A Journey to the smart world: Ifahamu teknolojia ya Artificial Intelligence na utendaji wake wa kazi

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,432
105,851
68664.jpg

Salute..
Maisha yanakwenda kwa kasi mno mengi hayawezekani hayapo wenzetu huko wanakesha kutuonyesha jinsi kila kitu kinawezekana kama ukiwa na nia thabiti na mipango. Huko duniani kuna vitu vinaitwa Futurist na Futurology, Futurist ni watu wanaojihusisha na mambo ya Futurology. Futurology inafahamika kama Future studies (masomo yanayohusu mambo ya baadae), Ni masomo yanoyohusu ku-predict mambo mbalimbali yajayo kwa kufanya tafiti kuangalia mambo yaliyopo sasa hivi na kutabiri mambo yajayo.

Futurist wanapredict mambo yajayo kwa kuangalia siasa za dunia,teknolojia ya mwanadamu, intelligence ya mwandamu, Ustaarabu wa mwanadamu, uchumi,nk nk na kutabiri kua miaka kadhaa ijayo kutakua na hiki au kile.

Kwa mfano Futurist wanaelezea jinsi labda maisha ya ya mwanadamu dunia baada ya miaka 20, 30, 50 ijayo yatakua ni maisha yatakayokua yame Advance zaidi. Tutakua tunaishi katika Smart World hivyo binaadamu anaweza kusafiri less than 30 min kutoka bara moja kwenda lingine, Binaadamu anaweza kuanaanza kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence At large, kilimo, Elimu, teknolojia vitaboreshwa, Dini zinaweza kua zimeungana nyingi kurudi kwenye shina kuu (Hasa ukristo)

Hapa tutaangalia Sayansi (Fizikia, Biolojia, hesabu) inaendea kubadili mfumo wa utendaji wa shughuli za kila siku za mwanadamu na kuzifanya ziwe rahisi zaidi. Miaka 20 tukijaliwa uhai tutaona dunia nyingine kabisa iliyopiga hauta katika mambo mbalimbali huku Teknolojia ya Artificial Intelligence ikiwa nyuma ya mabadiriko yote hayo..Always remember mwanadamu anafanya kila njia kua Achieve maisha yasiyo na kifo kwa ghalama yoyote ile.

5deb806fd3806c0da89e6816.jpg

Genesis
Tarehe 4 September 1927 Boston Massachusetts alizaliwa mtoto kutoka familia ya wahamiaji kutoka Ireland ya bwana John patrick na mkewe Ida McCarthy ambao walikua ni wayahudi, mtoto huyo aliitwa John McCarthy. John McCarthy akiwa mdogo aligundulika kuwa ni mtu mtoto mwenye uwezo mkubwa wa akili hasa zaidi upande wa masomo ya Hisabati, akiwa kijana mdogo yupo shule alikua anajifundishi yeye mwenyewe hesabu za vyuoni kwa kutumia vitabu. Mwaka 1951 alihitimu PHD ya hisabati kutoka chuo cha Princeton University. Alijikita zaidi kwenye masuala ya sayansi ya Computer.

Mwanzoni wa Miaka ya 1950 kulikua na majina mbalimbali amabayo walikua wanayatumia kuita mashine ambazo zina uwezo wa kufikiria, kulikua na majina kama Cybernetics,automata theory, complex information processing nk. Mwaka 1955 McCarthy akiwa ni profesa msaidizi wa hisabati katika chuo cha Dortmouth aliunda kundi ili kuthibitisha na kuendeleza theories zinazohusu mashine zenye uwezo wa kufikiria(thinking machine).

Upande wake alichagua jina la kuita hizo thinking machine ambalo ni Artificial Intelligence. Mwanzoni mwa mwaka 1955 McCarthy alienda kuomba ufadhili wa kifedha ili kuendesha seminar aliyokua amepanga ifanyike kipindi cha wakati wa joto yeye pamoja na wanasayansi 10. McCarthy alienda kuomba msaada huo kwenye Rockefeller Foundation inayomilikiwa na familia tajiri zaidi duniani ya Rockefeller Familly, walifadhiliwa. Semina/mkutano huo unaitwa Dortmouth Conference, ulidumu kwa muda wa wiki 8. Ndani ya mkutano huu ndio kukazaliwa rasmi Artificial Intelligence huku John McCarthy akiwa kama ndio founder wa project hii.

Artificial Intelligence ni nini?
Artificial Intelligence (AI)
ni software ambayo iliyotengenezwa kua na uwezo kama binaadamu, inaweza kufikiria, kupanga kitu, kujifundisha/kusoma kutenda kitu na kuweza kufahamu lugha zetu wanadamu. AI imegawanyika sehemu kuu mbili ambazo ni Weak/Specilized/Narrow Artificial Intelligence na Strong/Generalized/Specialized Artificial Intelligence.

●Weak Artificial Intelligence.
Ni aina ya AI ambayo imeundwa kufanya kazi fulani tuo (specific task). Haiwezi kufanya kazi nje ya kile kitu ilichoamuliwa kufanya, lakini inaweza kujifunza pia juu ya kitu hicho ilichoamuliwa kufanya.....ndio maana inaitwa Specializeed pia.

Mfano mzuri wa Weak AI ni Siri na Alexa, hizi ni Intelligence Virtual Assistance au intelligence personal Assistance ambazo zinatumia sauti katika kuwasiliana na mtumiaji. Siri inapatikana kwenye vifaa vya Apple na Allexa inapatikana Amzon.

Siri na Alexa ni mfano mzuri wa weak au Specialized Artificial Intelligence maana japo hizi AI zinaonekana kuwasiliana na kufikiri kama binaadamu pindi zinapoulizwa swali au kufanya kazi fulani, majibu yanayotolewa na siri au alexa yapo progammeda pia kabla ya siri au alexa kutoa majibu ya ilichoulzwa hua inakagua kwanza ni aina ipi ya jibu litakalofaa kutoka kwenye bank/akiba yao ya majibu/responces mbalimbali.

Kiuhalisia siri au alexa hua hafahamu alichoulizwa ila hua inachukua zile keyword unazotamka kisha inaenda kuzifananisha katika bank ya majibu iliyonayo. Baadhi ya mifano mingine ya weak Artifiacial Intelligence ni magari yenye uwezo wa kujiendesha,netflix, fraud detector, Email filters,Facebook newsfeed, google Assistance nk

●Strong Artificial Intelligence.
Hii ni aina ya AI ambayo hufanya kazi zake bila kusimamiwa na hufanya kazi nyingi (unspecified task). Ni aina ya AI ambayo inaweza kujifunza yenyewe vitu vipya. Mfano unapokua unacheza video game na computer technically unakua unacheza na strong AI, inaweza kujifundisha jinsi ya kukwepa mitego yako,inaweza kukusoma unavyocheza na kubuni njia za kukukwepa. Hapa kwenye Strong AI ndio lengo kuu ya mada hii.
ismedicinere.jpg


Kuwepo kwa strong AI wanasayansi wametengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinatumia AI, wametengeneza maroboti yenye uwezo wa kufikiri nakutenda kama binaadamu mfano kuna yule robot aliyepewa uraia wa Saudi Arabia anaitwa Sophia, kuna robot mwingine anaitwa QT-1 ambae yupo kwenye chombo cha anga huko juu anafanaya kazi ya kuongoza robot wenzake.

Makampuni mengi yanatengeneza maroboti mengi kutokana na matumizi ya shughuli mbalimbali. Inakadiriwa miaka 5 ijayo robots zitachukua nafasi nyingi za kazi. Sex robots zote ni Strong AI..Elon musk kawekeza sana kutengeneza vifaa vyenye teknolojia ya Artificial Intelligence

Pia Artificial Intelligence inaweza kua programed ikawekwa ndani ya Computer au mashine yoyote halafu wewe ukawa unatoa command halafu yenyewe inafanya kazi. Nadhani humu wengi tutakua tumeina muvi za Avangers, iron man zote 3, Captain America, spiderman homecoming na far from home. Ndani ya muvi hizo kuna Artificial Intelligence inaitwa F.R.I.D.A.Y na J.A.R.V.I.S, hizi ni baadhi ya AIambazo nazizungumzia hapa. Zinaweza kujifunza chochote na kutenda na kujibu chochcote. Unakua unazipa command zenyewe zinatenda lolote kutokana na jinsi ulivyozipa access.

Kubwa zaidi inasemekana AI inaweza kupandikizwa ndani ya mwili wa mawanadamu na kua intergrated with brain..Mwanzo huko juu niligusia kua John McCarthy alienda kuomba ufadhili wa mkutano wake uliozalisha hii Artificial Intelligence, nkasema kua alienda kuomba ufadhili kwenye Rockefeller foundation. Hivyo basi unaweza kuona kwa jicho la tatu kua AI ipo chini ya Rockefeller Family, Wazee wa conspiracy theories wanasema kua rockefeller family ni moja kati ya familia 13 tajiri za Illuminat (wanao andaa ujo wa mpinga kristo).

Kama mtakua mnakumbuka miaka ya 2011/2012 kuliibuka mashekhe na manabii uchwara mabao wao kila kitu walikua wanakihusisha na illuminti/Freemason huku wakisema kua eti wazungu wanataka watuwekee kitu ndani ya miili yetu ili kiwe kinatuocontrol. Wapuuzi wale walikua wanazungumzia Artificial Intelligence bila kua na uelewa wowote maana kuna uhusiano mkubwa kati ya kua Shekhe au nabii uchwara na ujinga…Then aint big deal, tuendelee na mada yetu.

Artificial Intelligence licha ya kutumiwa kwenye vifaa vya kiteknolojia na maroboti lakini pia inaweza kuwa intergrated na ubongo wa wanadamu, kwa waliosoma Neurology wanaweza kuelezea vizuri..Mtu anaweza kuwekewa chip ya AI kwa matumizi mbalimbali kutokana na yeye anataka nini. Lakini hili nadhani linatumiwa zaidi katika masuala ya ulinzi na ujasusi.

Turing Test.
Mika ya 1950 Mwanahisabati kutoka England aitwae Alan M.Turing alianzisha kipimo cha kupima kama kweli mashine/computer zinaweza kufikiri kama mwanadamu. Kipimo hicho kiliitwa Turing test, kipimo hicho pia kilitabiri kua mpaka miaka ya 2000 computer zinazotumia Artificial Intelligence zitakua haziwezi kutofautishwa na binaadamu kama mwanadamu na computer hiyo wakifanyiwa mahojiano.

GettyImages-1152335789-crop-1200x675.jpg

Matumizi ya Artificial Intelligence Jeshini.
Kama utakua unafuatilia maswala ya teknolojia utagundua kua kila teknolojia inayoanzishwa duniani hua ni katika kutafuta nyenzo mbalimbali za kuwezesha nchi fulani kuwa mbali kijeshi, Uvumbuzi wa Computer ulitoka jeshini. Ili askari waweze kuwasiliana kutoka kambi moja na nyingine inabidi vifaa viwepo kurahisisha mawasiliano.

Hivyo kutokana na hilo wanasayani wamekua wanaumiza vichwa ili kufanikisha majeshi ya nchi zao kua na vifaa madhubuti ili kulinda mataifa yao, hapo ndipo computer na vifaa vingine vimevumbuliwa…John McCarthy alikua ni mwanajeshi wa jeshi la marekani. So atleast gunduzi nyigi zimetokana na uwepo wa majeshi na kila teknolojia lazima itumiwe jeshini huko au idara za ujasusi. Zingine tunaletewa huku kwa matumizi ya kawaida zingine wanabaki nazo. Eg. Time travelling.

Huko juu tumeona kua Artificial Inteligence can be intergrated or linked anywhere. Mtu anaweza kua na kifaa kama miwani,saa halafu vifaa hivo vinakua vipo intergrated na AI, so anakua anatoa comand kisha AI inakua inampatia feedback kutokana na access iliyopewa kufikia taarifa fulani.

Marekani kuna kitu kinaitwa Global Information Grid(GIG), hii ni project iliyotengenezwa na Idara ya Usalama wa Marekani (United States Department of Defense). Project hii imekusanya taarifa zooote nyeti na zisizo nyeti kutoka kona mbalimbali ya dunia.

Hii GIG inaongozwa na kitengo kinaitwa NetOps, hiki kitengo kinaongoza majukumu ya vitengo vitatu vikuu ambavyo ni situational Awareness, command and Control na global Information Grid. NetOps inafanya kazi ya kuendesha kulinda na kuhakikisha taarifa zote zinazoingizwa kwenye GIG ni sahihi.

Hivyo basi wana kila taarifa ya mtu mmoja mmoja ilimradi taarifa zako ziwe zipo serikalini kama hivi huku kwetu tunavyopeleka taarifa zetu NIDA…turudi kwenye Artificial Intelligence.Mwanadamu wa kawaida anaweza kuwekewa AI chip ndani yamwili wa mwandamu then ikawa inafanya kazi pamoja na ubongo, hili linaelezewa kwenye Artificial Neural Networks (ANNs) na Neurolink..kuna mambo mengi sana upande huu yanaeleza how IA can intergrated into human body.

Sasa basi labda jasusi wa CIA anaweza kuwa amewekewa chip ya AI ndani ya mwili wake, chip hiyo ya Artificial intelligence kama ina access ya Global information Grid jasusi/askari huyo anaweza kua anapata taarifa zote kwa muda mfupi.

Yaani anaweza kuwa online kama smartphone ya internet, anaweza kuangali mtu au picha ya kitu akapata taarifa zote zinazohusu kitu hicho ilimradi taarifa za kitu hicho kiwe kwenye GIG. Anaweza kuona hadi taarifa zako z benki, background yako yote..sio kwamba anakua naviona ndani ya TV bali anaviona ndani ya ubongo wake.

Anaweza kupiga simu hata kwa kichwa, anaweza communicate na Setilite kupata taarifa fulani, ilimradi chip aliyowekewa ina access ya mambo yote hayo. Kiufupi mtu huyo anakua kama Computer,Computer yenye internet anaweza hata kufyatua mizinga ya bomu kwa kutumia kichwa.

Nchi nyingi za dunia ya kwanza wanatengeneza siraha ambazo zitakua zinajiongoza zenyewe kwa kutumia Artificial Intelligence. Wao wanaita Artificially Intelligent weapon system, yaani siraha zenyewe zinajiongoza…Kama nchi za USA,Russia,India,Pakistan,China,German,Iran,Uk nk zina mifumo ya siraha ambayo imeshategeshwa tayari muda wote siraha ziko tayari na zinajiongoza kwa kutumia AI.

Mfano kama Russia ikipigana vita na USA halafu labda Russia ikapigwa kabisa basi ina ipo mifumo amabayo italipua mabomu ya atom kuelekea USA na kuisambaratisha nchi nzima wakose wote.
Nchi hizo kila nchi imeelekeza mifumo yake kuelekea kwenye nchi amabayo wanaona ni tishio kwao mfano India imeelekeza Pakistan, USA imeelekeza Rusia,Israel imeelekeza kuelekea nchi za uarabuni.

Inasemekana zaidi ya wataalamu na wanasayansi/watafiti 1000 wakiwemo Stephin Hawking,Elon Musk,Steve Wozinak,John McCarthy wamesaini barua ya wazi wakitaka mamlaka za dunia zizuwie matumizi ya AI weapons system.

Artificial Intelligence ina matumizi mengi mengi karibia kwa kila aspect ya maisaha ya mwanadamu. Inaweza tumika vibaya au vizuri..usidanganywe sijui ni habari za kumleta sijui shetani au nani.

ai-in-healthcare-f.jpg

The End..
Da’Vinci..
El maestro
 
Kuna Facial Recognition au Biometric facial recognition.

Miji mikubwa duniani wameanza kutumia hii AI kukabiliana na hali zisizotabirika.

Hapa kunakuwa na taswira ambazo zimehifadhiwa kutoka kwenye live recording na baadae AI inafanya repetitive analysis ya target anaetafutwa.
 
Bahati mbaya sana, teknolojia zinapunguza umri wa mwanadamu kuishi.

Pia nadhani huko mbele tutakuwa na kizazi cha binadamu wenye maumbile na sifa za ajabu ajabu kweli. Immortal Robotic Humans? Sijui.

Halafu ni kama tutaingia kwenye mfumo hatari zaidi hasa tutakapoanza kuwa intergrated na mifumo ya kompyuta. Imagine umeungwa chip kwenye ubongo halafu kuna mtu somewhere ana full control na access ya kukufanya chochote in his fingertips; si anaweza kubonyeza tu buton ukapiga shoti ukufe?

Yajayo yanafurahisha kweli kweli!
 
Ni maeneo mengi sana yameanza kutumia AI kuna hoteli kadhaa nchini Japan unahudumiwa na robot ambae hukujongelea na kukuliza mahitaji yako ya breakfast..

Kisha robot huyo hukuandalia chai.

Mahospitalini nako AI inatumika.

Viwandani na kadhalika.

Hivyo ni suala la muda tu AI itakuwepo TZ.
 
Interest,
Hii ishu ina mafaida yake na hasara zake pia. Mtu kama huyo ambae yupo intergrated na AI uhai wake unakua umeshikiliwa na wakuu wa kitengo. Maana kweli wakiamua kumfinya ni dakika chache.

Labda nayeye aamue ku-Compromise mifumo yake ili wasiweze kua wanamuongoza.
Ila AI jeshini inasaidia sana utendaji wa kazi kwa ufanisi na haraka
 
Haya mambo yanatangulizwa kwanza kwenye movie halafu ndio yanatokea eti?
 
Kama umesoma Computer Science siyo I.T! Alichoandika jamaa huwez kuielewa. In short ameongelea 3 things only ila kavipigilia nyundo na mbwembwe nyingi sana!

Just know subsets za AI na uzisome. Alafu vidadavue. Huku tunaletewa vile vipande vitamu kusikia na vilaini kwa watu ila vina changanya watu mwisho wa siku alafu kila mtu anakuwa mjuaji kwa namna yake.

1.Data Mining
2.Machine Learning
3.Robotics
4.Speech and Vision
Etc.
 
114 Reactions
Reply
Back
Top Bottom