VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Najitokeza kwa mara ya pili leo kumzungumzia Alhaji Abdallah Bulembo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM na kada mbobezi. Mara ya kwanza ilikuwa alipohusishwa na kukwamisha uchaguzi wa Meya Dar. Nilimshauri ajitenge na uchaguzi huo.Uchaguzi ukafanyika.
Leo,natoa wito wenye mvuto kuwa kada huyu awe wa kwanza kufukuzwa toka CCM. Ameharibu mchoro wa chama. Chama kinajichora kiubora kuwa kipo makini na pamoja. Kinajichora kuwa imeamuliwa bila kulalamikiwa kuwa Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa chama hapo Julai 23.
Kusema kuwa wanaopinga Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti waondolewe chamani,ni kuharibu msimamo wa chama. Ndani ya CCM,kimchoro usio na kihoro,hakuna wanaopinga. Wote wanashangilia bila kulia kwa kadhia. Wote wanataka kukabidhi badala ya kuchagua.Hakuna anaowasema!
Kwakuwa amesema lisilokuwepo,Bulembo awe wa kwanza kufukuzwa CCM.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)