Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 15,842
- 20,687
Pole na kazi Mheshimiwa Rais na hongera pia kwa kazi nzuri sana unayoifanya ya kuwatumikia Watanzania,ni kazi nzuri mno,hongera sana.
Naomba pia nijitambulishe Mheshimiwa Rais kwamba mimi ni mtaalamu wa Kilimo ambaye nakerwa na msimamo usioeleweka wa wataalam wetu wengi wa Kilimo unaoashiria kwamba labda wanatumiwa na makampuni yanayojihusisha na GMOs ikiwemo Monsanto,ili kuunga mkono GMOs,huku ikiwa wazi kwamba GMOs hazifai kwa matumizi ya wanadamu.
Kazi hii nzuri unayoifanya Mheshimiwa Rais itakuwa bure, kama afya za Watanzania zitazorota kwa kula vyakula vizivyofaa,kunywa dawa zisizofaa na kwa ujumla kuingizwa kwenye mifumo ya maisha isiyofaa bila ridhaa yao.Mheshimiwa Rais Watanzania wanaumwa,tena wanaumwa kweli kweli.
Sababu kama nilivyosema zipo nyingi,lakini lipo janga la Genetically Modified Foods au Organisms, ambalo limeikumba dunia kwa sasa,na kama nchi yetu isipokuwa makini,ipo hatari kubwa ya kutumbukia pia katika janga hili.Kampuni ya Monsanto ndiyo kinara wa GMOs na kwa historia ya Monsanto,hatuwezi kuiamini kujihusha kwa njia yeyote ile na food sources za Watanzania!
Mheshimiwa Rais, wanasayansi wa kujitegemea na wa kweli wanakiri kwamba GMOs zina athari kubwa kwenye afya za wanadamu na kwa ujumla hazifai kutumiwa na Wanadamu.Wenzetu Marekani kwa sasa wanafanya campaign kubwa, ili vyakula vyote vyenye asili ya GMOs viondolewe mashuleni na mazao ya GMOs yasitumike kwa kuwa wanatambua ubaya wa GMOs.Zipo kesi nyingi Marekani kwa sasa zinazohusisha GMOs kwa kuhusishwa na magonjwa mbali mbali.Sina hakika kuhusu msimamo wa serikali yetu kwa ujumla kuhusu GMOs,lakini binafsi naomba tuwe na msimo imara usioyumba wa kupiga marufuku GMOs nchini mwetu.Asante sana kwa msimamo ulio onyesha kwenye swala la uzazi wa mpango,na naomba sasa uhamie kwenye GMOs,ili yale yanayowakumba mama zetu yasiwakumbe Watanzania kwa sababu ya matumizi ya GMOs.
Mheshimiwa Rais nimeambatanisha video inayo onyesha kwa undani sana ubaya wa GMOs.
Kwa kumalizia, naomba Mheshimiwa Rais nikufahamishe kwamba tafiti zinazotumiwa kuhalalisha matumizi ya GMOs, zinafanywa na makampuni yanayojihusisha na GMOs na hakuna independent verification by independent scientists,kwa hiyo recommendations za makampuni hayo haziwezi kuwa trusted.
Asante sana kwa kusoma bandiko langu Mheshimiwa Rais.