A trip of a lifetime: Sign the Petition to show your support! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A trip of a lifetime: Sign the Petition to show your support!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 19, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kwa muda nimeungana na waandishi wengine katika kukemea mauaji ya Watanzania wenye matatizo ya kijenetiki ya upungufu wa rangi (Albino). Wapo watu wengi na vikundi vingine ambavyo vinashirika katika harakati za kupiga vita na hatimaye kukomesha mara moja na daima aibu hii ya Taifa letu na vitendo hivi vya kinyama dhidi ya binadamu wenzetu.

  Kwa muda nimekuwa nikizungumza na watu mbalimbali nyumbani na wengine nao wamekuwa wakifanya hivyo. Hatimaye kundi hili la watu mbalimbali ambao wote tumeguswa na vitendo hivi tumeamua kuunganisha nguvu zetu, vipaji vyetu, na resources zetu kufanya kitu ambacho kitakuwa ni cha kihistoria.

  Baadaye mwezi ujao taasisi kadhaa zisizo za kiserikali kutoka US na Canada na zilizoko Tanzania zikiongozwa na Chama cha Maalbino Tanzania zimeandaa safari maalumu ya kuonesha mshikamano na ndugu zetu Maalbino wa Tanzania kwa kutumia elimu na pia kutoa misaada mbalimbali ili kufanya maisha yao yawe ya amani, utu na usalama zaidi. Katika kufanya hivyo:

  Kuna petition ambayo ilianzishwa na Mtanzania mwenzetu Pius Pius Mikongoti na taasisi ya "Under the Same Sun" kuichukua na kuifanya ya Kimataifa. Nimezungumza na baadhi ya viongozi wa taasisi hizo na natarajia weekend hii kufanya mazungumzo zaidi na kutoa kila ya msaada uliomo katika uwezo wangu kuweza kufanya trip hii kuwa muhimu.

  Ninachoomba kwa leo ni kitu kimoja cha pili nitasema tukikamilisha mazungumzo na kundi tunaloenda nalo nyumbani kwenye tripu hii ya kihistoria. Ninachoomba leo ni kuwa tembelea site ya UNDER THE SAME SUN na utie sahihi Petition ukionesha kukubaliana na mambo yafuatayo. Orodha hii inatarajiwa kukabidhiwa kwenye tripu hii kwa viongozi wa serikali (bado hatujajua for sure nani atakuwepo nyumbani kuipokea):

  1. Declaring my support for and solidarity with persons with albinism living in Tanzania during this time of dire crisis within the albinism commmunity.
  2. Reminding persons within the Tanzanian albinism community that they are NOT ALONE and that many throughout the world are standing with them in defense of their fundamental human right to safety, security and freedom.
  3. Calling on the Government of Tanzania to ensure that the 173 detainees presently in custody as suspects in the savage murders of at least 28 albinos during the last 18 months be brought before the courts and that those found guilty be prosecuted to the fullest extent of the law.
  4. Asking that the Government of Tanzania provides resources to the albinism community in terms of public education and protection with the goal to reduce the crippling discrimination albinos experience in their schools and communities.

  Tafadhali usitoe thanks kwa post hii; ila kama unaona ina maana tia sahihi petition! And if you really care, usisite kuituma kwenye mailing list yako au kwa wabongo wengine. We need to make this OUR (Tanzanians) campain na hawa ndugu zetu toka US na Canada wamekuja kutuunga mkono. Can we do that?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Zungumzeni, lakini msisahau kutia sahihi kuunga mkono harakati za kukomesha mauaji ya Albino. Hapo ndipo tofauti ya wazungumzaji na watendaji inapoonekana.
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,

  Kwa bahati mbaya sana sio utamaduni wetu kutenda; utamaduni wetu ni kuzungumza.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I know that part, I'm trying to prove myself wrong. Believe me I know JF ni wazungumzaji sana ikifika kwenye things that real matter usishangae ukajikuta peke yako. But well, kuna wakati mtu lazima uwe tayari kusimama peke yako. Kuna watu hata hivyo tayari wamesaini na hawa wametenda.
   
 5. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu MMM, nice move!! Cha kushangaza ni kwamba NGO iliyoanzisha idea nzima ipo Canada, sasa jamani hizi NGO mingi hapa mjini zinazosema zinashughulika na kutetea haki za binadamu wanangojea nini??

  Ni hatua nzuri nami nawaomba wana JF tuweke nguvu katika kusukuma swala hili kwani kele na maneno ya watu mwisho husababisha/kupelekea kupata matendo!!

  Mungu Ibariki JF, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika!!
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  M.M

  Kuna zaidi ya hio mpaka watu wasitende?
   
 7. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  duh yaani tusitoe thanks kwenye thread?. Mod naomba mwongozo wako. kwi kwi kwi (just trying prove my sense of humour)
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tuungane kwenye hili ndugu wabongo
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  natumaini watu waliochungulia humu wote wameenda kutia sahihi it takes you less than a minute ukichapa kwa haraka na 3 minutes ukiwa unadonyoa
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  MMKJJ,

  ............mimi Ogah naungana na wale woote wanaolaani vitendo viovu wanavyofanyiwa ndugu zetu hawa.......naenda kuweka sahihi yangu.........
   
 11. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji lakini lazima ufahamu kwamba kwa kusign hizo petition watu tunajicommit kutoa identity zetu ambazo zitakaa kwenye database zenu, kwa hiyo tunataka utoe kauli ya kutuhakikishia kwamba identity zetu zipo safe na hutazitoa kwa upande wa pili(iwe ni serikali au mtu yeyote) kwa namna yoyote isiyohusiana na malengo ya Charity hiyo!!!!!.
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  aibu kwa taifa linaloshabikia uchawi na ushirikina, aibu mno!
   
 13. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2008
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Thanks MKJJ for this information. I have always been in support of the Albinos' existence and protection. I have thus signed the petition and forwarded the wesite to other Tanzanians in my mailing list.
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mimi nawaruhusu wapeleke identity yangu halafu tuone watanifanya nini. Hawana cha kufanya sana sana ni vitisho na fitina lakini kwa sasa mambo yamewaendea kombo. Hebu angalia, Nape na sasa Sofia Simba, eti kosa lake alisema MAFISADI wasishangilie dawa zao ziko jikoni lakini tutaendelea kuwamega na kuwapata wengi zaidi
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Sep 21, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  gamba la nyoka, katika hili identity zetu si muhimu; majina ya wote waliotia sahihi yatapelekwa kwa uongozi wa serikali ili kuonesha mshikamano. Katika hili hakuna kujificha au majina bandia.
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wanaojirodhesha si wote wanaotoka JF na kwa wanaotoka JF kama mimi nikiandika Juma Makulaji, utajuaje kama ndiye mimi Halisi wa JF? Inawezekana mtu kweli akatumia njia ndefu kujua, lakini ili iweje? kwanza hawezi kukuchukulia hatua zozote za kisheria maana yeye atakuwa amekiuka sheria kufanya aliyoyafanya. Kama ni kwa Usalama wa Taifa, hata hapa JF kuna masharti japo watu wanakiuka mara kadhaa, lakini kwa ufupi ni kwamba hata JF hakuna atakeyekuruhusu kufanya uhalifu ndani ya jukwaa lolote, kwa hiyo hakuna uhalifu japo kuna UHURU mkubwa wa kuandika na kusoma
   
 17. Pope

  Pope Senior Member

  #17
  Oct 30, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuna haja ya kuficha jina kwenye hili kwani nadhani hapa ndio umoja na auti ya wengi itasikika niambie kama nia ni kukusanya sahihi 100,000 kweli wataanza kuangalia Mwanakijiji ni nani na yuko wapi na anafanya nini?
  Sidhani sema la msingi ni hakikisho kuwa hazitatumika kinyume na matarajio na hilonaomba kuhakikisha kwani hatuna mtazamo mwingine wowote zaidi ya kukusanya signature kwa dhamira husika.
  Asante ndugu mwanakijiji kwa kulivalia njuga hili.
   
 18. LadyMzuri

  LadyMzuri Member

  #18
  Oct 30, 2008
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Thank you for this information, hope many will be doers and not talkers!

  Already signed.

  PS hope people signed end of signing this October, which has only one day left!
   
Loading...