AAR insurance inapunguza wafanyakazi, wateja hakuna. Mashirika yote ya umma yameambiwa bima ni NHIF

ROho ya kimaskini na ulofa uliotukuka. Inakusaidia nini kumrudisha nyuma aliyeko mbele?

Mimi ningekuona una akili angalau kidogo kama ungezungumzia mwalimu naye atibiwe aga khan na sio kumuondoa aliyepo huko. Kanunue cherehani 4 ufungue kiwanda, maana akili zako zinatoshea kiwanda[/QUO.

roho ya huyu jamaa na mwenyekiti wao wa Chama Ni roho ya wivu, chuki na majungu, wanaombea matajiri wawe masikini kama wao lakini masikini wawe matajiri kama matajiri wengine
 
alafu hyo ni kasumba ya watz wengi sijui y tunapenda kumuona binadam mwenzetu akianguka!!!sijui ni nini jamani yaan ukianguka yanashangilia mxiew
ULOFA, nothing more. Kuna kakitu kanaitwa Inferiority Complexion, ugonjwa huu wa akili una shida mbaya sana maana unaeneza chuki. Mtu hukaa akijihisihisi tu kuwa anaonekana dhaifu au duni, huishia kuwachukia wote anaodhani wanamzidi kwa hili au lile.

Badala ya kulilia haki yake ya yeye kupata huduma ya hadhi ya Aga Khan, anaishia kushangilia wengine wakipokwa haki yao. Mimi sioni sababu ya serikali kuwa ya kiramli ramli namna hii, suala ni kuboresha taasisi zake na sio kulazimisha biashara kukwepa ushindani.

Ile pale Jakaya Kikwete Heart Insitute, ni nzuri, ni BORA. Watu wanamiminika pale kwa wingi, wengine hadi wanatoka nchi jirani. Huduma ikiwa nzuri huhitaji sheria kandamizi wala matamko, watu wataikimbilia wenyewe.
 
japo sipendi watanzania wakose kazi ila nachukia kampuni zinazokula hela za serikali kizembe zembe tu... mwalimu anatibiwa nhif huku mfanyakazi bot anatibiwa na AAR agakhan au best hospitals around the world.

hapa ndipo napomkubali magufuli...

hawa jamaa wamepiga sana hela za mashirika ya uma... wameguswa kidogo wanakimbilia kupunguza wafanyakazi

Wacha kupotosha umma, kupunguza wafanyakazi ni utaratibu wa kawaida kabisaa kwenye makampuni mengi hapa duniani. Kupunguza wafanyakazi inaweza kuwa kwa sababu kama,
  1. Kutoa wafanyakazi wasio na ufanisi kazini pasipo kushitakiwa au kupata mtafaruku kisheria
  2. Kwenda na kasi ya utendaji hasa baada ya kubadili mfumo katika kampuni
  3. Kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni husika
Makampuni mengi ya bima yamepunguza wafanyakazi kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi.

Mleta uzi umekuja na assumption zako zisizo na proof yeyote, thread umeaindika kiushabiki kwa lengo la kupotosha maana.

Hiyo barua umeforwadia, aliyekuforwadia mwambie akupe details zake zaidi.
 
Hawa wahindi wamekula sana pesa zetu, sasa tuimarishe bima ya Taifa Tanzania. Waende tu kwanza wengi wahindi wamejazana.
Hizi ndo roho za kimasikini..
Hao NHIF wangeshindana na AAR ili wapate wateja, sio waletewe wateja wa dezo..
 
Kwanini walazimishe shirika liende NHIF?

Hawaoni watabweteka wakijua watapata wateja tu??
sababu NHIF ni ya umma na mashirika si ya binafsi...
Hawana autonomy kihiiiivyo...

NHIF si mbaya ila kweli wasibweteke...
Si mbaya sababu ela yao inatumika kuboresha hospital zetu akati ela ya hao bima wengine inaenda makwao iwe South au wapi wanajua wenyewe...

Kwa nini tusinunue bidhaa zetu (NHIF)
 
sawa.. ndio maana nimefurahi mwalimu na mbunge wote wawe nhif.. baada ya hapo wataona umuhimu wa hadi mwalimu na nhif wote waende agakhan..

ila umuhimu huo hawawezi uona wao wakiwa bima binafsi... huku walimu nhif
Hutakuja kujinasua kwenye umasikini . MARK MY WORDS
 
sababu NHIF ni ya umma na mashirika si ya binafsi...
Hawana autonomy kihiiiivyo...

NHIF si mbaya ila kweli wasibweteke...
Si mbaya sababu ela yao inatumika kuboresha hospital zetu akati ela ya hao bima wengine inaenda makwao iwe South au wapi wanajua wenyewe...

Kwa nini tusinunue bidhaa zetu (NHIF)
Ni sawa na kulazimisha wafanyakazi wote wa umma wapate ATCL.
Sawa sikatai.
Ila tupo kwenye dunia ya ushindani. Haya mashirika yanatakiwa yapambane ili walete huduma nzuri za kuvutia wateja. Kama makampuni ya simu.
Wakati kabla makampuni ya simu, enzi za TTCL. Kulikuwa na huduma mbovu kupita maelezo. Unatoa hadi rushwa ili uje kuunganishiwa huduma.
Baada ya makampuni mengine kuja, angalia TTCL wanavyosuasua kwa kushindwa ku-cope up.
Vivyo hivyo kwa mashirika mengine ya umma, wanatakiwa wapambane na mashirika binafsi kupata wateja. Hapo ndo tunapopata ufanisi.
Sahivi watabweteka wakijua lazima wateja watakuja kila siku..
 
sababu NHIF ni ya umma na mashirika si ya binafsi...
Hawana autonomy kihiiiivyo...

NHIF si mbaya ila kweli wasibweteke...
Si mbaya sababu ela yao inatumika kuboresha hospital zetu akati ela ya hao bima wengine inaenda makwao iwe South au wapi wanajua wenyewe...

Kwa nini tusinunue bidhaa zetu (NHIF)
Utaambiwa hela zimeenda kujenga viwanda. Shirika halina hela kwa sasa..
 
Utaambiwa hela zimeenda kujenga viwanda. Shirika halina hela kwa sasa..
Kujenga viwanda pia ni kosa...
ziwe ni za afya tuuuu...

nachopendea NHIF ni kukubali kutibu wazazi...
Mashirika mengi wazazi ni no...

Ila hata mimi mwanza nilikuwa siwapendi na nilichukia sana tulipolazimishwa kuamia huko...
Ila sasa ni miaka kadhaa ...nimeshawazoea ... inasaidia sana
 
Mashirika ya umma yana wafanyakazi wangapi na watanzania wasio kwenye mashirika ya umma wako wangapi? AAR wafanye marketing wateja wapo wengi tu.
 
AAR nadhani kupunguza kwao wafanyakazi inatokana na hali ya uchumi kushuka, waliajiri sana kwa kujuana, Sales and Marketing Dept yao imeshindwa kuuza bidhaa zao, Kampuni nyingi za bima zikishaanza kuwa na vi dispensary kama wao wanavyofanya basi kuwalipa third party inakuwa ngumu.

NHIF tayari wanaonekana wamezidiwa mzigo kuna hospitali nyingi hazikubali bima zao mfano Sanitas, Agha Khan na hizi za nje ya miji ndio kabisa.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom