Abadilishiwa Mtoto Kutoka Wodini Hospitali ya Mwananyamala

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
MWANAMKE mmoja alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada kugundua kuwa amebadilishiwa mtoto wake aliyejifungua kutoka hospitali na kuondoka na mtoto sio wake.

Chanzo cha habari kilisema kuwa mwanamke huyo alifika katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kujifungua.

Tukio hilo la kubadilishiwa mtoto kwa mama huyo lilitokea leo asubuhi.

Inasema kuwa mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike ambaye alimfurahia kwakuwa alikuwa na watoto wa kiume watatu mfululizo.

Wakati mama huyo alipojifungua mtoto huyo wa kike alimpigia mumewe simu akimtaarifu kuwa amejifungua mtoto wa kike.

Hivyo manesi waliomsaidia walimkabidhi mama huyo mtoto wake na kumuhakiki kuwa alikuwa wa kike.

Hivyo katika pilika pilika katika wodi hiyo ya wazazi haijulikani ilikuwaje alijichanganya wakati gani wa kupima kilo za mtoto huyo na kuchukua mtoto si wa kwake ama alibadilishiwa wakati alipokwenda msalani ama ilikuwaje aliweza kubadilishiwa mtoto huyo bila kujitambua.

Muda wa kuruhusiwa uliwadia na mama huyo kumbeba kichanga wake kwa ajili ya kuanza safari kuelekea nyumbani.

Ndugu walifika na kumchukua mama huyo, wakati wapo ndani ya tax kabla ya kuanza safari mmoja wa waliokuja kumchukua kuelekea nyumbani alimfunua mtoto huyo kwaajili ya kumuangalia ndipo walipogundua tofauti hiyo

Ndipo mama huyo aliposhuka na kuelekea sehemu za wodi za wazazi huku akilia kwa uchungu na makelele hadi kupelekea kutokuelewana kwa watu waliokuwa karibu na eneo hilo la tukio.

“Nimebadilishiwa mtoto wangu nimechukua sio wa kwangu, nitafanyaje jamani na nitamwambia nini mume wangu nitaonekana muongo mimi” alilalama mama huyo

Chanzo cha habari kilisema kuwa aliwaelezea manesi na kuanza taratibu za kuhakiki upya kwa kuwauliza wazazi kama kuna mwingine aliyechukua mtoto sio wake.

Hadi Nifahamishe inaamua kuirusha hewani habari hii haikufahamika kama mama yule alifanikiwa kupata mtoto wake ama la, kwa chochote kitakachotokea nifahamishe itawahabarisha.

Chanzo: Nifahamishe.com
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2565206&&Cat=1
 
Lol! Hii ni hatari. Ndo maana kuna umuhimu wa kuwa na mtu mwingine wa karibu ku-monitor mambo yote maana humo mahospitalini hapaaminiki sana. Pole zake, lol, maana sijui anafanyaje sasa maana kwenda kulea mtoto unayejua si wa kwako bila ridhaa yako ni issue.
 
No wonder, wala mi sishangai!
Hawa madaktari na Manesi mbona hizo ni za kawaida kwao?...kwani tumesahau skendo ya hapo majuzi kati ya upasuaji?
Uangalifu hamna, Upendo hakuna, yaani ni kazi ya mshahara, ambayo ni kama vile na wao hawaipendi sijui..!!

Jinsia ya mtoto ni ishu bana... mtu kikosea kwa ishu sensitive kama hiyo ni kosa la jinai!...tuombe Mungu wampate huyo mtoto sahihi, vinginevyo hiyo ndoa iko mashakani. Pia natanguliza pole zangu nyingi sana hiyo couple!
 
kwani watoto hawafungwi vile vidude vina majina yao mguuni au mkononi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom