A man from Taured

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,875
2,000
Ilikua siku ya hali ya joto la kawaida ilikua ni July 1954 katika uwanja wa ndege wa Haneda huko Japan ambao ni uwanja wa kimataifa wa Japan ndege kama kawaida na siku zote za shughuli ndege ilishuka na abiria wote wakashuka wakati wa ukaguzi pakatokea hali moja ya sintofahamu kwa afisa wa ukaguzi alimuona mwanaume aliyekua anaonekana kama mwenye ndevu usoni pia alikua ana nywele za kahawia na viini vya blue vya macho alionekana kama mfanyabiashara aliekuwa kavalia suti ya kisasa na tai ya blue na viatu vilivyong'aa sana alikua ni mtu mwenye kujifuta sana jasho kupitia skafu alikua mwenye lugha kama ya machafuko hivi na alipofika alikua mtu mwenye kuongea kifaransa hakuna aliyemuelewa kwa uharaka pia badae alionekana kama alielewa kijapani na lugha takribani 5.Huu ni wasifu wa mtu huyo kulingana na maelezo ya Askari wa ukaguzi

Uajabu wake ulimfanya askari wa ukaguzi katika uwanja wa ndege kumsimamisha na kutaka mahojiano naye kwani alipoambiwa aonyeshe passport zilionekana zimeandikwa ametokea katika nchi inayoitwa Taured ambapo ni nchi ambayo haipo hapa duniani,afisa mshuhudiaji anadai passport yake ilikua imeandikwa kama kwa mfumo wa kiarabu hivi (arabic passport) hii ilimshangaza sana askari mkaguzi na kumuomba aende katika chumba cha ukaguzi ili kumkagua vema,yule bwana alionekana kama mwenye haraka na mwenye kukasirishwa na tukio la kuhojiwa na askari ingawaje alikubali kwenda kwenye chumba cha kuhojiwa,alipofika alikuta mkalimani pamoja na afisa wa ukaguzi ndipo alipoanza kuhojiwa kua ametokea wapi na nchi yake inaitwaje!? Majibu yake yalikua yale yale alidai ametokea katika nchi iliyokua ikiitwa Taured ndipo ofisa alipoona kama hawaelewani aliomba paspoti zake ili apate kuzikagua kuziangalia kweli zilikua zimefuata mfumo wa safari za kimataifa kwani ilikua na stampu na label ya kutokea Taured picha iliyokuwa katika paspoti yake ilikua ni picha ya kijana mdogo hivi (alionekana mdogo kuliko kimuonekano) ndipo afisa wa ukaguzi akaomba vidhibiti zaidi kuhusiana na nchi yake akatoa pesa na kweli zilionekana ametokea Taured lakini alikua na vitu vingine mfukoni mwake kama Sarafu,kura,picha zake ambazo miongoni mwa picha kulikua na mwanamke na watoto katika picha pia alikua na kura za kigeni na pauni

Afisa akapata wazo la kumpa ramani ya dunia ili aonyeshe nchi yake iko wapi ndipo huyu bwana alipoint katikati ya nchi ya Ufaransa na Hispania,lakini alionekana mtu mwenye kuchanganyikiwa sana baada ya kukuta nchi yake haijaandikwa katika ramani ya dunia ambalo ni jambo la ajabu kidogo aliuliza "mbona nchi yangu haipo katika ramani yenu!?" Alisema nchi yake imekua takribani kuanzia miaka 1000 iliopita katika ramani iwaje isionekane siku hiyo (hapo aliwashangaza askari)

Lakini walipoangalia document zake walikuta aliwahi kufika Japan kibiashara mara nyingi tu na walipoangalia mara ya mwisho kufika Japan walishangaa sana kwani document zilionyesha alifika mara ya mwisho mwaka 1986 na 1988 wakati mwaka huo ulikua ni 1954 yaani ilikua bado wapo nyuma na hawajafika miaka hiyo iliyoonyeshwa kwenye taarifa zake,askari walipoona document zake wakaamua kumchukua kizuiani mpaka atakapopatiwa uvumbuzi kua ni mtu wa aina gani huenda alikua mhalifu! Hakuna ajuaye

Wakaamua kumchukua na kumpeleka hoteli ya karibu ili awekwe huko mpaka watakapompatia uvumbuzi wanasema wakati yupo njiani alionekana mdadisi sana na alikua akiongea lugha yake isiyoeleweka kama ya machafuko hivi muda wote mwisho wa siku akakata tamaa akaanza kulia na kulaani alisema "niacheni bado nina shughuli kubwa ya kusaidia ulimwengu huu kabla haujaangamizwa" alilaani sana kitendo cha kuwekwa kizuiani lakini kilio chake hakikufua dafu mbele ya askari wa Japan bado hawakumruhusu kuondoka walihakikisha wanamfikisha hotelini (alidai amechoka sana kwani ana kazi kubwa sana)

Walimweka kwenye chumba kilichokuwa ghorofa ya nane katika hoteli hiyo na ili kupata uhakikisho zaidi waliweka askari wawili mbele ya mlango wa chumba alichokuepo kuhakikisha hatoki humo, document zake na taarifa zote ziliachwa katika kituo hapo airport

Ilipofika asubuhi waligonga mlango ili kumrudisha yule mtu katika mahojiano lakini walishangaa ukimya umetawala wala hakufungua ndipo walipotumia ufunguo wa spea kufungua mlango kwa nguvu ndipo wakakuta chumba cheupe kabisa wanadai palikuwa na harufu yake ndogo sana katika hewa ya chumba hicho askari walidhani alitokea dirishani lakini katika dirisha hilo hapakuwa na ushahidi wala uwezekano wa mtu kutoka na wala mlangoni askari hawakuona mtu yeyote aliyetoka ndipo wakaamua kuwahi kwenye kituo cha Airport kuangalia vitu vyake wakashangaa hawakukuta kitu chochote huko Airport hawakukuta mzigo wake wala passport zake vyote vilitoweka katika hali ya sintofahamu tangu hio siku mpaka leo hakuna anayejua yule bwana ni nani na aliwezaje kutoka katika hoteli bila kuonekana na pia ilikuaje ushahidi wake kupotea katika kituo kule airport ambalo ni jambo lisilowezekana mbele ya askari wa Japan

•Jambo la msingi la kukumbuka alikua akimaanisha nini aliposema "mniache nina kazi ya kuisaidia hii dunia kabla haijaangamia" !?

•Na kwanini alionekana tarehe zake zimetoka miaka ya mbele zaidi kabla hata watu hawajafika miaka hiyo

Kwa kipindi chote pamekua na imani nyingi kuhusiana na mtu kutoka Taured wengine wamedai kua huyu ni Time travel yaani mtu aliyetoka katika future maisha ya mbele

Mamlaka ya Japan walitoa taarifa kua akionekana popote azuiliwe haraka iwezekanavyo lakini hawakumpata tena wala ushahidi wake hawakuuona tena

JARIBIO LA STEPHEN HAWKINGS
Stephen Hawkings aliwahi kufanya jaribio la kuwakamata watu ambao ni time travellers lakini mwisho akagundua hawa watu hawapo kwa sababu:
•Time travellers hudaiwa kua watu ambao wanaishi kesho kabla ya leo yaani kesho wanaishi na wana uwezo wa kurudi kuishi na sisi leo!

•Huyu professa aliamua kufanya jaribio la kuandaa sherehe ya hawa time travellers na katika sherehe yake hakutoa kadi yoyote ya mwaliko wala kumwambia mtu ila aliandaa tu maandalizi na ilipofika kesho yake yaani baada ya sherehe ndo akatoa kadi ya mwaliko lakini ajabu hakufika time travellers hata mmoja hii ina maanisha kwakuwa alitoa kadi ya mwaliko kesho yake yaani baada ya sherehe na time travellers wanaishi kesho kabla ya leo basi wangefika katika sherehe kwa maana hawa time travellers wana lugha yao ya kuongea hivyo kama kweli wapo basi wangepokea ile kadi kesho yake na kuja kwenye sherehe leo hii

Hii ina prove kua hamna uwepo wa time travellers kwa mujibu wa Stephen Hawkings

Jaribio hili unaeza kulifanya nyumbani kwako kwa kuandaa kitu leo bila kumwambia yeyote na kutoa mwaliko kesho ukiona mtu amekuja leo kabla ya mualiko basi ujue huyo atakua time travellers mwenye uwezo wa kusafiri kwa kasi ya mwanga
FB_IMG_1618591854953.jpg
 

Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,066
2,000
Aisee huwezi kabla sijamaliza hii mada kuisoma nikasema lazima waliambulia patupu askari hao,na mwisho wa habari yako ni kweli imehitimisha hivyo.

Almuhimu jambo liko hivyo.

Lugha ya Machafuko ni lugha gani ? Naomba mfano wa lugha hiyo ?

Mimi swali langu ni moja,je unaweza kututhbitishia ya kuwa hili tukio lilitokea kweli au hujafanya utafiti huo ? Maana hili jambo lina maswali mengi sana kwayo yanahitimisha kuwa hii ngano tu za waja wakionyesha umahiri wao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom