Abbas Mtemvu afungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga ushindi wa mgombea wa CUF

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
attachment.php

Aliyekuwa Mgombea ubunge Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Abbas Mtemvu amefungua kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CUF Abdallah Mtolea (CUF) aliyepata kura 103,231.

Katika kesi yake amemshataki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi pamoja na mgombea wa CUF.

Katika madai yake Abbas Mtemvu anasema kuwa msimamizi wa Uchaguzi alibadilisha matokeo yake na kumpa mgombea wa CUF.

Amedai kuwa ushahidi wote anao na ana uhakika kesi ikienda vizuri na haki ikizingatiwa atatangazwa mshindi.
 
Attachments

  • MTEMVU.JPG
    MTEMVU.JPG
    13.5 KB · Views: 2,866
Hapo sasa Mwanasheria mkuu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa ccm naye anainguzwa kama shahidi na mshtakiwa ...atakua upande gani? Utoaji haki umevurugwa sana na ccm . Inainguza nchi katika uvunjaji mkuu wa katiba.
Ni hatari kubwa na mbunge akikemea tabia hii wale wa ccm wanazomea...bora angeitwa mwanasheria mkuu wa ccm tu
 
Atulie sasa huyu mzee alee wajukuu...hivi yule binti yake ajuza Sitti Mtemvu yuko wapi?
 
Hata uchaguzi ukirudiwa mara 100 kwa temeke mtemvu hawezi kushinda , ushauri wangu kwake , atafute jimbo mkoa wa dodoma agombee miaka ijayo .
 
Ha ha ha ha Mtemvu tulia tu.
Ni hivi, kinachomsumbua mtemvu ni namna ya kuficha uso wake mbele ya jamii , kwa mila za kiafrica ni aibu sana kwa mtu mwenye kitambi kushindwa jambo , na hasa kama ana mke zaidi ya mmoja .
 
Ndio maana hatuendelei,Yaani hiki kizee linataka kikasinzie tuu kule mjengoni na kuitika ndiyoooooo!.
 
Alianzisha mashindano ya mpira wa miguu mwaka wa uchaguzi tu anaoneka uchaguzi ukikaribia akadhani atawateka raia hahahaa ndo ajue kuwa watu wa Temeke wameelimika sasa
 
Ni hivi, kinachomsumbua mtemvu ni namna ya kuficha uso wake mbele ya jamii , kwa mila za kiafrica ni aibu sana kwa mtu mwenye kitambi kushindwa jambo , na hasa kama ana mke zaidi ya mmoja .
Bora umesema ukweli leo ,sio kila saa kujitoa ufaham ,et timeibiwa kura
Kwa mwaafrika kushindwa kwake amehujumiwa
akifa amelogwa
Cc
Mamvi
 
Msimamizi wa uchaguzi alifanya hivyo (kuhamisha kura za Mtemvu na kumpa huyo wa CUF) kwa maslahi gani na ya nani?
 
Msimamizi wa uchaguzi alifanya hivyo (kuhamisha kura za Mtemvu na kumpa huyo wa CUF) kwa maslahi gani na ya nani?

HUyo Mtemvu ni Kibaka Mzoefu wa Kura! Na hivyo ndivyo wizi aliokuwa akiutumia yeye Mtemvu katika chaguzi zote zilizopita na kumpatia ushindi . Yaani mwizi kaibiwa leo duuu! Muulizeni Tambe Hiza anamjua Mtemvu kwa staili yake ya wizi!
 
Hapo sasa Mwanasheria mkuu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa ccm naye anainguzwa kama shahidi na mshtakiwa ...atakua upande gani? Utoaji haki umevurugwa sana na ccm . Inainguza nchi katika uvunjaji mkuu wa katiba.
Ni hatari kubwa na mbunge akikemea tabia hii wale wa ccm wanazomea...bora angeitwa mwanasheria mkuu wa ccm tu

Ndugu, huo ndio utaratibu wa ufunguaji wa kesI zote za uchaguzi nchini. Hata awe Lissu ama Mdee ana Mwigulu ama Mwakyembe, once akishatangazwa ni mbunge, yule anayepinga lazima amshtaki pia AG. Na mbunge yule lazima ashirikiane na ofisi ya AG.So hapo AG ambaye kimsingi watakaoenda mahakamani ni wale wasaidizi wake na sio yeye lazima akaitetee serikali na yule mbunge ambaye by then ni mshindi.
 
Tulia tuu mzee vijana wameamua hivyo wamechoka na tabia yako ya kusema ndiyooooo bungeni
 
Back
Top Bottom