A New Day for U.S.A -Tanzania Relations : H.E. Samia Suluhu Hassan, President of Republic of Tanzania

3001942_SAMIA_KIJESHI.jpeg
 
Ukurusa mpya wa mahusiano ya pande mbili zinazoheshimiana na kuaminiana kufuatia kukaribiana kwa uwazi baina ya viongozi wa juu wawili yaani Mh. Rais Samia Hassan na Makamu wa Rais wa Marekani Mh. Kamala D. Harris
😍
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sasa serikali yake ipo katika mkakati wa kuiweka Tanzania mahala pake pa ushawishi kimataifa, kama aliokuwa nao baba wa taifa Mwl. Julius Nyerere.

FROM AP ARCHIVE 23 JULY 2015

SYND 19 1 76 NYERERE PRESS CONFERENCE

(18 Jan 1976) Tanzanian President Julius Nyerere at a press conference in Delhi where he says why his country supports the Popular Movement for the Liberation of Angola.
Source : AP Archive

😍
 
LIVE / MUBASHARA :

25 April 2022
District of Columbia

A New Day for U.S.-Tanzania Relations: H.E. Samia Suluhu Hassan, President of Republic of Tanzania

the Wilson Center Africa Program for A Conversation with H.E. Samia Suluhu Hassan, President of the Republic of Tanzania.

President Samia Suluhu Hassan will share her vision for Tanzania and U.S.-Tanzania relations, and sit in conversation with Ambassador Mark Green, President and CEO of the Wilson Center and former U.S. Ambassador to Tanzania from 2007-2009, to discuss key challenges and opportunities for the future of U.S.-Tanzania relations in various spheres.

Source : WoodrowWilsonCenter

Ipo live:
Mh. Rais Samia Hassan anazidi kuelezea masuala mbalimbali ikiwemo demokrasia, uhuru wa Bunge, sekta ya gesi , umeme wa mabwawa ya maji, nishati mbadala wa kuzalisha umeme, upungufu wa mbolea toka Ukraine na Russia ....

Mbali ya changamoto alizozijibu ktk maswali ya mtayarishaji wa kipindi pia, Mh. Rais agusia fursa nyingi zinazokuja baada ya nchi 'kufunguka' kwa dunia toka achukue hatamu za uongozi wa nchi ...

Miradi inayofadhiliwa na Marekani iliyosimamishwa mwaka 2016, sasa 2022 imefunguliwa baada ya mazungumzo ya uwazi baina yake Mh. Rais Samia Hassan na makamu wa rais wa Marekani Mh. Kamala D. Harris hivyo kufuatiwa na ukurasa mpya wa mahusiano ya kufahamiana kufunguliwa baina ya Tanzania na Marekani.

Mh. Rais afafanua sera ya nchi kuwapatia watoto wa kike wanafunzi waliopachikwa mimba kuruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan agusia umoja wa kitaifa unaojengwa chini ya uongozi wake ikiwemo kuachiwa toka mahabusu viongozi wa vyama vya upinzani, kufunguliwa magazeti yaliyofungiwa, bunge kuwa 'live' ili wananchi waweze kufuatilia kinachoendelea bungeni kupitia wawakilishi wao na serikali kujibu kero za wananchi . Kutoa elimu kwa taasisi zinazohusika na utoaji haki kupitia mfumo wa haki jinai (criminal justice system) kama Polisi, Ofisi za Mwendesha Mashtaka, Magereza na Mahakama

Uchumi wa buluu, biashara na mahusiano mapya baina ya Tanzania na dunia ....

Aione Nyani Ngabu

Tena akome kukiponda Kiingereza na Mama Samia
 
Mkuu watu hawapingi hizo safari bali ufujaji na kuhalalisha upigaji, kwani wewe unaishi nchi gani?.
"Ukitaka kula na wewe ukubali kuliwa japo kidogo" JK.
sasa kwa taarifa yako sisi tumekula na tutaendelea kula pakubwa sana,

utalii utafunguka mara dufu na hivyo tutarudisha pesa zote na faida ya kutosha.

Uwekezaji kutoka marekani utaongezeka mara dufu na hivyo kuinua uchumi wetu lkn pia kuongeza ajira.

Masula ya Elimu yataimarishwa, Afya n.k n.k

Ziara ya Rais na ujumbe wake huko Marekani inafaida nyingi sana na endelevu kuliko unavyo fikiria.
 
Kazi inaendelea... Kazi iendelee...
Mungu Ibariki Tanzania.
Wabariki viongozi wake akiwemo Mama.
P
Pascal, hivi unadhani bado ni muafaka kuendelea kuitumia hiyo kauli ya "kazi iendelee"?
Kwa maoni yangu nadhani umefika wakati wa kuachana nayo na kuanzisha slogan mpya. 'Kazi iendelee' ilipoanza ilimaanisha kuendeleza kazi iliyoanzishwa na kamanda JPM. Sasa kwa kuwa JPM siyo mpendwa wa 'watu' tena, na hao walioanzisha 'kazi iendelee' ndio wanamnanga kila siku, mi nadhani umefika wakati sasa wa kuachana nayo na kuanzisha slogan mpya.
Au wadau mnaonaje?
 
Paskali huwa hatabiriki, kuna wakati anaeleweka kuna wakati haeleweki kama ilivyo hali ya hewa
 
Kazi inaendelea... Kazi iendelee...
Mungu Ibariki Tanzania.
Wabariki viongozi wake akiwemo Mama.
P
Kazi itaendeleaje kama Rais wa nchi anaishi magharibi ya mbali? Inawezekana wenzetu wanajiuliza Rais anawezaje kuishi nje ya nchi na nchi ipo ipo tu bila Rais? Kwa hali hii nchi haitaendelea na ndiyo sababu haiendelei, ninajua unajua kuwa wakati tunakabidhiwa nchi Tanganyika na Indonezya zilikuwa zinalingana kimaendeleo, lakini leo sisi tuko kwenye kunyang'anyana kura tu, na kutabiri ushindi ujao utakuwa wa kishindo! Hayo ndiyo maendeleo myajuayo, amka.
Kuna wakati Tanzania ilianza kuamka kimaendeleo, Pugu Road ilichangamka kwa viwanda vyenye tija siyo vya marumaru, Moro, Mwanza, Tanga, Arusha, Musoma, Tabora, Mbeya na Mang'ula kuliinuka kwa viwanda vyenye tija si vyakuunganisha bodaboda toka China.
Hatuwezi kuendelea kiuchumi kwa Rais kuishi nje ya nchi akifanya mazungumzo na machalii.
 
LIVE / MUBASHARA :

25 April 2022
District of Columbia

A New Day for U.S.-Tanzania Relations: H.E. Samia Suluhu Hassan, President of Republic of Tanzania

the Wilson Center Africa Program for A Conversation with H.E. Samia Suluhu Hassan, President of the Republic of Tanzania.

President Samia Suluhu Hassan will share her vision for Tanzania and U.S.-Tanzania relations, and sit in conversation with Ambassador Mark Green, President and CEO of the Wilson Center and former U.S. Ambassador to Tanzania from 2007-2009, to discuss key challenges and opportunities for the future of U.S.-Tanzania relations in various spheres.

Source : WoodrowWilsonCenter

Ipo live:
Mh. Rais Samia Hassan anazidi kuelezea masuala mbalimbali ikiwemo demokrasia, uhuru wa Bunge, sekta ya gesi , umeme wa mabwawa ya maji, nishati mbadala wa kuzalisha umeme, upungufu wa mbolea toka Ukraine na Russia ....

Mbali ya changamoto alizozijibu ktk maswali ya mtayarishaji wa kipindi pia, Mh. Rais agusia fursa nyingi zinazokuja baada ya nchi 'kufunguka' kwa dunia toka achukue hatamu za uongozi wa nchi ...

Miradi inayofadhiliwa na Marekani iliyosimamishwa mwaka 2016, sasa 2022 imefunguliwa baada ya mazungumzo ya uwazi baina yake Mh. Rais Samia Hassan na makamu wa rais wa Marekani Mh. Kamala D. Harris hivyo kufuatiwa na ukurasa mpya wa mahusiano ya kufahamiana kufunguliwa baina ya Tanzania na Marekani.

Mh. Rais afafanua sera ya nchi kuwapatia watoto wa kike wanafunzi waliopachikwa mimba kuruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan agusia umoja wa kitaifa unaojengwa chini ya uongozi wake ikiwemo kuachiwa toka mahabusu viongozi wa vyama vya upinzani, kufunguliwa magazeti yaliyofungiwa, bunge kuwa 'live' ili wananchi waweze kufuatilia kinachoendelea bungeni kupitia wawakilishi wao na serikali kujibu kero za wananchi . Kutoa elimu kwa taasisi zinazohusika na utoaji haki kupitia mfumo wa haki jinai (criminal justice system) kama Polisi, Ofisi za Mwendesha Mashtaka, Magereza na Mahakama

Uchumi wa buluu, biashara na mahusiano mapya baina ya Tanzania na dunia ....
Tatizo ni huko Bungeni, wananchi hawakuwachagua hao waliopo huko. Wote walioko huko walipachikwa na dikteta marehemu Magufuli. Tunatokaje hapo? Hakuna mtu wa kuwafuatilia hao maharamia waliopo bungeni.
 
Back
Top Bottom