Abasi Mtemvu acha utapeli wa kujifanya unawatafutia vijana ajira uarabuni

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,841
ImageUploadedByJamiiForums1402418283.299187.jpg

Mimi nimekuwa nikipinga siasa za kipuuzi zinazofanywa na wabunge wa CCM,kwa mfano huyu mbunge wa Temeke Abasi Mtemvu amekuwa akijifanya anatafutia vijana ajira nje ya nchi Lakini kimsingi ni kama anawauza tu huko kwa washikaji zake na kwa masilahi yake binafsi.

Nimefuatilia muda mrefu zoezi hili nilichogundua ni kuwa Mtemvu kwanza ni mdini sana, 99% ya watu anaowapeleka huko ni waisilamu wenzake.99% ya anaowapeleka huko ni wanawake mbona si wanaume?

Zoezi lenyewe analifanya kutafuta huruma ya kisiasa na utapeli ili 2015 watu wampe kura.

Kwa taarifa tu jimbo hilo mwakani litakuwa chini ya CHADEMA hata mkiwarubuni wanachi kwa njia zote.

Aingi akilini badala ya kupambania maji afya na elimu yeye kutwa kucha kuuza watu huko uarabuni kwa kigezo cha kuwatafutia ajira.

Huu ni utapeli wa wazi kabisa na haukubaliki hata kidogo.
 
Mimi nipo kwenye huo mstari kwamba mwakani jimbo litakuwa la cdm..mkuu unaijua temeke na viunga vyake vizuri..!? cdm inafanya mkakati wowote wa kuandaa mazingira ya ushindi yaani inao wapigakura..au itatumika tu nguvu ya uma bila mikakati..?! Maana solution ya mambo kama hayo ya human trafficking ni kumng'oa pale.. temeke je mikakati ipo.?!
 
Mkijipanga vizuri hiyo biashara ya binadamu ndo itakayomung'oa 2015. Ukipata akina mama wawili ambao watoto wao wameuzwa uarabuni na hawajawaona kwa miaka 5, au vijana waliowahi kuuzwa na wakabahatika kurudi...Unawasomesha, then unatinga nao kwenye mikutano ya hadhara... Pia pata documentary ya BBC kuhusu madhira ya wafanyakazi wa ndani uarabuni., irushe mkutanoni...Nakwambia lazima ang'oke..!
 
Hizo fitina mkuu zinaruhusiwa kabisa
Kikubwa huyo jamaa akapumzike anapopajuwa
Wanaume waingie kazini temeke ibadilike.
 
Mimi huyu jamaa kinachonikera kila siku wanaotafutiwa ajira ni waislamu tu! Je huu si uchochezi wa kidini kweli?Serikali imelala usingizi wa pono,migogoro ya kidin ikiibuka ndiyo wazee matumbo akina Wasira utawaona na porojo kibao huku kwa sasa wanajifanya wamefumba macho!
 
post yako nzur ila umeka udin. Kama kwel anawatafutia ajira nampongeza sana anaisaidia serikal.
 
so ni tapeli ambae anawauza mabinti sio?
wakati huo huo hao wanaouzwa huko unataka haki ya dini zote wawepo?

na unasema anafanya zoezi ili apate kura sio?
la kuwauza wapiga kura?

wewe unajua unachoongea au unabwabwaja?
 
mtoa mada na baadhi ya wachangiaji wenye mihemko ya Udini, chungeni ndimi zenu usiwe mwepesi wa kurusha tuhuma za udini kama hupendi udini, yawezekana una lengo zuri kutujulisha anachokifanya lakini kuchochea udini sio. Kila mtu akimtuhumu kiongozi kwa imani yake jamii hatutaelewana, tunaishi sehem moja watu wa dini tofauti, tukishatofautiana na kupingana ni dhahama mtaani. Unaeza ona ni rahisi kuzungumza lakin madhara yake ni makubwa.
 
unajichanganya kwenye uzi wako.
anafanya kwa maslahi binafsi halafu ni mdini anawachagua waislamu tu. unamaana anawachukia waislam ndo maana ameamua kuwatumia kwa maslahi yake binafi?
anachagua wanawake tu, je hao waislam wanaume umewaweka wapi?
Naona chuki tu kwenye huu uzi wako. Upuuzi kabisa.

View attachment 164052

Mimi nimekuwa nikipinga siasa za kipuuzi zinazofanywa na wabunge wa ccm
Kwa mfano huyu mbunge wa temeke Abasi Mtevu amekuwa akijifanya anatafutia vijana ajira nje ya nchi
Lakini kimsingi ni kama anawauza tu huko kwa washikaji zake na kwa masilahi yake binafsi
Nimefuatilia muda mrefu zoezi hili nilichogundua ni kuwa mtevu kwanza ni mdini sana
99% ya watu anaowapeleka huko ni waisilamu wenzake
99% ya anaowapeleka huko ni wanawake mbona si wanaume
Zoezi lenyewe analifanya kutafuta huruma ya kisiasa na utapeli ili 2015 watu wampe kura
Kwa taarifa tu jimbo hilo mwakani litakuwa chini ya chadema hata mkiwarubuni wanachi kwa njia zote
Aingi akilini badala ya kupambania maji afya na elimu yeye kutwa kucha kuuza watu huko uarabuni kwa kigezo cha kuwatafutia ajira
Huu ni utapeli wa wazi kabisa na haukubaliki hata kidogo.
 
mkuu nahisi huyu jamaa ni taahira. ninachokiona hapa ni chuki tu hakuna chochote.

so ni tapeli ambae anawauza mabinti sio?
wakati huo huo hao wanaouzwa huko unataka haki ya dini zote wawepo?

na unasema anafanya zoezi ili apate kura sio?
la kuwauza wapiga kura?

wewe unajua unachoongea au unabwabwaja?
 
unajichanganya kwenye uzi wako.
anafanya kwa maslahi binafsi halafu ni mdini anawachagua waislamu tu. unamaana anawachukia waislam ndo maana ameamua kuwatumia kwa maslahi yake binafi?
anachagua wanawake tu, je hao waislam wanaume umewaweka wapi?
Naona chuki tu kwenye huu uzi wako. Upuuzi kabisa.

kaomba nafasi akakosa wengine wakapata Ndio mana chuki zimemjaa.
 
so ni tapeli ambae anawauza mabinti sio?
wakati huo huo hao wanaouzwa huko unataka haki ya dini zote wawepo?

na unasema anafanya zoezi ili apate kura sio?
la kuwauza wapiga kura?

wewe unajua unachoongea au unabwabwaja?

hana analoweza kulijibu; chuki zinamsumbua Japokuwa anajaribu kuzificha.
 
Ni ukweli pekee ndio utakaoumaliza uongo,uongo haumalizwi kwa uongo.Nichukue nafasi hii kumpongeza bravo braza AM kwa ubunifu,huu ni ubunifu ambao kila mbunge anapaswa kuwa nao katika kuwaondolea kero wapiga kura wake kwa jitihada za nje ya budjet.AM anastahili pongezi na si kutukanwa na kuvurumishiwa matusi kwa mazuri anayoyatenda.Ni nani asiyejua kuwa asilimia 92 ya wakazi wa jimbo la temeke ni waislamu?ni nani asiyejua kuwa aslimia zaidi ya 50 ya wakazi hao wa temeke wameishia darasa la saba na sekondari? na ni nani asiyeujua ukweli kuwa nchi za bara arabu zinatoa ajira nyingi za wafanyakazi wa majumbani na vibarua?Hivi AM ana kosa gani kuwakusanya vijana wa kike wahanga wa kukosa ajira na kuwapeleka bara arabu kwa kipato cha ujira wa kati? wa kati ya dolla 700 na 500?madereva wengi kutoka temeke wamenufaika kwa initiative hii,vijana wetu wa kike leo wanarudisha fadhila kwa wazazi wao kwa sababu wana kipato.Kwa taarifa tu ni kuwa waislamu wahindi ndio wanaoongoza kufanya kazi za vibarua na majumbani dubai,oman na kwingineko wametengeneza chumi za nchi zao kwani dolla zinarudi nyumbani kila mwezi.katika dunia ya sasa ajira nchi za nje ni mkakati wa kila nchi katika kukuza uchumi,unapokuwa na kundi la watu wanaofanya kazi nje basi unahuisha uchumi kwa kuwa mpokeaji wa fedha za kigeni,pia watu wanapata ajira na ndugu na jamaa wanaboreshewa maisha .pia wafanyikazi wa nje hupenda kuwekeza nyumbani na hivyo huongeza ajira zaidi na kuinua uchumi,Hivi kwenye kaya 100 za waislamu ukitangaza vijana wajitokeze na wakajitokeza waislamu wote unaahirisha na kutafuta wakiristo wasiojitokeza? ipo mifano ya vijana wa kikiristo kujitokeza na wazazi wao huwakataza kwa kuchelea kuwa wakienda bara arabu watabadilisha dini na kuwa waislamu,je hili nalo ni kosa la AM?HONGERA ABBAS MTEMVU kwa kuona mbali.
 
umeandika ukweli mno , binafsi ninao uhakika kwamba wengi wa wasichana wanapelekwa uarabuni kufanya kazi za ndani , kama vile KUFUA NEPI ( ZA WAKUBWA NA WATOTO ) , KUSAFISHA VYOO NA KUDEKI , INASEMEKANA HAWARUHUSIWI HATA KUPIKA ( MAANA WANAONEKANA NI WACHAFU ) , UCHUNGUZI UNAENDELEA .
 
so ni tapeli ambae anawauza mabinti sio?
wakati huo huo hao wanaouzwa huko unataka haki ya dini zote wawepo?

na unasema anafanya zoezi ili apate kura sio?
la kuwauza wapiga kura?

wewe unajua unachoongea au unabwabwaja?

kama serikali isipoingilia hili jambo , WASICHANA WENGI SANA WATADHALILISHWA .
 
kaomba nafasi akakosa wengine wakapata Ndio mana chuki zimemjaa.

ni vema ukafanya utafiti kwanza kabla ya kukurupuka , usisubiri mpaka dada yako apate matatizo ndiyo uamini , wadau wameleta habari humu ili tuzichambue badala ya kumsakama mtonyaji , YAANI HUKO KUNA KAZI ZA NDANI TU , ZA VIWANDANI AU MAOFISINI HAKUNA ?
 
Back
Top Bottom