A. Mahimbo apeleka pingamizi kwa Pengo dhidi ya Dr Slaa

Mkuu DALLAI LAMA mtu akidai haki yake basi anakuwa anatumika? Hii kitu kwa Dr. Slaa inaonekana kuwa janga. Mahimbo anatumika, Rose Kamili anatumika!

Mkuu kabla ya kuendelea na hizi 'brouhaha' ambazo ninaamini kwa 100% kuwa zina mkono wa CCM wakidhani ni karata ya kuiangushia CDM, mtueleze kwanza ile kesi aliyofungua Mahimbo wakati wa uchaguzi mwaka 2010 kwa msukumo wa Rajab Makamba na kundi lake iliishia wapi?. Je zile hela walizompatia wakati ule zimeishia? wamemuahidi nyingine?.

Hivi tukianza hasa kuchambua maisha binafsi ya viongozi wa CCM na mawaziri kuna mtu atabaki salama. Si bora Dr slaa yeye ameweka wazi uhusiano wake na Josephine na kuamua kufunga ndoa kuliko wale wanaochukua vibinti vya vyuoni na hata kuwapatia madaraka wake za watu na kuwafanya nyumba ndogo zao?.

Hizi ni politics ambazo CCM will be the biggest loser, maana wananchi wanawafahamu na kuwajua viongozi wote wa CCM vizuri sana linapokuja suala la infidelities.
 
Acha uongo huyu jamaa hana mke,unamzushia bure wacha jamaa adahi mke wake,naomba nikuulize swali la kizushi wewe baba yako angeibiwa mama yako ungefurahi?acha kutetea dhambi ya uzinzi,huyo Josephine ni mzinzi!

unataka kuniambia kuwa huyu jamaa mda wote huo alikuwa hagongi mzigo mwingine?
 
Mkuu Nikupateje.
Kwa hakika umenifumbua akili hata mimi. Asante. God blease you.
 
wewe huwa hutumii? Kama hujawahi fanya ngono utakuwa we ni ccm maana ndo WATAKAVITU..pambav.MNATAFUTA SINGO MPYA KUMSUMBUA DR KILA MARA ILA TUMEWAZOEA.


Wewe sasa hapa itikadi za vyama zinakujaje, kwanini hutaki kukubali kuwa Slaa amechukua mke wa mtu na amemtelekeza mzazi mwenzie?
 
It just a delay tackicks!lilopangwa limepangwa huyo mahimbo na kamili madai yao hayawezi mnyima usingizi Dr.
 
matatzo yote anayataka huyu mzinzi slaa kamkimbia demu wake rose kamili kamchukua mke wa mtu halaf tumpe uongoz si atakuwa gumegume au kicheche? huyu jamaa hafai kabisaaa kwan anaonekana malaya...hao ndo waliojitokeza wasiojitokeza wapo weng...ampe mwenyewe mkewe yeye akitaka changudoa aende bugurun.

mbona raisi wako anawake wa ndoa wengi na bado anazini na wanawake wengine? Asili haipotei ndugu
 
Huyu Mahimbo naye anatia aibu sasa wanawake wamejaa chungu nzima unabaki unan'gan'gania mwanamke asiye kupenda tena isitoshe ameshazaa na mwanaume anayempenda, we kama vipi njo kijijini kwetu Madaba huku wanawake wapo wengi utawapatu, jitu zima linan'gan'gania mwanamke haya ndoa isipofungwa huyo mwanamke ndo atakuja kwako? takataka2


Mkuu usimvunje moyo mwenzio, umesahau Kipenda roho hula nyama mbichi, hacha apiganie haki yake ya ndoa
 
Mahimbo anafikiri mke ni kama commodity!!! eti Slaa amrudishie mke wake...hahahahahahahahahahaha
 
Nikupateje Mkuu asante kwa ufafanuzi ulioshiba nimejifunza vitu ambavyo nilikua sivijui,ubarikiwe sana.!
 
Last edited by a moderator:
Acheni upotoshaji kama kuna zuio la ndoa unapaswa kupeleka kwa paroko wa mtu na wala sio kwa Pengo.Kanisa katoliki sio kilabu cha pombe, kuna hierarchy
 
Jamani huyu bwana alipewa nafasi ya kuitetea ndoa yake na kuleta mashahidi ambao walimuangamiza kabisa kwa kumueleza yeye ni nani.

Alishindwa kuitetea ndoa kwa wazee wa kanisa na wakaridhia iende mahakamani ndani ya miaka miwili tumelishughulikia hili na hatimae mahakama ikaendesha shauri kwa miezi minne,na aliposhindwa kuishawishi mahakama .
Nilipokea Talaka yangu kwa kupitia taratibu zote.

Kwa yale aliyoyafanya 2010, na haya anayofanya sasa, ninashawishika kuamini kwa dhati kabisa kuwa ulifanya uamuzi wa busara wa kuachana naye. Kwa saikolojia ya wanaume, kufanya haya anayoyafanya sasa, huyu hayupo sawasawa. Kama kuna jambo ninaloweza kukusikitikia Josephine, ni kutofanya uchunguzi wa kina hata kabla ya kuwa na huyu jamaa, ungekuwa makini ungefahamu kuwa huyu si sawasawa.

Pamoja na yote haya anayoyafanya, nina imani hayasaidii wala kupunguza chochote, ndoa hufungwa moyoni mwa mtu wala si kanisani, mahakamani au kwa Mkuu wa Wilaya. Nadhani mwanaume huyu nia yake kubwa ni kutaka angalao na yeye watu wamfahamu kuwa yupo katika ulimwengu huu.
 
Nikupateje,

Hivi mie na wewe nani kakurupuka? Narudia tena Mahimbo alifunga ndoa na Josephine Sep 7, 2002 kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama...sasa kama wewe uitambui utajijua mwenye na wameishapata watoto wa wawili.

Naomba nikuulize kwa hiyo Katoliki wanaruhusu kupora mke wa mtu kwa sababu hawayatambui Makanisa mengine?
 
Last edited by a moderator:
Nikupateje,

Hivi mie na wewe nani kakurupuka? Narudia tena Mahimbo alifunga ndoa na Josephine Sep 7, 2002 kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama...sasa kama wewe uitambui utajijua mwenye na wameishapata watoto wa wawili.

Naomba nikuulize kwa hiyo Katoliki wanaruhusu kupora mke wa mtu kwa sababu hawayatambui Makanisa mengine?

Riztz

Kwa imani ya Kanisa katoliki, Tony Blair alifanya ufuska na mkatoliki aitwaye Chery Blair hadi miaka minne iliyopita Tony Blair alipojiunga na Ukatoliki kutoka Anglican.

Kwa imani hiyohiyo na msingi huohuo, Jakaya Kikwete anafanya ufuska na Salma Kikwete hadi siku Jakaya na Salma watakapoamua kuacha uislam na kujiunga na ukatoliki kama mwenzao Tony Blair alivyojiunga.

Ndivyo ninavyotakiwa kuitetea imani yangu na utaona kuwa tumewastahi vya kutosha tunapokaa kimya tusitetee imani yetu tukiogopa kuwaudhi.

Ila mnapotuudhi kama hivi basi inabidi tu-quote imani yetu na ndipo tujue ni nani anarusha mawe wakati amekaa kwenye nyumba iliyojengwa kwa vioo.
 
Kuna thread jana niliwaambiwa mnapotaka kujua mambo ya kanisa katoliki basi inabidi mjipinde kusoma. Kwa mvivu wa kusoma na bingwa wa kuropoka basi kwa Kanisa katoliki utakuwa unaumbuka kila siku.

Wenzenu magazeti ya Ulaya na America wameweka waandishi maalumu kwa ajili ya kusoma na kulielewa kanisa katoliki na inapotokes issue ya Kikatoliki hawawi wababaishaji.

Inaelekea ndoa hii itafungwa kanisani. Kama ni hivyo basi kanisa Katoliki huwa linaangalia mambo yafuatayo.

Kwanza ndoa ni Sakramenti ambayo padre haitoi bali mke anampa mume na mume anampa mke. Ukishapewa Sakremant basi haiondoki hadi kifo chako.

Kitakachofanyika ni ndoa kutangazwa kama kuna kipingamizi. Na vipingamizi ni hivi kwamba labda mhalifu alifungia ndoa jimbo lolote duniani halafu akaja jimbo jingine na kudanganya.

Kinachotakiwa hapo ni kutaja tu diocese mtu aliyofungia ndoa na wala huna haja ya kuleta ushahidi kwani padri wa parokia {Paroko} iliyofungwa ndoa atapigiwa simu na kujulishwa alete kopi ya rekord za ndoa ile.

Kama hakuna kipingamizi hakuna kizuizi cha kuzuia ndoa isifungwe.

Kwa Dr. Slaa na Josephine sijajua watafungia ndoa yao jimbo gani. Lakini kwa sheria za kanisa Dr. Slaa hajafikisha miaka mitano ya makazi yake jijini D'Slaam, hivyo nasita kusema kuwa kikanisa yeye ni mkazi wa Archdiocese of D'Salaam.

Ni wazi bado anahesabika kuwa yeye ni Maktoliki wa Jimbo la Mbulu kwa Askofu Beatus Kinyaiya na si mkazi wa D'Salaam kwa Askofu Polycarp Pengo.

Hivyo hata kama ingekuwa issue inapelekwa kwa askofu ni ujinga kuipeleka kwa Pengo wakati Dr. Slaa hajawa muumini wake. Ningemuona huyu jamaa ana uelewa kidogo kama ningesikia anadhamiria kumuona Askofu Kinyaiya.

Lakini je anatakiwa kufikisha kwa askofu?

Ukweli ni kwamba wanaomuelekeza huyu mtu wanazidi kumpa Dr. Slaa sifa. Wanasahau kwamba Dr. Slaa ni mtaalamu mkuu wa Sheria za kanisa Katoliki katika level ya Phd. Ikibidi Dr. Slaa anaijua vizuri Sheria za Kanisa kuliko maaskofu wengi ikibidi kuliko wote.

Hivyo, nikisikia kuwa anafunga ndoa Kanisani sishangai na najua haitakuwa na kipingamizi.

Vilevile suala hili ni dogo sana ambalo liko mikononi mwa Padri atakayewafungisha ndoa. Usipolielewa kanisa Katoliki unaweza kudhani kwamba Askofu ni kama bosi wa Jimbo hivyo anaweza kuzuia sakrament.

Sivyo. Sakrament hutolewa na padri kwa niaba ya Yesu hivyo hakuna mtu hapa duniani wa kuzuia kama haina kipingamizi cha imani.

Yeye aende kwa Polycarp Pengo, ikibidi apande ndege hadi Vatican aeleze suala lake. Lakini kama Josephine hajawahi kufunga ndoa ndani y aKanisa Katoliki basi huyu bwana na washabiki wake imekula kwao.

Polycarp Pengo atamkaribisha vizuri, atapewa juice, chai na keki kama zipo. Ataona sanamu nyingi nz nzuri za Bikira maria zilivyopambwa pale na Rozari, kisha Pengo atakuja.

Wataongea naye na Pengoa atakachofanya atamfundisha katekism ya Kanisa katoliki kuhusu mambo ya ndoa. Ikibidi atamshauri aonyeshe upendo kwa kuhudhuria misa ya ndoa ya Mkatoliki aitwaye Wilbrod Slaa na Josephine Mushubusi.

mkuu natumia simu ningekugonga like
 
matatzo yote anayataka huyu mzinzi slaa kamkimbia demu wake rose kamili kamchukua mke wa mtu halaf tumpe uongoz si atakuwa gumegume au kicheche? huyu jamaa hafai kabisaaa kwan anaonekana malaya...hao ndo waliojitokeza wasiojitokeza wapo weng...ampe mwenyewe mkewe yeye akitaka changudoa aende bugurun.

Mods huyu jamaa ametumia maneno ya kuudhi. Naomba muongozo au ban
 
Huyu jamaa anawatia aibu wanaume wenzie; yaani bila lepe la soo eti anirudishie mke wangu.... wanawake wameisha? Au amejaribu wote wanamtolea nje? lol. No wonder dada yangu Josephine kampiga chini; anaonekana ni mwanaume dhaifu. Lol.


Hivi wewe kwa akili yako unaweza kumtaka mwanamke aliyekuacha akaenda kuishi na mwanaume mwingine hadi wamezaa mtoto! Unaweza kuendelea kumwita ni mkeo eti kwakuwa tu una cheti cha ndoa! Unadhani ndoa ni cheti au ni uhusiano!? Shtuka!
 
Namkumbuka prince Philip na Camilla Parker Bowles....mtalaka alionyesha ushirikiano wa kutosha mpaka akaalikwa kwenye harusi ya Andrew...

Mahimbo aonyeshe ushirikiano chanya...maana kwa mwanaume wa Kitanzania aliyekamilika idara zote anaibiwa mke, anajua mwizi wake, anamezea , anazalishwa anamezea anajua mwizi yuko wapi.....well lakini wanasema you should strike where it hurt the most, Dr Slaa should have gone through the process of ensuring divorce proceedings are concluded before wanting to marry....

Hii ndoa itakuwa dissolved through irreperable(sp) damages
Hii ndoa itakuwa halali kisheria kwa sababu tayari kuna divorce kati ya Mahimbo na Josephine. Hakuna kardinali atakayeweza kuzuia hii ndoa UNLESS
Ndoa kati ya Mahimbo na Josephine ilifungwa kanisa katoliki ... ambalo halina divorce.
Ila kama ilifungwa wilayani au assemblies of god ni Josephine mwenye uamuzi wa kuitambua au kutoitambua ndoa hiyo kabla ya ndoa yake na Dr. Slaa haijafungwa kikatoliki.
 
Back
Top Bottom