ABCs za kulinda kura - kwenu mawakala na Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ABCs za kulinda kura - kwenu mawakala na Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 29, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Naomba mawakala wa Chadema wafanye yafuatayo ili kudhibiti wizi au udanganyifu wa matokeo ya uchaguzi kwa ujumla:

  1. Kabla ya kufungua kituo wawe na idadi ya wapiga kura kutokana na majina yaliyobandikwa milangoni,

  2. wajue idadi ya karatasi za kupigia kura katika kituo kwa ngazi zote za uongozi - udiwani, ubunge na urais,

  3. mara tu baada ya kufunga kituo wapate idadi ya watakaopiga kura kwa ku-tally (yaani kuweka alama za mafungu matano matano na baada ya zoezi watajumlisha),

  4. pia wapate idadi ya karatasi za kupiga kura zilizobaki,

  5. wafanye mahesabu ya kutoa na kujumlisha ili kuweza kufahamu kama kuna wapiga kura zaidi ya waliobandikwa pale mlangoni, kama kuna karatasi za kupigia kura zaidi ya idadi ya mwanzo,

  6. kwenye kuhesabu kura hasa kwenye idadi, jumla ya kura za wagombea wote, zilizoharibika, ambao hawakupiga kura ziwe sawa na idadi ya majina yaliyobandikwa mlangoni. Mfano: majina mlangoni ni 400, walioingia na kupiga kura ni 350 au 450. Kama ni 450 tayari hapa kuna dosari kubwa hivyo wakala lazima amwite mgombea mara moja. Kama ni 350, basi jumla ya kura za matokeo lazima iwe 350 yaani kwa wagombea wote ikiwemo zilizoharibika: mfano halisi ni huu kwenye mabano (CCM 30, Chadema 250, NCCR - Mageuzi 10, TLP 2, DP 8, zilizoharibika 50 jumla ni 350) kwa kila ngazi ya uongozi.

  7. wakala hahakikishe zinafungwa hizo kura 350 vizuri; zikifunguliwa tena ngazi ya kata au jimbo idadi iwe ile ile na masanduku yasibadilike, ikiwezekana pendekeza kuwa yale yenye kura zilizokwisha kupigwa na kuhesabiwa yawekewe alama kwa marker pen rangi ijulikane hapo hapo

  8. idadi ya kura zote iwe sawa na idadi ya kwenye vituo, tofauti yoyote, kiongozi wa Chadema apewe taarifa mapema

  9. mawakala wahakikishe yule mtu wa tume ya taifa ya uchaguzi ambaye atakuwa na komputa kabla ya kutuma matokeo makao makuu ya Tume anaonesha alichokijaza kabla ya kutuma, yaani -preview-, halafu washuhudie anabonyeza kitufe cha 'save and send' na baada ya muda mfupi majibu kuonesha 'tayari' (relayed successfully or saved) [inategemea kama hiyo database ni web based kama ni web based bas saved inatosha

  10. mawakala wapate nakala za matokeo yote kwa ngazi zote kwenye karatasi zenye nembo na mihuri ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  11. mawakala wajiandae kama wanakwenda kwenye mtihani - wawe na penseli (kalamu ya risasi), kifutio, note book, kalamu ya wino, simu zao ziwe na hela kidogo, muda wote wawe makini, wayasome mazingira ya kituo vizuri - ndani na nje mita 400 za mraba.

  NB: Tukijitahidi na ili nchi imekombolewa jamani. Kama mna ABCs nyingine changanyeni na hizi.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wizi wa kura kila sehemu
   
Loading...