A-Z: Wazo langu la biashara lililokamilika kwa kila kitu linalohitaji Mtaji

Feb 27, 2020
6
7
Bila ya kupoteza muda ningependa kuchukua nafasi huu kwenda moja kwa moja kwenye mada husika.

Ninakwenda kufunguka na kueleza kila kitu hatua kwa hatua juu ya wazo hili lilipotokea na kwanini muda huu ni muafaka kulitekeleza
Bila kificho nitaeleza kila kitu kinachohitajika na namna wazo hili litakwenda kutekelezwa..

Kwanza ningependa kujitambulisha by professional mimi ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia ya habari (I. T) nikiwa nimebobea kwenye utengenezaji wa mifumo ya mtandaoni (web application/website) na application za kwenye simu (mobile apps)

Kupitia ujuzi / utaalamu huu nimeona fursa ambayo kama karata zake zikichangwa vizur linaweza kuwa ni wazo lenye kuleta tija.

Wazo hili limejikita katika biashara/huduma ambazo ni common(zimezoeleka) na zinajulikana kwa kila mmoja wetu. Kwa namna ninavyoiona hii fursa ama wazo hili na jinsi ambayo ninataka kulitekeleza linaweza kuonekana ni geni ama gumu kwa baadhi yetu ila naamini wapo kwa uchache wanaofahamu biashara au idea ya namna hili wazo ninaloenda kulitambulisha hapa linavyofanya kazi.


Nadhani kila mmoja wetu anafahamu sekta ya (hospitality) hii industry nimeshindwa kupata jina zuri la kiswahili... ila inatambulika kama hospitality industry.... sekta hii imejikit katik hudum kama malazi, chakula na vinywaji...uandaaji sa mikutano na matukio.. usafirishaji.. matembezi.. hapo ni kwa uchache tu..

Huduma hizi zimekuwa kongwe enzi na enzi.. kwa sababu zisizoepukika kwakuwa kila siku watu wana safiri kutok eneo moja(majumbani) kwenda eneo jingine (ugenini)... ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya msingi yaliyowapeleka huko ugenini... jambo la kwanza ambalo mtu ataliwaza akifika ugenini ni kupata MALAZI...

Na hapa ndipo wazo langu linapochimbukia...

Wengi tupo familiar kuwa kitu cha kwanza kinachomjia akilini anapowaza namna atakavyoweza kukidhi mahitaji ya kimalazi awapo ugenini ni Hoteli au Lodge... nitatumia haya kama mrejeo wa kufanya andiko langu liweze kueleweka..

Its ok.. hotels na lodge zipo.. jee wazo langu linaleta kitu gani cha tofauti?

Ninachotaka kuleta ni kubadili mazingira ya ugenini na kuyafanya kuwa kama nyumbani si kama ambavyo msemo wa "jisikie upo nyumbani" bali ni kwa mazingira kabisaa yawe ni yenye mandhari ya kinyumbani kweli...

Wazo langu hili litahitaji vitu/wahusika watatu.. 1.mgeni (guest) 2.Mwenyeji(host) 3.MFUMO(Platform)

Mgeni ambaye ndiye mtu anayetoka eneo lake na kwenda ugenini anapohitaji makazi ya muda mfupi atajihakikishia uhalali, usalamafaraghana ubora wa mazingira ambayo yameandaliwa kinyumbani kwa ajili yake...

Ili mgeni aweze kujighakikishia hayo yote niliyoyaeleza hapo jii ni lazima kuwepo kwa MFUMO (platform) itakayoaminika kumwezesha yeye kumpatia taarifa zote zinazohitajika.. ili ajiridhishe kwa eneo atakalofikia.

Mwenyeji huyu ndiye mmiliki wa makazi ambaye atatoa eneo lake kwa ajili ya wageni watakaotambulishwa kwake kupitia MFUMO rasmi atakaokuwa anaweka na kujulisha juu ya eneo lake ambalo liko wazi kwa wageni.... mwenyejji anaweza kusimamia mwenyewe nyumba yake au eneo ambalo anataka kulitoa kwa ajili ya wageni... au akakabidhi kwa wamiliki wa mfumo na kusimamia kila kitu kitakachoendelea baina ya mwenyeji na mgeni...
Mwenyeji huyu anaweza kutoa nyumba nzima.. chumba binafsi (private room) kinachojitegemea au kutoa nyumba kwa maana ya kuigawa vyumba vyenye kushirikiana baadhi ya maeneo (shared rooms)

Tumepata character wawili katika wazo hili.. je hawa wahusika wawili wataaminianaje katika kushirikishana, kukabidhiana na kulipata kwa huduma hii ya makazi ya muda mfupi?...

Hapa ndipo anapokuja mhusika wa tatu ambaye ndiye kiunganishi wa hawa wahusika wengine wawili... Naye ndiye MFUMO (Platform)...
.
Kazi ya mfumo ni nini?
Mfumo huu wa kimtandao ndio utakuwa muangalizi muhakiki wa nyumba zote ambazo mwenyeji angependa kuzikodisha kwa wageni.. kabla ya nyumba au maeneo hayo hayajatambulishwa kwa wageni kupitia mtandao... ikiwa nyumba hiyo inakidhi vigezo stahiki.. basi itaruhusiwa kuwekwa wa ajili ya wageni.. aidha itasimamiwa na mwenyeji mwenyewe au itasimamiwa na wamiliki wa mfumo...

pia mfumo au platform hiyo itakuwa na kazi ya kuhakikisha ikiwa wageni watarajiwa ni watu wakuaminika kabla ya kuwaruhusu kuomba makazi ya muda yatakayowekwa na wenyeji kwa ajili yao.....

nini faida ya mfumo huu wa kupangisha makazi ukilinganisha na mfumo tuliozoea wa mahoteli na lodges?

1.Kama ambavyo nimeeleza hapo juu lengo kuu ni kubadili mazingira ya ugenini na kuwa kama y nyumbani kwa kuwa mgeni atapata mazingira yote ya kumfanya awe kama yupo nyumbani kwa kipindi chote atakachokuwa ugenini.. tofauti na mazingira ya kihotel yenye muingiliano mkubwa wa watu...

2.Gharama kuwa nafuu... katika wazo hili mmiliki wa myumba ndio mpangaji wa bei kulingana na ubora wa mali yake na vitu/ huduma ambazo mgeni atajipatia... hata hivyo kwa comparison ndogo ya kimkakati wa masoko.. bei ya nyumba hizi zitakuwa chini kwa zaidi ya 70% ya malipo ya kweny hoteli kwa kulingana na hadhi ya kihuduma...

3.Pia mfumo huu utakuwa murua Kwa wageni ambao watakuwa wapo wengi (kama familia) kuchukuwa nyumba nzima zitakazopatukana kwenye mfumo huu wa upangishaji ukilinganisha na kawaida ya kuchukua vyumba vyumba katika majengo kama mahoteli..

4.Uhakika wa makazi kwa mgeni pindi anapotaka kufanya safari ya kwenda eneo geni ambalo kuna makazi yanayopatikana katika mfumo huu... hapa mtu anaweza kufanya booking yake mapema na kujihakikishia malazi eneo husika hata kabla hajaanza safari yake..

5.Ufaragha na utulivu wa kimazingira ambao hautoingiliana na shughuli kama zifanyikazo kwenye mahoteli kwa kuwa tu mgeni atakuwa katika mazingira private zaidi.. tofauti na. pangilio wa kihoteli wenye muingiliano wa watu wengi katika eneo moja..

Hizo ni faida za uchache za matumizi ya mfumo huu... ukilinganisha ma mazingira ya upangishaji wa malazi tuliozoea...

Hayo ni kwa uchache wa maelezo juu ya namna ninavyoona hili wazo linavyoweza kufanya kazi...

Na kama nilivyoeleza hapo juu mfumo huu ni wa kiteknolojia na nimejitambulisha kuwa mimi ni mtaalamu wa masuala hayo ya kiteknolojia.... Niseme tu kuwa mfumo wote kuanzia WEBSITE MPAKA MOBILE APPS UPO TAYARI

1.Mfumo huu unampa mmiliki wa nyumba ambayo anaamini itafaa kwa kupokeawageni kuiwasilisha na haiwezi kuwa hewani mpaka ithibitishwe na timu kama imekidhi vigezo vyote vitakavyowekwa

2.Mmiliki anaweza kuamua atoehuduma gani kwa wageni na kwa gharama zipi...

3.Kupitia mfumo huu Mgeni ataweza kuchagua nyumba anayotaka kukaa kwa muda fulani kulingana na mahitaji yake... na huduma zinazotolewa

4.Shughuli zote za kutafuta mpaka kufanya malipi ya nyumba ambayo mgeni angependa kufikia zinafanyika katika mfumo huu

5.Baada ya malipo kufanyika na kuwa comfirmed nyumba husika haitaweza kufanyiwa booking kwa tarehe ambazo imeshafanyiwa booking...

6.Malipo kwa mmiliki wa nyumba yatawasilishwa 24 hrs baada ya mgeni kuwasili

7.Mgeni anaweza kutoa malalamiko ikiwa hajaridhishwa na huduma alizopatiwa au alizotaarifiwa ama kama kutakuwa na udanfanyifu wowote kutoka kwa mmiliki

8.Huduma za refund zipo kwa pande zote mmiliki au mgeni kulingana na malalamiko yarakapokuwa yametokea

9.Mmiliki wa mfumo / wenye system watapata commission kutoka kwa kila booking itakayofanyika...

10.Rating na review itakuwepo kwa pande zote mmiliki na mgeni ili kutoa nafasi kwa uboreshwaji wa huduma.. na kuleta uaminifu wa wageni wengine wanaotarajia kufanya booking kwenye mfumo huu

HITIMISHO
Ili mradi wa wazo hili uweze kufanya kazi unahitaji jambo kuu zaidi ambaloni marketing ya kuwafikia wamiliki o. pamoja na wageni ambao ndio wateja wakuuwa biashara hii.. hapa ndipo gharama pekee ambazo ndio kubwa za uendeshaji zinazohitajika... kutokana na ugeni wa wazo hili..

si lazima mmiliki wa mfumo huu awe na makazi bali wenye nyumba wenyewe kwa makubaliano na wamiliki wa mfumo huu ndio watakaotoa makazi yao kwa ajiki ya wageni...

Naomba nichukue nafasi hii kuifikisha kwenu kwa mdau/wadau yoyote/wowote atakayekuwa tayari kushirikiana nami katika wazo hili hadhimu..

Hii ni fursa kwa wawekezaji wenye kutaka mawazo ya kuweza kuwekeza pesa zao. katika miradi mipya..

Nakaribisha maoni mawazo au hata changamoto ambazo wazo hili la biashara linaweza kuwa nazo... TUJADILI PAMOJA......

N.B Marketing strategies gani nilizonazo pamoja na kujua namna shughuli hii itaweza kuoperate pia kiasi cha mtaji utakaohitajika ninaweza kuziweka wazi kwa mtu ambaye nitaona anauelekeo wa kutaka kujishirikisha katika hili wazo... kila kitu nimeshakiandaa....

NARUDIA TENA WEBSITE + APPS ZOTE ZIPO TAYARI

nakaribisha maswali zaidi..
 
Mkuu wazo lako sio baya ila limebase kwenye hisia zaidi...

A rational investor anahitaji numbers kujiridhisha kuwa umelifanyia tafiti wazo lako vizuri.

Numbers kama, market size, market growth, competition, target customer, Break even, ROI n.k...
 
Mkuu wazo lako sio baya ila limebase kwenye hisia zaidi...

A rational investor anahitaji numbers kujiridhisha kuwa umelifanyia tafiti wazo lako vizuri.

Numbers kama, market size, market growth, competition, target customer n.k...
Namba siwezi kuzifungua hapa mkuu...
Huu haukuwa MPANGO WA BIASHARA (business plan)
Business plan ndio inakuwa na kila ktu kuanzia marketing strategies hadi financial analysis..

Nimetoa mwanga wa namna ya nini nimekifanya..
nina system nzima...siwezi kufanya system bila ya namba
 
Sina uhakika kama ni wazo jipya, maana kuna watu wanafanya hilo wazo lako ingawa kwa tofauti na ukubwa zaidi.

Nakushauri ingia Airbnb.com kuna mengi utajifunza.

Jifunze jipange,, tafuta mtaji pambana,, compete na giant waliopo kwenye business. Siyo rahisi ila persistence itakusaidia kutoboa
 
Air bed and brakefast....(AirBnB) sio wazo jipya sana hebu jaribu kuipitia hii website

Angalia business model ya huyu jamaa hamtofautiani sana then angalia ups and down za mapato yake na nini kinacho fanya effect mpk zitokee ups and down kwenye mapato yake.......but kitu muhimu zaidi wekeza kwenye CUSTOMER CARE
 
Sina uhakika kama ni wazo jipya, maana kuna watu wanafanya hilo wazo lako ingawa kwa tofauti na ukubwa zaidi.

Nakushauri ingia Airbnb.com kuna mengi utajifunza.

Jifunze jipange,, tafuta mtaji pambana,, compete na giant waliopo kwenye business. Siyo rahisi ila persistence itakusaidia kutoboa
Ipo moja inaitwa couchsurfing...pakua hiyo app playstore.

ni tofaut na airbnb yaani yenyewe ni bure kwahyo ukitaka kwenda London kupitia couchsurfing utapata wenyeji utakaa bure kwa muda utakao.
hapa bongo couchsurfers wako wengi sana especially dar na Arusha na wanapokea wazungu sana.

hii ishu sio mpya.
 
Sikukatishi tamaa ila ukweli nikwamba dunia ilipofikia haipo tayari kuwekeza kwa mtu mwenye mawazo but inasubii kuona impact ndo iamini uwezo wako ili kushawishika kuweka pesa. Ko saka pesa hata kwa kuwa kibarua ili uje uanze kuishi mawazo yako japo kwa kiwango kidogo na hapo ndo utaushawishi ulimwengu kukusaidia. Hata mimi leo akinifata mtu na mawazo yake hata mia apati ila nimewahi pita mitaani nikashawishika na vijana wanajituma na kutamani kufanya nao kazi
 
Namba siwezi kuzifungua hapa mkuu...
Huu haukuwa MPANGO WA BIASHARA (business plan)
Business plan ndio inakuwa na kila ktu kuanzia marketing strategies hadi financial analysis..

Nimetoa mwanga wa namna ya nini nimekifanya..
nina system nzima...siwezi kufanya system bila ya namba

Nini maana ya ‘kufunguka kila kitu’ kama ulivyoahidi huko juu!
 
Back
Top Bottom