A.G. Werema: Tutatafsiri Muswada Kama Walivyofanya Wanakongamano wa UDASA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A.G. Werema: Tutatafsiri Muswada Kama Walivyofanya Wanakongamano wa UDASA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Apr 5, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ni swali lililoulizwa na Mchungaji Peter Msigwa. Kwamba muswada huu wa Katiba umeandikwa kwa ung'eng'e, halafu tunasema tutaupelekwa kwa wananchi, ambao kimsingi wengi wao hawajui Kiingereza, Je, hatuoni kama Serikali inawanyima haki ya kutoa maoni yao wananchi?

  Jibu la Bwana Werema ni kwamba watapeleka watu wa kutafsiri ili wakatafsiri kama walivyofanya watu wa UDASA kwenye Kongamano.

  My Take:
  1. Matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Kwani watu hao kwa vyovyote vile hawatafanya hiyo kazi bure. Na hata kwa kutumia akili za mbayuwayu tu, ni gharama kutuma watu wa kutafsiri kuliko kuchapisha nakala ya kiswahili na kuidurufu.

  2. Nani atawateua hao watu wa kutafsisi.

  Changanya na zako.

  Source: CTN
   
 2. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Bureee, kwani wakiuandika kiswahili nini kitapungua, kweli huyo werema hafikirii sawasawa, nchi hii lugha yake ya taifa ni kiswahili na siyo kiingereza, sanasana wanaendelea kumtukuza mzungu....
   
 3. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mkuu hata mimi nimemckia kupitia habari channel ten,jioni hii,yaani cjamwelewa kabisa,.kumbe watu wa kutranslate wapo,bac wafanye hiyo kaz sasa,kwanza itapunguza gharama na itakuwa na tija zaid..ila hawa maA.G wetu,mmh!
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  asilimia 100 ya watanzania wanazungumza kiswahili na idadi y watanzania wanaozungumza kiingereza haifiki asilimia 10. sasa ninani anayepaswa kutafisiliwa wote wanaozungumza kiswahili au wale wachache ambao wanaozungumza english. kuna vitu vingine serikali hii inavifanya havingii hata kichwani. mtasambaza watafsiri wangapi ktk nchi hii ili kila aliyenao huo mswada haweze kusoma akiwa na mtafasiri? hizi ni dalili mbaya kuwa watanzania kutopewa nafasi huru ya kuuelewa na kuujadili vyema muswada.
   
 5. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nawaomba HAKI ELIMU ikishirikiana na Wadau wengine wapenda maendeleo ya Nchi yetu, wautafsiri muswada huu na kama ilivyo kwa katiba tuugawe kwa wananchi wote popote pale katika nchi hii. Kila Mbunge atoe kopi nyingi na zigawiwe kwa watu.
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Leo katika Bunge, akihoja juu ya kwa nin Mswaada wa Marekebisho ya Katiba imeandikwa kingereza amesikika akisema ktk majibu yake kuwa HATA KATIBA IMEANDIKWA KISWAHILI, kwamba KATIBA KM IMEANDIKWA KTK LUGHA TOFAUTI SIYO KATIBA. Swali; Vp kuhusu zile zilizoandikwa kingereza?
  Soure; TBC HABARI..
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kupitia hili unaweza kupima dhamira ya serekali katika hili......haiwezekani jambo linalogusa maisha yetu lichukuliwe kama ni la kawaida sana,mimi naomba tupigane hili hii rasimu iwe katika kiswahili,la sivyo watatutenga watanzania wengi ambao tunaumizwa na ubovu wa katiba ya sasa...
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yani mimi siwaelewi kabisa! Wanajikanyaka kanyaka sana!
   
 9. p

  plawala JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Werema na Kombani waliupinga huu mswada tangu awali,hata raisi mwenyewe alilaumiwa na baadhi ya watu ndani ya ccm baada ya kuunga mkono,serikali haina nia ya kweli kusimamia mabadiliko makubwa ktk katiba au tuseme kuleta katiba mpya,funika kombe muda upite!lakini wajue hatutakubali tena kurubuniwa
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hawa mabwana sina imani nao kabisa,hasa kwenye maamuzi na mipango yao kwa nchi hii....wamejawa ufisadi na kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kutunyonya..,kwa hili la muswada huenda ni mbinu ya kuchota mabilioni yetu eti kwa kuwalipa translators,unaweza kuta wamesha anzisha kampuni hewa ili kutimiza lengo lao....HAWAFAI Hawa!
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huu ni mpango wa serikali na CCM kutaka kuwauzia walalahoi mbuzi kwenye gunia.Kulikua na sababu gani kushindwa kutoa katika lugha ya Kiswahili?Inapofika wakati wa kuomba kura wako tayari kuandika na kusambaza vipeperushi na mabango kwa kiswahili na hata kilugha.Katika swala muhimu kama hili wanaandika kingereza.Hii kutaka kuwadanganya walalahoi au ni mradi wa mafisadi kuchota pesa kwa kisingizio kutafsiri?MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ni aibu AG na akili zake timamu anaweza kufananisha umati watu waliokuwa ukumbi wa nkrumah na watanzania milioni 40.
   
 13. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  3. Hao translators tuna imani nao kiasi gani? Nani wa kuwahakiki?
  Je wakiwapotosha wananchi nani wa kuwajibika? Werema au?

  4. Nani kaishauri serikali kuhusu hili? Ilishawai kufanikiwa sehemu? Au tz ndio sample kwenye hili la watafsiri?
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Werema anaiaibisha taluma ya sheria ambao ndio wanaoaminika katika jamii yetu kwa kusukumiza mapinduzi ya kifikra. Sijui yeye ni mwanasheria wa jeneresheni gani.
   
 15. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi AG ni judge eeh? Aisee...kweli walio jela sio wote wana makosa, I can c!
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kifup sielewi huyo mwanasheria km anaufahamu wa yale ayatamkayo. Mswaada wao nimeusoma, UPO HOVYO!
   
 17. O

  Old ManIF Senior Member

  #17
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa ni watu wangapi watahitajika kuwa wakalimani nchi nzima? Gharama ya kuwapeleka kila pembe ya nchi itakuwa kiasi gani. Hapa kuna kila dalili ya kutengeneza mazingira, anyway ndio tanzania yetu ilivyo.
   
 18. Piere. Fm

  Piere. Fm JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sikushangaa sana kwasababu nihis Warema ana matatizo mengi mnooooo!! Ni huyu warema aliyepinga suala la katiba mpya kwa mara ya kwanza, hakushauriana na boss wake Jk mpaka wakakinzana me na wewe hatujui. Pia ni huyu Warema aliyesema Dowans lazima ilipwe, amekuwa msemaji wa serikali me na we hatujui. Me nahis kama tauluma yake haina mushkeri basi ana matatizo ya kufikiri. Tafakari.
   
 19. m

  macinkus JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kama nakumbuka vizuri, wenzetu Kenya waliweza kuwa na lugha zote mbili za katiba kabla ya kupigiwa kura. Iweje Bongo ambayo kwa sasa ina katiba (au nakala) ya kiswahili sasa ishindwe kutwa na katiba mpya ya kiswahili?

  macinkus
   
Loading...