Aamua kujiua mafisadi wamezidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aamua kujiua mafisadi wamezidi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, Jun 26, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mbona ni shirtcut mno? Huyo dogo vipi! Asijitoe roho bana. Apambane mpaka ushindi. Kujitoa roho ni dalili ya kukata tamaa, kupoteza matumaini, kushindwa vita.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :jaw:
   
 4. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyo kijana nilimuona asubuhi hapo Ubungo, sikujua nini kinaendelea, eh,
   
 5. doup

  doup JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  sifa kwa kikosi cha zima moto na uokoaji; wamejitahidi kuokoa maisha
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  pamoja na kuwapa sifa zimamoto, ambayo nakuunga mkono, lakini laana ziende kwa wote waliosababisha msongo wa mawazo kwa huyo kijana. Tunaye mmoja ambaye ameweza kueleza bayana matatizo yake, je ni wangapi wana matatizo na wanaishia kujiua bila kusema.

  Hivyo ni kweli nchi yetu inashindwa kusomesha vijana wake? Hivyo watanzania wanaJF hii inawezekana kweli katika nchi ambayo ina rasilimali tele. Nani ambaye yuko madarakani aliyesomeshwa na baba yake wote wamesomeshwa bure toka darasa la kwanza mpaka la nane, mpaka sekondari High School na chuoni kwa nini tushindwe sasa wakati katiba yenyewe inasema wazi kuwa elimu ni haki ya msingi???
   
 7. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ..........namuunga mkono kijana Frank!! kwangu mimi ni zaidi ya shujaa! kwa vile system ya nchi hii ilivyojaa unafiki utasikia kauli za kichefuchefu toka kwa 'wenyenchi' dhidi ya 'mwananchi' huyo ilhali wanajua chanzo cha kijana huyo ku-behave alivyo-behave. Ni kweli kwamba wapo wengi sana sana sana sana waliokata tamaa na namna nchi inavyoendeshwa! hakuna matumaini ya hali kuboreka zaidi ya 'kila kukicha afadhari ya jana'. CCM wana tendency mbaya sana ya kupuuzia dalili....kuna matukio hatarishi sana yanayo sign tulipo na tunapoelekea ni kubaya sana. Suicide bombers wanaanza hivi hivi.....just imagine kama kijana yule angepewa mafunzo ya kigaidi na kuahidiwa mapesa kibao na kuelekezwa kuwauwa hao 'mafisadi' wanaotaka kumtoa roho, je angekataa? Tena unakuta JK anawakusanya mawaziri na manaibi wao hotelini katika ulinzi hafifu kabisa (niliwahi kuwaona pale Ubungo Plaza kukiwa na loose security measures). kwenu Usalama wa Taifa, kazi yenu si ku-deal na usalama wa viongozi wa juu tu ila hata kukemea mwenendo m'bovu wa serikali maana mambo yakitibuka hamtakuwa na namna ya kukwepa lawama ilhali mnaona dhahiri trend ya kiusalama nchini from within the citizens.
  ANGALIZO: kama kuna mtu asiyeitakia mema nchi hii, unafikiri akiamua kuwakusanya vijana jamii ya huyo kijana atapata tabu kuwapata? then nini kitatokea?
   
 8. Azikiwe

  Azikiwe Senior Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Kuunga mkono kwa maneno haitoshi, panda na wewe tujue kweli bana.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hii kali!!!

  kama wote wanaopinga mafisadi wakiamua kujiua basi itakua kazi kubwa!!! Hebu na wewe muunge mkono frank kwa vitendo na sie tuko nyuma yako
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lakini mimi nina mashaka na huyu kijana Frank, nahisi kama ana matatizo ya kiakili kwani kwa jinsi alivyokuwa akihojiwa na waandishi wa habari, majibu yake yalinitia shaka.
   
 11. S

  Shelute Mamu Member

  #11
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kijana nilivyomuona pale Ubungo, niligundua kuwa haikuwa nia yake ya makusudi kujiua, maana angetaka kujiua angejiangusha mara moja baada ya kufika kileleni.Lakini alikaa pale juu zaidi ya saa nzima huku akibadilisha mikono kushika nguzo. Hata walipokuja watu wa FIRE walimbembeleza muda mrefu ndipo akakubali kushuka. Nilivyolitafakari huyu kijana ni maroho machafu yalimwingia, na watu MUNGU waliokuwepo pale walioomba sana ili damu isimwagike huku watu wakishuhudia. Naamini kwa ajili hiyo Mungu alisikia Maombi yao. Kuna makabila fulani hapa TZ wanaweza wakakunuiza mtu mwenyewe anakwenda kujitupa kwenye mto au kujinyonga ili ijulikane kwamba amejiua mwenyewe. Lakini Mungu anaonyesha ushindi kwa watu wote wenye mwili ndiyo maana hata huyo kijana aliokolewa - nadhani Mungu amemkusudia kitu maishani mwake.
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kwa waelewa tu.... kama huyo ameamua kujiua.. au kutaka kujiua..... je hawa ambao hawataki kujiua wanataka wafe na nani??? Huyo kaamua kuondoka peke yake, wengine watataka waondoke nao hao mafisi-maji, tunakoelekea siko RAHISI sorry raisi na watanzania wote tuamkeni jamani sasa. Ukiona moshi unafuka.........................................
   
Loading...