Elections 2010 'A word of mouth' itasadia?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Jamani tujaribu kuwaelezea vizuri marafiki, ndugu na jamaa wa karibu kuhusu ukombozi kupitia Dr. Slaa. Juzi nilikuwa shamba nikaongea na mlinzi wangu mpaka akakubali kumchagua Dr. Slaa na maongezi yalikuwa hivi:

Mimi: Mwaka huu utapiga kura?

Mlinzi: Ndio, lazima.

Mimi: Kwa kusema ukweli wewe utachagua chama au mtu?

Mlinzi: Udiwani Chadema, Ubunge CCM, na Urais CCM

Mimi: Kwa nini Udiwani Chadema

Mlinzi: sina sababu

Mimi: Kwa nini ubunge na urais CCM?

Mlinzi: kwa sababu ni chama kikongwe

Mimi: Kwa muda wote huo wa chama hiki kikongwe hali yako kimaisha inazidi kuwa mbaya au nzuri?

Mlinzi: La! mbaya kweli kweli.

Mimi: Sasa kwa nini usichague atakayekusaidia kwenye elimu ya wanao na kuachana na yule anayesema hatakusaidia?

Mlinzi: ni kweli

Mimi: Ukimchagua ambaye hataboresha hata maisha yangu mimi, mshahara wako hautapanda, unalionaje hili?

Mlinzi: Hapo kweli umesema

Mimi: Sasa toa nafasi kwa maamuzi ya juu yaani kumchagua Mbunge - Mnyika na Rais - Dr. Slaa kwani wana uwezo bila kuangalia chama

Mlinzi: Mzee hii ni kweli

Mimi: Hivi si hata chakula huwa tunabadilisha - dagaa, maharage, ndizi, ugali, wali? Kwa nini isiwe kwenye uongozi?

Mlinzi: Mzee hapo nimekupata - Kura yangu sasa kuanzia udiwani mpaka urais Chadema!

Mimi: hapana usichague chama, yaani utachagua Maganga kwenye udiwani; chagua Mnyika kwenye ubunge, na Dr. Slaa kwenye Urais

Mlinzi: Mzee nashukuru.

Mimi: siku njema.

Du! wapiga kura bila kuwaelewesha bado ni wazito!
 
Huyo ni mlinzi wako lakini wananchi wa kyela walikuwa na ujumbe huu
Waahidi kumpa urais Slaa, ubunge Mwakyembe

Tukio hilo lilikuja baada ya Dk. Slaa kupanda jukwaani na kuwauliza wananchi waliokuwa wamefurika katika mkutano wake wa kampeni ni mgombea gani wa urais waliyekuwa wakimuunga mkono na kwa kauli moja wakamjibu wakisema ‘ni wewe Dk. Slaa’ na ilipofika katika ubunge wakamjibu kwa sauti ya pamoja ‘Mwakyembe’.
 
Back
Top Bottom