ABC za biashara ya Bajaji

Niite Profesa

Senior Member
Jun 19, 2015
100
106
Habarini ndugu wana JF

Poleni na mihangaiko ya siku.

Niende moja kwa moja kwenye mada,ndugu zangu mimi ni kijana ninayepambana ili kuhakikisha naweza kutimiza ndoto na malengo niliyojiwekea.Nimekuwa nikipambana kwa muda sasa yapata miaka 3 tokea nilipomaliza elimu yangu kwenye chuo fulani.

Nimekuja hapa kwenye jukwaa la JF kuomba ushauri na kupatiwa maelekezo ya kina kuhusiana na issue ya Bajaji.Mambo ninayohitaji kuyafahamu ni kama ifuatavyo,

1.Nahitaji nianze kazi ya Bajaji.Je,ni vitu gani muhimu vya kuzingatia kabla sijaanza hii kazi kama dereva wa Bajaji?

2.Wapi naweza pata mafunzo ya uendeshaji wa Bajaji na kupatiwa leseni?

3.Kazi/biashara hii ya Bajaji inakabiliwa na changamoto zipi?

Pia kama kutakuwa na kitu cha muhimu ambacho sijakiuliza naomba unifahamishe ndugu mwana JF.

Natanguliza Shukrani na Mungu awabariki
 
Tafuta dereva wa bajaji muombe akifundisha japo kwa malipo kidogo wakati anakufundisha utapata retail zote hapo,

Baada ya hapo zama veta au driving school yeyote daka leseni anza kazi.

Amani iwe nawe
Asante sana kwa mchango wako ndugu ntafanyia kazi ushauri wako
 
Jifunze kuendesha vijiweni tu halafu,

Nenda ofisi ya TRA Mkoa halafu waambie unahitaji leseni ya udereva daraja A2 halafu wasikilize.

*Beba 150K na NIDA au TIN Number.

Just one working day,jioni yake unapokea SMS ya TRA ufuate leseni yako.
 
Namna mzuri ya kujifunza udereva ni kwa Hawa madereva wa vijiweni.

Tafuta rafiki Muombe akufundishe kwa kumlipa kidogo ukishajua Anza kufatilia leseni TRA achana na Mambo ya driving school watakupiga Sana hela.
 
Jifunze kuendesha vijiweni tu halafu,

Nenda ofisi ya TRA Mkoa halafu waambie unahitaji leseni ya udereva daraja A2 halafu wasikilize.

*Beba 150K na NIDA au TIN Number.

Just one working day,jioni yake unapokea SMS ya TRA ufuate leseni yako.
Safi hii ni shortcut.mambo ya vyuo yatamchelewesha jamaa.😁😁😁
 
Jifunze kuendesha vijiweni tu halafu,

Nenda ofisi ya TRA Mkoa halafu waambie unahitaji leseni ya udereva daraja A2 halafu wasikilize.

*Beba 150K na NIDA au TIN Number.

Just one working day,jioni yake unapokea SMS ya TRA ufuate leseni yako.
Asante kwa mchango wako mkuu ntafanyia kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom