Abdallah Ali Hassan Mwinyi na Said Gharib Bilali ni miongoni mwa waliojitokeza kugombea ubunge

JacksonMichael

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
339
61
WANACHAMA Saba wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) wamejitokeza kuchukua fomu za Ubunge wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kupitia chama hicho, wakiwemo wabunge watatu wanaomaliza muda wao.

Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama, Ali Hassan alithibitisha kujitokeza kwa wanachama mbalimbali kuchukua fomu katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, mjini Unguja.

“Ni kweli wamejitokeza wanachama saba wa chama cha Mapinduzi kuchukua fomu kwa
wakati huu ambapo muda wa mwisho wa kuchukua fomu utakuwa saa kumi za jioni,” alisema
Hassan.

Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwemo viongozi wa mashirika mbalimbali ya Serikali walionekana wakiingia katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

Hata hivyo, baadhi yao walifika katika ofisi ya Idara ya Oganaizesheni na kuziangalia fomu hizo na kuondoka, wengine wakidai kwenda kupata ushauri zaidi wa kitaalamu kabla ya kuchukua fomu hizo.

Wabunge waliochukua fomu ambao muda wao unamalizika ni pamoja na Dk. Said Gharib Bilali,
Septuu Mohd Nassor na Abdallah Ali Hassan Mwinyi.

Hata hivyo, sura mpya zilizojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwamtipura kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita la Jamhuri ya Muungano, Zuberi Ali Maulid.

Wengine ni Mariam Ussi Yahya, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali awamu iliyopita, Khamis Jabir ambaye alikuwa Mwakilishi wa jimbo la Bububu.

Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM-Zanzibar inatazamiwa kukutana hapa ikiwa ni sehemu ya kupanga ajenda za kikao cha Kamati maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar ambacho kitapokea taarifa ya majina ya wagombea nafasi hizo.
 
Back
Top Bottom