A light touch: Dakika kumi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A light touch: Dakika kumi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 30, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katika pita pita ya kanzi mitaa ya uarabuni kalikutana na mazungumzo yafuatayo kwenye Benki moja yenye makao makuu Canada.

  Mfanyakazi:"Habari za leo kanzi?"

  Ka-nzi: "Nzuri tu habari za hapa Dubai"

  Mfanyakazi: "kwema tu, naona mambo ya tanzania siyo mabaya bwana"

  Ka-nzi: "Kwanini tena, wenzio tunabangaiza tu"

  Mfanyakazi: "Hivi wenzetu mnabiashara gani siku hizi Tanzania?"

  Ka-nzi: "Una maana gani?"

  Mfanyakazi: "Naona hela nyingi kweli inatoka huko kwenu bwana" akajibu huku anamtazama nzi anavyosafisha mikono yake kwenye mbawa zake kujihakikisha kuwa yeye ni msafi.

  Ka-Nzi: "Una maana gani hela nyingi"? kakauliza kwa udadisi.

  Mfanyakazi: "Wiki hizi mbili zimepitia hapa fedha karibu dola miliioni 30 hivi kutoka Tanzania"

  Ka-nzi: "Zimepita kama maji yanavyopita mtoni yakaenda zake au zimepita zikatuwama?" kakagangamala kuuliza.

  Mfanyakazi: "Zimepita kama maji mtoni, zimeingie na baada ya muda zikatoweka kwenda akaunti mbalimbali na hii si mara ya kwanza"

  Ka-nzi: "Wanajulikana waliopitisha au ni mizimu ya watu wa kale?"

  Mfanyakazi: "Wanajulikana sana tu, wanakuja hapa mara kwa mara na kutumia watu wao hapa"

  Ka-Nzi: "Ni kina nani hao?" Ka nzi kakauliza. Jamaa hakutoa jibu. Akanyanyuka kupekua kabati lake la kisasa lililoupande wa kushoto wa kiti chake. Dirisha la ofisi yake liliangalia upande wa barabara maarufu ya Sheikh Zayed. Alirudi na makaratasi kadhaa hivi ambayo yamshikanishwa pamoja kwa pini. Akayaweka mezani.

  Ka-nzi: "ni watu ambao naweza kuwajua ukiwataja?" aliuliza.

  Mfanyakazi:"theluthi mbili unawajua kwani mnao huko huko" alikuwa anaangalia yale makaratasi huku akitingisha kichwa. Alipomaliza akarudia tena "ndiyo karibu asilimia 75 ni watu wenu huko huko". Aliyaweka mezani. Akamuangalia nzi machoni. Kwa haya nzi akapepesa macho yake kwingine.

  Mfanyakazi akachukua simu yake na kubonyeza namba fulani na mara baada ya upande wa pili kujibu akazungumza maneno kadhaa kwa lugha ya Kiarabu, na baada ya kumaliza akamgeukia kanzi.

  Mfanyakazi: "natoka mara moja nisubiri hapa, nitarudi kama dakika kumi hivi". Akanyanyuka kwa ghafla akiyaacha yale makaratasi mezani. Akafunga mlango nyuma yake na kumuacha kanzi mle ndani. Kuna dirisha kubwa la kioo kwenye ofisi ya "mfanyakazi" lakini likiwa limewekwa vioo vyeusi vinavyozuia walio nje kuona waliyomo ndani, lakini wa ndani kuweza kuona kinachoaendelea.

  Ka nzi kakaa pale. Kakabakia kujiuliza swali. "Ni kina nani hao".

  * * *

  Baada ya dakika kumi, mfanyakazi alirudi.

  "Samahani, kulikuwa na jambo nashughulikia." Alisema na kuyaangalia makaratasii yake aliyokuwa ameyaacha mezani.

  "hamna neno, miye ni mtu wa subira" alisema ka nzi.

  "Aisee natumaini hukuchungulia haya makaratasi maana wakijue nimefungwa." aliyakusanya haraka na kuyarudisha kwenye kabati lake na kutia "komeo".

  Ka nzi: "usiwe na wasiwasi mkuu". Hakukanusha.

  "Kama nilivyokuambia, kuna mzungunguko wa ajabu sana wa fedha za kigeni kutoka Tanzania, ni mamilioni ya dola na watu ni karibu wale wale tu". alisema mfanyakazi.

  "Sidhani kama watu wengi wanajua hilo" kanzi kalikiri.

  "Wengi wanafikiri ni biashara tu, Dubai hapa ndiyo Uswisi, watu wanahamisha na kufunga maakaunti yao Geneva wanakuja hapa, ndiyo kitovu siiku hizi cha offshore banking na wanauhusiano wa karibu sana na Costa Rica, Cayman Islands n.k" alisema mfanyakazi na kama aliyebadili mawazo akakoma hapo hapo.

  "Well, tuyaache hayo, habari za familia lakini" aliuliza.

  Ka nzi: "Ni nzuri tu, ila magonjwa magonjwa tu kila kukicha"

  Wakaendelea kuzungumza mambo ya familia zao huku wakikumbushana maisha yao ya ujana kabla "mfanyakazi" hajapata nafasi ya kwenda Dubai kikazi akitokea Canada. Urafiki wao umekuwa wa muda mrefu na wa pekee, mmoja akiwa ni Mtanzania mwenye asili ya Uhindi na mwingine ana asili ya Uarabuni. Walisoma pamoja shule ya Popatlal Tanga. Walisoma miaka ile ya sabini chini ya mwalimu mkuu mashuhuri Chaudry.

  Walipomaliza kukumbushana walikubaliana kuonana nyumbani kwa "mfanyakazi" kwa maakuli ya jioni kwani ka"nzi" alikuwa aendelee na msafara wake maeneo ya Oman katika biashgara zake za "njugu na korosho".

  Kanzi aliondoka akisindikizwa hadi kwenye lift na 'mfanyakazi'. Waliachana kwa kutakiana heri.

  Alipoingia kwenye lift, ka nzi alishika mfuko wake wa nyuma. Alikuwa amekunja nakala za "makaratasi". Alijisemea moyoni "namna hii tumekwisha!". Kichwa kilikuwa kinamzunguka. Alipofika hotelini tu, hakuchelewa alichukua simu yake na kubonyeza makao makuu ya ANTI-UFISADISM INTERNATIONAL HQ".

  Sauti iliyopokea upande wa pili ilikuwa ni ya kike, nyororo na yenye mvuto wote wa haiba na yenye kuweza kufamfanya simba acheze sindimba na nyoka acheze "mugongo mugoongo".

  Kanzi: "Mwanakijiji please!"....


  The END...
   
 2. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ebwana wee
   
 3. 911

  911 Platinum Member

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Waitin for the coming episode....
   
 4. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sijui hiyo task force iliundwa baada ya kugundua ka nzi kamendoka na nakala ya makaratasi,mungu akalinde aka ka nzi!
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwnkjj, usije ukawa umetoa data nyingi sana ka-nzi wakakashtukia or are you the master of misinformation?:
  Lakini hapo utakuwa umewapatia lazima kesho utaona hata humu JF wataongezeka wapiga debe wa mafisadi.... kwikwikwiiii!
   
 6. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaani umetoa hints ambazo wenye kuchemsha bongo wataunganisha nukta, hususan wale waliopitia kwa mzee Chaudry (longest serving HeadMaster in Tanzania) miaka hiyoo .....halafu kanzi kalikaa wiki moja hapo 'uarabuni' nini?? :confused: :confused::confused:
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du ndiyo maana halisi amesema kuwa kuna majambazi yanayokuwinda kumbe ni kwa ajiri ya hako kanzi ah haa! Du vijana wa mafisadi wakiongozwa na mzee wa masters Gembe wana hali ngumu sana ya kupata posho. Lazima watakuwa wanapanga njama za kukanyamazisha kanzi ili masters wamalizie ooh oh!
   
 8. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Mar 30, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  siku hizi muungWAna kila akisafiri ni lazima alale dubai...
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  koh koh koh! I'm so tempted to nyambulishaling hilo neno "alale" in the context of Dubai.. but my guts tell me not to. Ila lina ukweli sana.
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  huko kusafiri si mpaka mtu uwe na travel documents au?
   
 12. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante MKJJ, tunasubiri hizo ..... kwa hamu.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  MMKJ you are extraodinaire!.
  I have been reading people with ESP (Extra Sensory Perception) na wenye PSI-Powers ( ParaPsychology Inspiration), nikidhani ni wazungu tuu na hizo ni hadithi tuu!.
  PSI na ESP ni mambo ya Teleknesis, Telepathy, Precognition, Preamonition, Deja vu, Claivoyance and the sort.
  Sasa naanza kuamini na wengine tunao miongoni mwetu and they posess such powers not by chance but for a purpose!.
  Big Up MMKJ!.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Habari zingine zinaumiza vichwa. Unapokuwa umetoka kukimbizana na kibarua utamani kitu kimoja tu, maji ya baridi yakupoze joto la Dar isiyo na umeme!! Sasa unapkuna na hadithi kama hii, unasikia maumivu ya kicha yakianza taaratibu...!
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  kalagabaho!
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu PM pale si ndo kituo cha Emirates anaunganisha pipa.
   
 17. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  kwa namna hii ina maana kuna vi- Kagodas kadhaa vinatokea kwa mwaka....
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu ulikuwa hujui?
  Toka tumpoteze mzee Julius saizi kila mtu anajilimbikizia mali yaani Miafrika sijui tukoje.
   
 19. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Nakwambia wapiga debe wa mafisadi wamevamia JF kwa fujo! Lakini tutakula nao sahani moja tu hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke. Alutta Continua!
   
Loading...