AAR Healthcare (T) Ltd imetangaza kuuza vifaa vyote vilivyopo kwenye kliniki zake saba Nchini kutokana na kufilisiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,858
2,000
Kampuni ya AAR Healthcare (T) Ltd imetangaza kuuza vifaa vyote vilivyopo kwenye kliniki zake saba nchini vilivyokuwa vikitumika kutoa huduma za afya.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kampuni hiyo kutangaza kufunga kliniki zake zote zilizokuwa zinatoa huduma kwa wagonjwa wa nje kote nchini kwa sababu kampuni hiyo sasa imefilisiwa.

Aprili 28, 2021 wafanyakazi wa kampuni hiyo waliandamana katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam wakidai kulipwa stahiki zao baada ya kupata taarifa kwamba kampuni hiyo ilikuwa imefiliwa.

Kwa mujibu wa tangazo katika gazeti la Mwananchi leo Mei 7, 2021 kampuni ya AAR imetangaza kuuza vifaa vyote vilivyokuwa vinatumika katika kliniki saba nchini zilizopo mkoani Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.

AAR ina kliniki tano Dar es Salaam; Posta (City Centre Clinic na New Chato Clinic), Mbagala, Tabata na Tegeta wakati Mwanza iko moja eneo la Mlango Mmoja na Arusha moja eneo la Philips.

Tangazo hilo limebainisha vifaa vinavyouzwa kuwa ni kompyuta pamoja na vifaa vyake kama vile printa, UPS, server na kompyuta mpakato. Vingine ni vifaa vya kieletroniki kama vile friji, projekta, mifumo ya CCTV na vifaa vya kuunganishia mtandao wa intaneti.

Vilevile, AAR inauza vifaatiba kama vile stendi za dripu, vipimo cha mkojo (urine analyzers) na kitanda cha magurudumu kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza au wale wanaopokelewa kutoka kwenye gari la wagonjwa (collapsible stretcher trolley).

Kampuni hiyo pia inauza vifaa vya maabara kama vile mashine ya X-Ray, mashine ya oksijeni, mashine ya kupima shinikizo la damu na kipimio cha meno (dental unit).

Mbali na vifaa hivyo, kampuni ya AAR pia inauza samani mbalimbali kama vile meza na viti vya ofisini, stendi za TV, mashefu, makabati pamoja na mabenchi.

“Kliniki hizo ziko katika viwango vinavyohitajika katika tasnia na viko tayari kutumika. Vifaa vya kudumu vinapatikana kwa ajili ya watua huduma za afya,” linaeleza tangazo hilo huku likibainisha kwamba watakaohitaji vifaa watume maombi kabla ya Mei 17,2021.

Chanzo: Mwananchi
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
MLETA mada umechanganya AAR ni kampuni tofautI na AAR HEALTHCARE (T) LTD naona una uelewa mdogo.

AAR ni kampuni ya bima ya afya wakati AAR HEALTHCARE (T) LTD inamiliki hospitali na clinic ni vitu viwili tofauti hiyo inayomiliki hospitali ndio imefilisika na ni kitu kizuri kwa hospitali kufilisika kwa kukosa wagonjwa ina maana watanzania tumekuwa na afya nzuri hadi corona imetupita mbali ni kitu kizuri lazima hospitali itakosa wagonjwa na kufilisika.

Ni sawa na kampuni ukisikia kampuni kubwa sana iliyoajiri watu wengi sana ya kutengeneza majeneza imefilisika kwa kukosa wateja ni kitu cha kumshukuru Mungu.

NIMEFURAHI SANA KUSIKIA HOSPITALI IMEFILISIKA TUWEKEENI NA ZINGINE ZILIZOFILISIKA NI TAARIFA NZURI SANA.
 
gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,030
2,000
MLETA mada umechanganya AAR ni kampuni tofautI na AAR HEALTHCARE (T) LTD naona una uelewa mdogo

AAR ni kampuni ya bima ya afya wakati AAR HEALTHCARE (T) LTD inamiliki hospitali na clinic ni vitu viwili tofauti hiyo inayomiliki hospitali ndio imefilisika na ni kitu kizuri kwa hospitali kufilisika kwa kukosa wagonjwa ina maana watanzania tumekuwa na afya nzuri hadi corona imetupita mbali ni kitu kizuri lazima hospitali itakosa wagonjwa na kufilisika..
Uliemkosoa ndo yupo sahihi sasa hajaongelea ya Bima kasema AAR HEALTHCARE ili uonekane una uelewa mpana kuliko yeye, mtoa mada yuko sahihi matunda ya mfalme wa chattle.
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,687
2,000
MLETA mada umechanganya AAR ni kampuni tofautI na AAR HEALTHCARE (T) LTD naona una uelewa mdogo

AAR ni kampuni ya bima ya afya wakati AAR HEALTHCARE (T) LTD inamiliki hospitali na clinic ni vitu viwili tofauti hiyo inayomiliki hospitali ndio imefilisika na ni kitu kizuri kwa hospitali kufilisika kwa kukosa wagonjwa ina maana watanzania tumekuwa na afya nzuri hadi corona imetupita mbali ni kitu kizuri lazima hospitali itakosa wagonjwa na kufilisika...
Wakat mwingne usiwaze Sana vyama mkuu

Mbona mleta mada kaandika ulichoeleza wewe

Tatizo unadhan kila anayeleta habar lengo n kukosoa nch hapana jiongeze brother vyama vipo Tanzania itabak kuwa juu Zaid ya vyama

Elewa tu si CCM Wala chadema yenye lengo la kuikomboa nchi hii
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Ulie mkosoa ndo yupo sahihi sasa hajaongelea ya Bima kasema AAR HEALTHCARE ili uonekane una uelewa mpana kuliko yeye, mtoa mada yuko sahihi matunda ya mfalme wa chattle
Na mimi nimemjibu kwa mlengo huo kuwa kufilisika hospitali ni kitu kizuri imekosa wateja sababu sasa hivi watanzania afya zetu nzuri tutegee hospitali nyingi zaidi kufilisika kwa kukosa wateja.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Wakat mwingne usiwaze Sana vyama mkuu

Mbona mleta mada kaandika ulichoeleza wewe.
Sijataja CHADEMA wala CCM nimesema kufilisika hospitali kwa kukosa wateja ni kitu kizuri ni sawa na kampuni ya kutengeneza majeneza kufilisika kwa kukosa wateja
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,687
2,000
Sijataja CHADEMA wala CCM nimesema kufilisika hospitali kwa kukosa wateja ni kitu kizuri ni sawa na kampuni ya kutengeneza majeneza kufilisika kwa kukosa wateja
Mkuu huwa nakufuatilia post zako nying Sana wewe umeweka uchama mbele KUWA PRO ACTIVE Kama mwenzio YOHANA MBATIZAJI
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,785
2,000
Kwahiyo kwako kufilisika kwa hospitali ndo kipimo cha watanzania kuwa na afya nzuri acha uvivu wa kufikirisha akili mkuu.
 
gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,030
2,000
Na mimi nimemjibu kwa mlengo huo kuwa kufilisika hospitali ni kitu kizuri imekosa wateja sababu sasa hivi watanzania afya zetu nzuri tutegee hospitali nyingi zaidi kufilisika kwa kukosa wateja
Acha wafilisike tuu wana huduma ya bei ghali sana harafu watumishi wanawalipa kama vibarua wa ujenzi.

Ila mm nilisema hili neno lako 👇👇👇

(MLETA mada umechanganya AAR ni kampuni tofautI na AAR HEALTHCARE (T) LTD naona una uelewa mdogo

AAR ni kampuni ya bima ya afya wakati AAR HEALTHCARE (T) LTD inamiliki hospitali na clinic ni vitu viwili tofauti hiyo inayomiliki hospitali ndio imefilisika
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,433
2,000
Na mimi nimemjibu kwa mlengo huo kuwa kufilisika hospitali ni kitu kizuri imekosa wateja sababu sasa hivi watanzania afya zetu nzuri tutegee hospitali nyingi zaidi kufilisika kwa kukosa wateja.
Afya nzuri za uchumi wenu wa kati, una wadudu kichwani.
 
Nautico

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
267
1,000
MLETA mada umechanganya AAR ni kampuni tofautI na AAR HEALTHCARE (T) LTD naona una uelewa mdogo.

AAR ni kampuni ya bima ya afya wakati AAR HEALTHCARE (T) LTD inamiliki hospitali na clinic ni vitu viwili tofauti hiyo inayomiliki hospitali ndio imefilisika na ni kitu kizuri kwa hospitali kufilisika kwa kukosa wagonjwa ina maana watanzania tumekuwa na afya nzuri hadi corona imetupita mbali ni kitu kizuri lazima hospitali itakosa wagonjwa na kufilisika.

Ni sawa na kampuni ukisikia kampuni kubwa sana iliyoajiri watu wengi sana ya kutengeneza majeneza imefilisika kwa kukosa wateja ni kitu cha kumshukuru Mungu.

NIMEFURAHI SANA KUSIKIA HOSPITALI IMEFILISIKA TUWEKEENI NA ZINGINE ZILIZOFILISIKA NI TAARIFA NZURI SANA.
Mmiliki wa AAR Insurance na AAR health care ni mmoja mkuu.
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,079

In 2011, the AAR Group’s shareholders resolved to separate the business into two distinct units, AAR Healthcare and AAR Insurance. The insurance wing exited Tanzania in 2019. Kwa hio sasa hakuna tean AAR insurance wala AAR healthcare. Zote mbili ni kaputi. Msijifanye mnajua sana mbambo wakati hakuna kitu. Pata ukweli kwanza kabla ya kupost kitu
 
K.Msese

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,858
2,000
Na mimi nimemjibu kwa mlengo huo kuwa kufilisika hospitali ni kitu kizuri imekosa wateja sababu sasa hivi watanzania afya zetu nzuri tutegee hospitali nyingi zaidi kufilisika kwa kukosa wateja.
vetting yako sijui nani aliifanya, ama ni zao la kamlete..!

haikuumizi wafanyakazi kukosa ajira?

kila kitu ushabiki tu..
una mume kweli?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom