Aanze rais kuhamia Makao Makuu Dodoma, wengine watafuata

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,388
2,000
Wasemaji wamesema, wadadavuaji wamedadavua, wapangaji wamepanga na bado jambo hili limeendelea kuwa hadithi. Serikali ya Tanzania iliamua kubadilisha makao makuu yake tangu mwaka 1976, sasa ni miaka 38, uamuzi huo bado haujatekelezwa.


Kuna wakati Serikali ilijikakamua, ikajenga majengo ya wizara kadhaa mjini Dodoma kwa dhamira ya kuhamishia utendaji wa wizara hizo makao makuu pendekezwa, baadhi ya wizara zilihamia Dodoma, lakini taratibu wizWasemaji wamesema, wadadavuaji wamedadavua, wapangaji wamepanga na bado jambo hili limeendelea kuwa hadithi. Serikali ya Tanzania iliamua kubadilisha makao makuu yake tangu mwaka 1976, sasa ni miaka 38, uamuzi huo bado haujatekelezwa.ara hizo zikajikuta zinarudisha majukumu yake yote makubwa Dar es Salaam.


Serikali ikidhamiria kiukweli, Dar es Salaam inaweza kubaki kuwa Jiji la biashara na Dodoma ukawa ni mji mkuu wa shughuli za Serikali. Serikali ikitaka kufanya hivyo, isiwahamishe watumishi tu wa wizara zake, bali inapaswa kwanza imhamishe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyo akihamia Dodoma kila wizara itahamia tena kwa nguvu zote.


Wiki iliyopita, mbunge wa Chilonwa (CCM), Hezekiah Chibulunje aliulizia tena dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma, yeye alishangazwa na kitendo cha Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Ushirika ambayo ina majengo yake Dodoma, hivi sasa shughuli zake nyingi zimesharudishwa Dar es Salaam. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Sophia Simba alijibu swali la Chibulunje kisiasa, kama ambavyo miaka yote linavyojibiwa kisiasa kwamba dhamira ya Serikali bado iko palepale.


Mbunge mwingine alitoa pendekezo kuhusu nyumba za watumishi wa Ikulu ambazo kwa muda mrefu zinakuwa tupu kwa maana ya kuwa hakuna watumishi wanaozitumia, hoja ilikuwa nyumba hizo ziwe chini ya mamlaka ya halmashauri ya wilaya ya Chamwino ili watumishi wake wapate makazi.


Jibu lililotolewa ni kuwa nyumba hizo ni za watumishi wa Ofisi ya Rais ambao wanakuwapo Dodoma rais akienda Dodoma, hivyo haziwezi kugawiwa kwa taasisi nyingine yoyote ile.


Tunaweza kuangalia safari za Rais Dodoma ni mara ngapi kwa mwaka na huwa anakaa kwa siku ngapi?


Ikiwa idadi ya safari zake ni kidogo na siku anazokuwapo Dodoma ni chache, binafsi sioni haja ya kuwapo kwa nyumba maalumu kwa ajili ya watumishi wa Ofisi ya Rais. Kama haja hiyo ipo, basi ni bora zaidi ikiwa Rais atakuwa anaishi Dodoma.


Rais akihamia Dodoma, ofisi zote za Serikali zitahamia huko, ofisi zote za ubalozi zitahamia huko kwa sababu huko ndiko kwenye kitovu cha nchi na Dar es Salaam litakuwa ni jiji la biashara la kimataifa (metropolitan city), hapo ndipo tutakapoweza kuifanya Dar es Salaam kama Dubai, Hongkong au Tokyo.


Dubai ni mji mkubwa, mzuri na maarufu, ndiko kwenye majengo makubwa ya biashara, ndiko ambako uchumi wa nchi za Falme za Kiarabu unakoonekana, lakini mji wa shughuli za Serikali ni Abudhabi, mji tulivu na mwanana.


Kama mtu anataka kutafakari na kufanya kazi kwa utulivu, Abudhabi ndiyo pahala pake, kama mtu anataka pilika na hamkani, Dubai atakuwa amefika, hivyo si vibaya kuiga watu wa mataifa mengine kwa mambo mazuri waliyofanikisha.


Nigeria nayo iliazimia kuhamisha mji wake mkuu, kutoka Lagos kwenda Abuja mwaka 1976, dhamira hiyo ilikuja kufanikiwa miaka 15 baadaye, lakini cha muhimu ni kuwa wameweza.


Hivyohivyo, Marekani, yenyewe iliondosha makao makuu ya Serikali kutoka Washington DC na kuyapeleka New York, sababu za kufanya hivyo ziko nyingi lakini la muhimu zaidi ni kupunguza msongamano wa mambo katika eneo moja na kulipa eneo lingine nafasi ya kukua na kujitanua.


Ni kweli si rahisi kuhamisha shughuli za Serikali kwa vuu, vuu, lakini miaka 38 si michache kwa mtu kujipanga na kutimiza malengo, Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu Dodoma, CDA, inapaswa sasa ikamilishe mipango yote itakayoiwezesha Serikali kuhamia Dodoma. Hakuna haja ya kusuasua tena, kwani ahadi za kuhamia Dodoma sasa zimekuwa ni ahadi za kuku na vifaranga vyake, kila siku kesho na kesho haifiki.


Binafsi nadhani labda wakati Serikali inaweka mikakati ya kuhamia Dodoma haikuweka muda, ilikuwa ni nadharia zaidi kuliko vitendo.


Wakati umefika sasa wa kufupisha maneno na kuongeza vitendo, ahadi ya serikali kuhamia Dodoma isiwe ahadi hewa. Kipaumbele cha kwanza iwe ni kuhamisha Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu, watu wawafuate viongozi hao Dodoma, hapo ndipo watakapoona ugumu wa kuishi Dar es Salaam na kuwajibika Dodoma, kinyume cha hivyo tutakuwa tunacheza makida makida tu.


Serikali kwa upana wake ikihamia Dodoma, tatizo la foleni jijini Dar es Salaam litapungua. Hivi sasa mfanyakazi anatumia zaidi ya saa tatu barabarani kabla hajafika kazini. Wakati wa kurudi nyumbani tatizo huwa hilohilo, hivyo wengi huamua kutoka kazini kuanzia saa mbili usiku ili kuepukana na foleni.


Hayo ni matatizo makubwa kiuchumi, kijamii na kimaendeleo, watu hutoka nyumbani alfajiri na kurudi usiku, tafiti zinaonyesha kuwa foleni ni sababu mojawapo ya ndoa nyingi kuvunjika.


Wazazi hawapati muda wa kukaa, kucheza na kuzungumza na watoto wao, kila mmoja yuko katika mahangaiko ya maisha huku foleni zikiongeza msongo wa mawazo.


Wana Dar es Salaam hawawezi tena kuhimizana muda, kwani ‘zingatia kufika kwa wakati’ haina maana tena, hata mtu akizingatia vipi, bado foleni itamkwaza, imekuwa vigumu kutimiza miadi kwa wakati. Changamoto za foleni Dar es Salaam ni nyingi zisizoweza kumalizwa na udadavuaji wangu leo, ila nisisitize tu kwamba wakati umefika kwa Serikali kuhamia Dodoma.

Source: Mwananchi
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,177
2,000
Serikali ya Nyerere ilikuja na hoja kama hiyo na ikaanza kuhamia 1973 lakini safari yake ikaja kuzimika ghafla.
Hoja si ukubwa wa mji wa Dodoma,hoja ni huduma,miundo mbinu,na hali ya hewa,madhara na faida ya rift valley.
Bahati mbaya waasisi wa kwanza wenye majibu sahihi kukwama kuhamia Dodoma yaani Chief Adamu Sapi Mkwawa,Sir George Kahama,Rashidi Kawawa na Mwalimu Nyerere wameishatangulia mbele ya haki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom