Abbas Sykes katika kitabu cha Abdul Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,854
30,200
ABBAS SYKES NDANI YA KITABU CHA ABDULWAHID SYKES

Hesabu yangu ya wanachama watatu waliobakia wa siku za mwanzo za TANU na harakati za kudai uhuru mwaka wa 1954 imepungua baada ya kufariki Abbas Sykes.

Yawezekana sana kuwa bado wapo waasisi wengi wa TANU walio hai lakini hawajulikani.

Daftari langu limebakia na Mama Maria Nyerere na Mzee Athmani Matenga wa Magomeni Mwinyimkuu.

Mama Maria Nyerere nimeelezwa kuwa ameshauriwa asizungumze na waandishi wa habari.

Ikiwa hivi ndivyo ni kuwa haiwezekani kwa sasa kupata lolote kwake kuhusu historia ya TANU.

Inawezekana imeingia hofu kidogo huenda Mama Maria akazungumza mambo katika historia ya TANU ambayo hayakubaliani na historia rasmi.

Katika hii miaka ya karibuni nimekuwa nikipokea waandishi vijana wengi kutoka vyombo vya habari wakitaka kujua mengi kuhusu historia ya Abdul Sykes na TANU na mimi nikawa kila mara nawashauri wakamhoji Mama
Maria na sababu ni kuwa yeye kayaona yote kwa macho yake.

Nilikuwa nawashauri wakazungumze na Mama Maria ili wapate yakini kwa yale niliyowaeleza.

Abbas Sykes ni kati ya watu wa mwanzo kumjua Julius Nyerere pale alipofika nyumbani kwao kuonana na kaka yake Abdul na Nyerere hakuwa pekee katika watu waliokuwa wakienda kwa Abdul Sykes wakati ule akiwa secretary na Act. President wa TAA.

Nyumba ya Abdul Sykes ilikuwa ilikuwa nyumba ya wanasiasa wa TAA na pia machifu wa Tanganyika kuanzia Mangi Mkuu wa Wachagga Thomas Marealle na Chifu wa Wasukuma Chief David Kidaha Makwaia na Mtemi wa Wanyamwezi Chifu Abdallah Said Fundikira hadi Mwami Theresa Ntare wa Kasulu.

Miaka hii Abbas Sykes alikuwa kijana mdogo mtazamaji wa yale yote hakuwa mchezaji wa siasa za Tanganyika.

Mimi nimekutana na Abbas Sykes mwaka wa 1953 ndani ya Nyaraza za Sykes kumbukumbu zao wenyewe kuhusu harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Huu mwaka wa 1953 ndiyo Abbas Sykes alianza kupangwa kucheza mechi na mpangai wa timu alikuwa kaka yake Abdul Sykes kiongozi wa juu kabisa katika TAA pale Makao Makuu, New Street.

Mwaka wa 1952 baada ya Japhet Kirilo na mkalimani wake Earle Seaton kurejea mikono mitupu kutoka UNO kuwasilisha mashtaka ya Wameru waliodhulumiwa ardhi yao na Wazungu Septemba 1953 TAA iliamua kuunda kamati ya watu watatu izunguke Tanganyika kuwaeleza Watanganyika dhulma hii na pia kuchangisha fedha kupeleka ujumbe mwingine UNO kudai uhuru.

Wajumbe wa kamati hii walikuwa Abbas Sykes, Japhet Kirilo na Saadan Abdu Kandoro.

Kwa takriban mwezi mmoja kamati hii ya watu watatu ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.

Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.

Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kusudio hilo.

Kabla kamati haijakamilisha ratiba yake Abbas akaugua ikabidi arudishwe Dar es Salaam haraka apate matibabu.

Picha ya kwanza kushoto kulia wa kwanza ni Abbas Sykes na chini yake aliyekaa kwenye kiti ni Dossa Aziz.

Katika mstari huo wa Dossa mtu wa sita ni Julius Nyerere.
Hii ni katika miaka ya mwanzo ya TANU.

Picha nyingine na Athmani Matenga mmoja katika wana TANU wa mwanzo katika tawi la Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu lililoasisiwa na Ali Msham.

1621097290449.png


186491478_949029289177783_3473432066027363475_n.jpg


186334630_949173499163362_3999256643605141086_n.jpg
 
katika watu ambao natamani sana kukutana nao....aisee ni wewe mzee wangu...namuomba mwenyezi Mungu atukutanishe...unifundishe
 
Back
Top Bottom