A renown directors speech

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa yamawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa. Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo:
'THE DIRECTOR'S SPEECH '

'Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa, mimi nashauri muwe makini. Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii gharama yake ni kubwa. Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa. Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kupatikana kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.
Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina hatari kubwa mno. Pia unashauriwa kutopiga TiGO kabisa kwani hii inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.
Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari, kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua kupiga kabisa.
Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu zitamaliza chaji, hii si kweli. Hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio inaongoza mawasiliano yote. Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double-skrini. Hizo ni mbwembwe tu. Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya, usidanganyike.
Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi.

Asanteni sana kwa kunipa fursa hii na nawatakieni mawasiliano mema.

NB Fidel huyu jamaa anapendekeza usipige tiGo
 
Back
Top Bottom