujua hata kuipiga. Tuliiteka na vijana wetu walijua jinsi ya kuitendea haki. Ikipigwa ilikuwa inawika kama ngurumo ya radi. Waganda waliiita 'sabasaba'. Lakini zaidi ya yote Mzee Julius Nyerere alikuwa kichwa jamani. Hivi kwa ma rais wa Afrika ni nani angeweza kutamka mbele ya hadhara kwamba 'uwezo wa kumpiga tunao,sababu ya kumpiga tunayo na nia ya kumpiga tunayo na tunataka dunia ituelewe hivyo' huku akielewa Ghadaffi anamsaidia amini. Tena alisema nchi zote zinazotaka kumsaidia Amin zimsaidie yeye atasimama peke yake. Hiyo ndiyo definition ya mwanamume kwenye matatizo!
   
 17. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hatujapata kiongozi asiye mung'unya maneno kama Mwalimu hadi hii leo, hasa in times of contoversy.
  Lakini uwezo wake ni jinsi wananchi hata wa kawaida kabisa walivyomuelewa na kulichukulia tatizo la kuvamiwa kwa uzito unaostahili.
  [​IMG]
  BM-21 Grad multiple rocket launcher system(katyusha)  BM-21 tulikuwa nayo mkuu na ilikuwepo sana ikionekana mitaani ikielekea huko vitani.
  Ni siku hizi tu inaelekea iko stoo.
   
 18. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Choko choko za wamalawi zinafanya tuwakumbuke mashujaa wetu
   
 19. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2013
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 530
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Waungwana Philemon Michael,Chimunguru,Thanda, JokaKuu,Kichuguu,Roullete , pamoja na wadau wengine, tafadhalini kuna mada moja humu inazungumzia kwa mtiririko mzuri jinsi ile vita ilivyokua inaendelea .
  Yaani Gen. Kiwelu alipitia mpakani mwa Rwanda na Uganda pamoja na kikosi cha Museveni, naitafuta sana hiyo mada ipo wapi ?

  Natanguliza shukrani
  JF JUNGU KUU.

   
 20. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2013
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 943
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli kabisa kitabu hicho kina maelezo ya kina kuhusu vita vya Kagera na na makamanda wetu. Nilikisoma kitambo sana na nilikuwa impressed sana na Ben Msuya alivyokuwa akiongoza kikosi chake.
   
Loading...