Aamua kuishi na nyoka wanne chumbani kwake

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
NGURE1.jpg




Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Peterson Ngure mkazi wa kijiji cha Kiandegwa nchini Kenya, ameshangaza watu baada ya kugundulika kuwa anaishi na nyoka wanne wenye sumu kali chumbani kwake.

Peterson ambaye ameacha shule akiwa darasa la sita, amesema huwa anatumia njia zake za maajabu kuwasiliana na nyoka hao, ambao amedai amewapata kwenye shamba la mpunga jirani na anapoishi.

Habari zinaeleza kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akiwachaji wananchi shilingi 20 za Kenya ambazo ni sawa na takriba shilingi 500 za Tanzania, kwa kila mtu anayetaka kuwaona nyoka hao.

Chifu msaidizi wa eneo hilo Julius Waweru amesema wanakusudia kumchukulia hatua kwa kitendo hiko ambacho si sahihi, na kwamba alishawahi kujaribu kumshawishi kijana huyo kurudi shule lakini juhudi zake ziligonga mwamba, bila kujua anajihusisha na shughuli hiyo ambayo ingeweza kuleta madhara kwa watu, iwapo nyoka hao wangewadhuru watu.
 
Kuna maduka ya kuuza hawa viumbe nchi nyingi duniani, na baadhi ya nchi hizo hawana hawa viumbe bali wanawaiba au kuwanunua kutoka Africa.

Sasa cha ajabu ni kutaka kumchukulia hatua kijana anaewalea lakini airport wanapita kwa misaada ya wakubwa

Ujinga hautakwisha au wanatuona wote mafala
 
Ni bora kuishi na nyoka wanne kuliko kuishi na Zitto kwenye mji mmoja.
 
Hyu nadhani ame fall in love kwa nyoka maana mpaka kaamua kuwatunza ndani yaitaji ujasiri ila Kenya awaishiwi mambo.
 
story yako haikp relevant......nyoka yuko porini jamaa yupo mlangoni kwake....sasa hyo habar tunaaminije
 
hao wanamihemko tu.......sasa mtu inamana hana haki ya kuishi na mnyama anayeona anampenda
 
Back
Top Bottom