Vyama hasimu vya kisiasa nchini Afrika Kusini zaidi ya tisa, pamoja na civil societies vimeungana hivi leo kwenye maandamano katika mji mkuu Pretoria wakimshinikiza Rais Jacob Zuma kuondoka madarakani.
Maandamano hayo kuelekea kwenye eneo la Union Buildings, yalipo makao makuu ya serikali, yameandaliwa katika siku ambayo kiongozi huyo anasherehekea miaka 75 ya kuzaliwa kwake na yanafanyika baada ya maandamano makubwa nchi nzima kumtaka ajiuzulu wiki iliyopita.
Hatua yake ya hivi karibuni kumfukuza waziri wa fedha anayeheshimiwa sana, Pravin Gordhan, imemfanya apoteze uungwaji mkono wa umma huku hasira dhidi ya ufisadi serikalini zikipanda, ukosefu wa ajira ukiwa wa kiwango cha juu na uchumi ukidorora.
Kufukuzwa kwa Gordhan kumemfanya Zuma akosolewe na hata watu wake wa karibu ndani ya chama tawala cha African National Congress (ANC), akiwemo Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa.
Wengine wamekwenda umbali na kusema kwamba hawamtaki mwizi kuiongoza nchi hiyo huku wakati huohuo ripoti zikisema aliyekuwa waziri wa masuala ya tawala za mikoa amejiuzulu kiti chake bungeni na kuwa waziri wanne wa zamani kuchukua uamuzi kama huo tangu Zuma alipoamua kufanya mabadiliko yake ya baraza la mawaziri wiki mbili zilizopita.Chama cha African National Congress kimetangaza uamuzi wa Ramathlod katika mtandao wa Twita kikimshukuru kwa mchango wake wa kukisaidia chama hicho.
Waandamanaji walibeba mabango yanayosomeka "Zuma lazima aondoke", "Hamba tsotsi" ("Ondoka mwizi"), na "Zuma muongo".