A day in the Buddhist college

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,605
696,697
1438949170726.jpg
Hapa ndio chuo nilipoanzia kujifunza mambo ya Buddhism, meditation, chanting nk. Hii ni picha ya mwaka 1997, na hiyo ni sehemu ya wanachuo.

Hiki kilikuwa ni chuo kugumu na chenye sheria kali kuliko jeshi, tulikuwa wanachuo 21 toka Tanzania lakini tulifanikiwa kumaliza chuo tulikuwa kumi tu na mwishoni watano.

Tulipewa kila kitu bure lakini vinavyofanana kuanzia nguo mpaka dawa ya mswaki. Tuliishi maisha ya useja (total celibacy) huku tukiziadhibu hisia kwa kiwango cha juu mno!

Tulikuwa kwenye self cultivation (bringing back the scattered mind) Na hii ndio ilikuwa ratiba ya siku moja inayojirudia mara sita kwa wiki.

05:40 kuamka kutandika vitanda na kupiga mswaki/ kuiga

05:50 parade/ rollcall

06:00-0650 chanting/ meditation

06:50-07:00 parade/ rollcall na kwenda dining hall kimya na kwa mistari bila kuangalia kulia wala kushoto

07:20 chanting and giving offerings kwa milefo, na hungry ghost kisha breakfast

07:20-07:50 usafi

07:50-8:00 parade/ roll call na kuingia darasani

Vipindi vilikuwa ni dk 50 mapumziko dk 10 kuanzia saa mbili mpaka saa tano na dk 50

11:50-12:00 parade/ roll call na kumatch kwa mistari iliyonyooka kwenda dining

-Kuchant kutoa offerings kwa Milefo(future buddha?), hungry ghosts na kisha kula

12:00-13:50-lunch, walking meditation na kupumzika

13:50-14:00 parade roll call na darasani mpaka saa 15:50

15:50-16:00 parade roll call na kubadili nguo

16:00-16:50 martial arts, kung fu karate tai chi nk

16:50-17:50 free time hapa ndio sasa mnaweza kupiga soga na kuendelea na martia arts gym library etc

17:50-18:00 parade rollcall na kumatch kwenda dining

18:00-18:50 chanting offerings kwa Buddha na hungry ghost na kupata dinner

18:50-19:00 parade roll call

19:00-20:50 darasani

20:50-21:50 meditation/chanting

21:50-22:00 kurudi vyumbani kwa kumatch kwenye mistari tena kimya, kuingia vyumbani kuzima taa na kulala
Ukionekana nje baada ya hapo ni majanga

Chuo kiliongozwa na sheria kwenye kila kitu, sheria ya kutumia Maji, kutembea, kuongea kukaa kula kugeuka kulala, kutandika kuvaa etc kila kitu kilikuwa ni sheria na ndio maana wengi sana walishindwa maisha yale
Hii picha ni jinsi tulivyokuwa tunakaa mstarini kila mtu na nafasi yake kwahiyo hata kama haupo nafasi yako inabaki wazi.

1438949170726.jpg
 
Inavutia

Lengo lako lilikuwa nini? Na hao watz wote mlikutana huko huko ama kulikuwa na mradi flani? Ni kozi ya muda gani?

Mlikaa kwa muda gani?
Gharama kiasi gani?

Initial/basics ni miaka miwili baada ya hapo unaenda Asia miaka mitatu, mwishoni mwa mwaka wa tatu unafanyiwa ordination kuwa official Buddhist master.

Ordination si kitu kidogo nikitu kikubwa mno kwakuwa ndio unapigwa mhuri rasmi
 
74 Reactions
Reply
Back
Top Bottom