Taavid
JF-Expert Member
- Feb 7, 2018
- 7,858
- 67,293
imenibidi nicheke tuTuendelee na simulizi
Chuoni tulikuwa na nyakati za furaha pia
Siku za Jumapili kwakuwa ilikuwa kama visiting day tulipata wageni wengi sana na chakula kilikuwa kizuri
Jumatatu pia kwakuwa ndio siku ya mapunziko
Tukialikwa kwenye matamasha na mashindano ya martial arts
Lakini cha Ajabu kuliko zote ilikuwa tukialikwa kwenye misiba
Huko kulikuwa kuzuri Sana kwakuwa baada ya kumchoma marehemu(cremanation) tuliandaliwa misosi ya maana Sana, Yani tulikuwa hatuoni soo kabisa kuiandaa maiti mwanzo mwisho mpaka kuichoma moto kishapo kwenda Kura as if tuko kwenye Sheree.... Binafsi nilichoma zisizopungua 20. Naomba niseme tu Kwamba sikuwa na hisia zozote juu ya wale marehemu
Chuoni pia tulikuwa na likizo na kipindi cha likizo tulipelekwa sehemu mbalimbali kutembea kama watalii kabisa! Nimetembea nchi na miji mingi sana kwasababu ya hiki chuo
Kuna thread nyingi nimesimulia sana kuhusu wafu mochwari na maiti ni kupitia chuo hiki ndio nilijifunza yote hayo kwa nadharia na kwa vitendo! Mochwari ni sehemu inabeba mambo mengi ya kuogofya mno ya kutisha kushangaza lakini pia sometimes kuchekesha
Kwa mfano siku moja nikiwa session mochwari ililetwa maiti moja ya like ikiwa almost uchi ikikamilika Kila idara sasa wakati inafanyiwa utaratibu wa kuwekwa kwenye barafu ilalazwa pembeni mwa maiti ya kiume nayo ikiwa uchi kabisa.... Aisee hivi mnajua ile maiti ya kiume ilidindisha?