A Nexus of a Strike: Kinachogombaniwa na madaktari ni jambo kubwa zaidi - tutawaliwe vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A Nexus of a Strike: Kinachogombaniwa na madaktari ni jambo kubwa zaidi - tutawaliwe vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kuna kanuni ya msingi inagombaniwa katika mgomo huu wa madaktari ulioanza tena baada ya kusitishwa kwa muda wa wiki tatu. Kwamba je wananchi wa Tanzania watatawaliwa jinsi ile watawala wanataka au jinsi wanavyotaka wao kutawaliwa? Kwamba, serikali inaweza kufanya lolote na kutenda lolote bila kuulizwa, kuhojiwa na kupingwa na wananchi wake? Je, wananchi wanalazimika kukubali na kupiga magoti ya kuitikia pale "serikali" inaposema jambo moja lifanyike hata kama jambo hilo linaonekana linapingana na maslahi ya wananchi hao? Ndugu zangu, tunachoshuhudia sasa hivi ni wananchi wa Tanzania wakisimama kudai watawaliwe ipasavyo!

  Mgomo huu wa madaktari ni miongoni mwa migomo ya ajabu kabisa kutokea duniani! Toka mwanzo tulionesha kuwa ni mgomo ambao ungeweza kuepukika mapema sana kwa watawala kuonesha heshima, nidhamu na kujali madai ya madaktari badala ya kuyapuuzia na kuwakebehi madaktari kana kwamba Tanzania ni koloni la mafisadi! Madaktari walichohitaji kuona ni uongozi wenye kuonesha heshima, kujali, na kuyapa uzito madai ya madaktari lakini badala yake walichopewa ni dharau na kejeli na sasa wamepewa hadi ubabe!

  Inaendelea kwenye tovuti dada ya JF:

  Mgomo wa Madaktari na udhaifu wa kutawaliwa "wapendavyo" | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  serikali ya watanzania imechoka na haina mbinu mpya zinazokwenda na wakati'wanashindwa kuelewa tofauti ya watanzania wa leo na wale wa miaka 20 iliyopita,kwa kuwa wanafikiri wanafaa kuongoza kuliko makundi mengine itawafanya watanzania kulipa gharama kubwa kuwatoa madarakani
   
 3. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa linaloikumba Tanzania ni kukosa uongozi uliomakini. Serikali iliyopo madarakani imeundwa kishikaji na kwahiyo inaongozwa kishikaji kishikaji tu. President wetu mshikaji na baraza la mawaziri ni washikaji tu. Katika mazingira kama hayo hakuna kitakachoendelea katika Taifa letu. Watanzania tunayo kazi ya ziada kuondokana na hali hii. Mtazamo wa Rais wetu anona heri Watanzania wote wakafa kuliko kujarihu kumfukuza Waziri mmoja tu. Hii inatokana na serikali kujaa washikaji wa Rais. Watanzania kazi tunayo Mungu akae upande wetu kuepusha madhara makubwa yanayokuja mbele yetu.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi tunajua wazi kuwa watawaliwa nao wana sauti! Tumegundua kuwa baada ya uchaguzi haina maana wananchi wanatakiwa kukaa pembeni na kusubiri miaka mitano ipite ndio waje kuuliza "walitawaliwaje"?
   
 5. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni wadanganyika na ujinga wetu hakuna asiyejua kuwa serikali sio sikivu kama wanavyojisifu ndo tufaham kuwa uroho wa madaraka, ufisadi ni afrika nzima hatuna utawala bora.

  Jiulize wapi Mwinyi na gongo la mboto, malima na ngeleja kama wadanganyika tumewawajibishaje mpaka sasa na nkya na mponda unadhani ni kwann hawataki kujiuzuru?
   
 6. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tatizo kubwa linalojionesha hapa ni kuunda utawala kwa kufuata itikadi za umimi na urafiki badala ya kuangalia uadilifu, weledi na uelewa katika kile unachomtwisha ama kumtaka mtu akakifanye. Unapokuwa na kundi la watawala wanaoangaliana katika urafiki na ubinafsi wao zaidi inakuwa vigumu na pengine haiwezekani kabisa kuelezana ukweli pale linapotokea tatizo na mwisho wa siku ni mambo kwenda ndivyo sivyo.

  Katika sakata hili la madaktari Rais anashindwa nini kumwajibisha waziri na naibu wake ili kuweka mazingira bora zaidi ya kupata suluhu. Ama Rais anaamini kuwa bila Dr. Mponda na Dr. Nkya wizara haitaweza kutekeza wajibu wake. Ni lazima Rais atambue kuwa huyu waziri na naibu wake ni watu kama walivyo watu wengine na alichokifanya yeye ni kuwapa dhamana ya kuongoza wizara kama Taasisi ya umma na kuwa kuwepo ama kutokuwepo kwao hakuondoi dhana halisi ya wizara hiyo.


  Kitu kinachofanywa sasa na viongozi wetu wa juu ni kujazana kiburi na sasa imefikia mahali viongozi hawa wanajiona kama Miungu watu na kuwa wao ndio Tanzania na hakuna anayeweza kuhoji lolote kwa yale wanayoyafanya.
   
 7. b

  bilabaye Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Tatizo kubwa ni Watanzania wenyewe. Umma unasubiri nini kuwaunga madaktari mkono!
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Umesema kweli mkuu lawama zote hizi ni zetu kwa kuchagua watu wasiofaa kuongoza natumaini 2015 tutachagua kwa weledi na sio mazoea!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hata kama wananchi wamefanya makosa kuchagua viongozi wabaya hii haina maana viongozi hao basi watawala wapendavyo; wananchi wakigundua makosa hayo wanayo haki ya kulalamika na kuishinikiza serikali ibadili mwelekeo wake.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hata mimi ndio ningekuwa Kikwete, I'll would never bow down to pressure ya madaktari kumtimua Dr. Mponda na Dr. Nkya ili kuepuka kuweka precedence ya weakness dhidi ya undue pressure!.

  Yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, sasa itakuwaje apokee amri kutoka kungine?. Akitekekeza hii amri ya madaktari, itafuatia amri ya walimu, then amri ya polisi, then amri ya wafanyakazi wa serikali na mwishowe amri ya wananchi na sisi kujitengenezea Taharir Squire yetu!.

  Sasa ndicho kitafanyika kile nilichosema ule mgomo wa mwanzo!.

  Kwenye thread yangu ya mazuri JK nimemsifu ni mtu mwenye upendo na watu na mwenye kukumbuka fadhila yaani appreciative person wote waliomsaidia amewakumbuka. Kwa vile Dr. Mponda ni chaguo lake binafsi, you never know walitoka nae wapi?. Hata Mama Nyoni na Jairo wanasubiri kwenda ubalozini!.

  Katika thread ya mapungufu ya JK nimesema JK ana upendo na huruma iliyopitiliza hivyo kugeuka weakness!, kama aliweza kuyasamehe majizi ya EPA kwa kuyahurumia tuu, kwa nini amwadhibu Mponda na Nkya?!. Itakuwa ni kuwaonea bure!.

  Madaktari kama wanagoma tena, na wagome tuu, watu kama watakufa na wafe tuu!, but this time cha moto watakiona na belive me someone must be held accountable!.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Bilabaye, umma gani unaouzungumzia?. Sisi sio kama waMisri, waTunisia au Walibya!. Sisi ni watulivu, watu wa amani, wanyenyekevu na watiifu kwa serikali yetu!.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280

  SIJAWAHI ONA HOJA DHAIFU ZA UTETEZI KAMA ZAKO PASCO. Does it says much about you?
   
 13. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Napita nitarudi baadae maana kila nikisoma uzi wa mgomo huu nazidi kupata hasira na vidonda vya tumbo.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Mojawapo ya fallacies zinazoenezwa sana ni hii ya "kutengeneza precedence"; ni fallacy inayojuliakana kama ya "sleepery slope". Kwa kweli ni fallacies zinazovutia hata watu makini. Madaktari wamegoma ni kweli lakini wenye kuwa held accountable wanatakiwa wawe serikali!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni kweli nyinyi ndivyo mlivyo lakini wengine hawako hivyo; madaktari wameonesha kuwa hawako hivyo na wapo watu wengine wanaoendelea kuwa hawako hivyo. Hivi serikali iko juu ya wananchi?
   
 16. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa tulilonalo watanzania ni kutokujua nini cha kufanya kwa nyakati kama hizi. Na kwawanao jua chakufanya ili kuishinikiza serikali tuliyoiweka wenyewe nao hawajui waanzie wapi na hawana uhakika kama watapata support ya wasiojua chakufanya, baada ya hapo hofu na woga wakutopata support inatufanya tuishie kuongea (kulalamika) bila kujua chakufanya.

  Kizazi hiki kinaongea na kulalamika, kizazi kijacho kitakua kimechoka na kitaamua kufanya jambo bila kujali matokeo mabaya.

  Mimi naamini wengi tunajua kuwa tunatakiwa kwa hili serikali imekosea na tunatakiwa kuiwajibisha. Tuiwajibishe vipi? Nani wakutuongoza? Tupo tayari kuingia gharama?

  LHRC walijaribu nani alitoka? Kulikua na impact gani? Leo hii sidhani kama wapo tayari tena kuanzisha move ile wakiangalia uma uliowaunga mkono.

  Watawala wataendelea kujinufaisha na kunyanyasa mpaka tutakapofikia mahali hatuna pakupumulia, tukifika mahali bora kutoka kuliko na kuiwajibisha serikali kuliko kukaa na kuongea peke yake hapo ndipo ukombozi utapatikana. Nadhani hatujaikia hapo. Mbeya walifikia hapo tukaona kilichotokea. Muda ukifika tutachukua hatua bila kutafuta wakuanzisha wala wakutangulia mbele. Mimi naamini muda bado
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  biashara inaendelea, wauza majeneza wapate faida.
  wauza sanda nao hawabaki nyuma, hitima na arobaini kwenye kila kaya ya mlalahoi ndo itakayogeuza kondoo kuwa kama simba walau kwa siku 1.
   
 18. MANI

  MANI Platinum Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Je wananchi wangapi wanaweza kuliona hilo?
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,501
  Likes Received: 5,612
  Trophy Points: 280
  Viongozi wamezoea kutumia unyenyekevu wetu Watanzania kufanya watakavyo.Kizazi cha unyenyekevu huo kinaondoka na sasa kuna damu mpya zinazohoji! Akina Dr Ulimboka ni vijana waliomaliza vyuo miaka ya karibuni! Kitu ninachoona kutokana na system mbovu Machafuko ndio yatayokuja kubadili mitizamo ya viongozi hawa wa sasa.hakuna anayependa Machafuko na ndugu zetu kufa lakini ndio muelekeo wa nchi sasa! Tuombe asijekuibuka muasi wa msituni ghafla alafu wananchi wakamuunga mkono maana kwa hali ilivyo sasa hata usalama wa nchi upo kwenye rehani!
   
 20. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati ukifika tutabadilisha misamiati. Yupo wapi Mobutu na kizazi chake na vibaraka wake!!? Utajiri sio kitu cha kujivunia wakati wengine wanakufa. Viongozi wakiafrika hawajifunzi!!!
   
Loading...