A New Call To Action: Tuchangie Chama cha Msalaba Mwekundu kusaidia Waathirika wa Mafuriko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A New Call To Action: Tuchangie Chama cha Msalaba Mwekundu kusaidia Waathirika wa Mafuriko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 21, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280  Japo natamani kusema maneno makali juu ya mafuriko ya Dar najikuta napatwa na mzigo mkubwa moyoni kwa mara nyingine tena. Mwaka Jana Januari tulianzisha Harambee ya kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania kukipa uwezo wa kukabiliana na janga la mafuriko la Kilosa. Kama nilivyosema wakati ule (na kuandika kwenye Gazeti la Tanzania Daima) kuchangia TRC (Tanzania Red Cross) ilikuwa ni kuwekeza kwa majanga ya baadaye kwani hakuna chombo nchini ambacho kina uwezo wa kusaidia wakati wa majanga kama Chama hiki cha Misaada ya dharura.

  Niliandika hivi:

  Makala yote unaweza KUISOMA HAPA

  Sasa matuko haya ya majanga ambayo yanaendelea nchini na kama nilivyoandika kwenye FIKRA PEVU kuwa mvua hii haiishi hadi Jumamosi (Mkesha wa Krismasi) ni wazi kuwa mnachoona kuwa ni madhara bado hayajafikia kikomo chake kwani Jiji letu litapigishwa magoti. Naweza kusema mengi ya kisiasa (Ningeweza kukumbushia mojawapo ya zile makala za "Taifa lisiliojiandaa kwa majanga, limejiandaa kwa maafa"). Lakini kwa sasa najizuia kulipuka (japo ni vigumu). NInatoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya Tanzania kuanza kampeni mara moja ya kuisaidia TRC kukabiliana na majanga haya.

  Binafsi sipendi na siungi mkono sana kupeleka misaada kwa "mkuu wa wilaya" au vyombo vya "serikali". SIVIAMINI KWANI NI SEHEMU YA TATIZO ZIMA LA KUKUBILIANA NA MAJANGA. Tuungane kusaidia Chama cha Msalaba Mwekundu kiwezi kutoa misaada ya kiutu na kibinadamu kwa waathirika. Tusisubiri wapewe misaada kutoka nje ya nchi. Najaribu kuona jinsi gani kama sisi JF wenyewe tunaweza kuanzisha kitu chetu wenyewe kwa ajili ya kutoa misaada ya kiutu - inatosha kulumbana na kubishana lakini zinapotokea changamoto za Kitaifa tuwe pamoja.

  Mimi mwenyewe naweza kuhisi kuwa haya marufiko yatagusa siyo chini ya watu milioni 1 na watu wasitegemee sana misaada mingi ya kigeni hasa kwa vile nchi nyingine nazo zimekumbwa na mafuriko na hali ya uchumi wa dunia ni mbaya sana - ni LAZIMA TUJITEGEMEE KWA KIASI KIKUBWA SISI WENYEWE.

  Kwa wanaokumbuka mwaka jana kwenye janga kama hili tuliweza kutoa misaada ya vitu na mali mbalimbali kwa TRC vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi tukiongozwa na Kamanda Sanctus Mtsimbe na timu nzima ya TPN.

  Wakati tunasubiri to set up a mechanism* napendekeza watu wachangie moja kwa moja kwa TRC - the best option.

  MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
  1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
  P.O. Box 1133 Dar es Salaam
  Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843
  logistics@raha.com


  Nitawajulisha mpango wowote ambao JF tunaweza kuja nao kuweza kutoa misaada yetu. Japo wakati wa kuwakalia kooni na shingoni tena unakuja kuhusu uzembe uliokithiri kuhusu mafuriko haya kwa wakati huu tusaidiane kwanza kuwasaidia watu kwa sababu baadhi ya vitu ambavyo vitahitajika kwa haraka ni:

  Maji ya Kunywa
  Nguo
  Dawa za maumivu (ambazo hazijaharibika)
  Vitu vya Usafi kwa wanawake (female hygienic products)
  Sabuni
  Non-perishable food products (zaidi vyakula vya makopo)
  Vitu kwa ajili ya watoto (nepi, n.k)
  Vyandarua

  * Nadhani kabla ya kesho tutakuwa tumekuja na mechanism ya kuratibu shughuli zetu kama JF kusaidia TRC kukabiliana na majanga haya. Kama kuna mtu ana suggestion ya jinsi gani tunaweza kufanya hivyo please I'm open to hear it.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. c

  chama JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji;
  Tuelezeni namna ya kuchangia; pia ishauri serikali badala ya kutaka kukimbilia kuilipa Dowans; pesa hizo zitumike kwenye maafa yaliyotokea.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Wenye kuiangalia serikali kwa kweli imekula kwao.
  Believe me.. hili la serikali nilishakata nao tamaa - wala kuwaambia kitu chochote sioni sababu.
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mimi nilichangia wakati wa mafuriko ya kilosa lakini sijui kilipatikana kiasi gani na kilitumika vipi.halafu mchango ulikuwa wa mwezi mmoja lakini mimi nilikatwa zaidi ya mwezi husika,haya ni maeneo ya kuangaliwa kabla ya kutoa michango yetu kwa mara nyingine.halafu sijui ile kodi yangu ninayokatwa kwa mwezi ni kiasi gani kinatengwa kwa ajili ya majanga ya kimazingira au zote zinaishia kwenye sherehe za uhuru pekee!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280

  Mbona taarifa zote zilikuwa zinawekwa hapa hadi tulipowasilisha mchango wa mwisho?
   
 6. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo la hiki chama cha msalaba mwekundu kikishachangiwa huwa hakileti mrejesho kuwa kimepata kiasi gani na zimetumikaje, sasa watu watakuwa wagumu kuchangia kwani hata kwenye makanisa kama kwa Kakobe watu wanataka kujua zinakusanywa ngapi ndio m,aana wamemburuta kortini.

  Washauri watueleze za Kilosa zilipatiokana ngapi,
  Za Gongola Mboto zilipatikana ngapi


  Na zilitumikaje ili sasa wawe na uhalali wa kukusanya tena michango.
   
 7. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mi nawasiwasi na wale wenzangu wa siasa kali, ile alama ya msalaba ile tena mwekundu italeta tabu kidogo kwao, nawasiwasi kama hawataweka kunji juu ya uchangiaji... kwa walio nje ya tanganyika itakuwaje mzee mwanakijiji?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280

  Unaweza kupata taarifa zaidi hapa za matumizi: Tanzania Red Cross National Society - IFRC
   
 9. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Srkali hii ya ccm ina hela za sherehe tu..watu wako na shida wamekumbatia mikono,,kisa hapo hakuna 10%......
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe changia tu siyo lazima upate auditing report hata kwa issue ya misaada lol
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Napenda kuchangia, lakini naogopa uchakachuzi kama ule wa Kilosa, michango itolewe na wana JF halafu presentation ya michango ifanyike kwa jina la Voda na Clouds. MØ@x!"#¤%&/
   
Loading...