Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Kitu kinachoitwa Trend Reading, ni moja ya maeneo magumu sana kufanywa na wasomaji wa kawaida, inaweza kufanywa na wale tuu wenye uwezo wa kusoma kitu katikati ya mistari.
Hivyo katika kusoma taarifa ya Press Conference ya Acacia iliyofanyika jana kule London, trend reading zinaonyesha hawa Acacia wameisha jua kilichomo kwenye Ripoti ya kamati ya pili baada kuwapatia ushirikiano wa hali ya juu!, ambao kwa tafsiri yangu binafsi, ushirikiano wa aina hii kwenye Tume za uchaguzi could as well be compromised!.
ACACIA; Taarifa ya mkutano na wanahabari uliomalizika UK ;Kuhusu sakata la mchanga "Makinikia"
Sababu zangu ni hizi.
1. Mchanga wa Makinikia uko Tanzania, aliyepiga marufuku kusafirishwa Mchanga huo ni Rais wa JMT, mgogoro wote wa mchanga huu uko nchini Tanzania, kwa nini press conference ya kuzungumzia kadhia hii ufanyike London? .
2.Acacia wangefanyia Canada ingekuwa halali kwa sababu huko ndio makao yao makuu baba yake Barrick yalipo, au Press Conference hiyo ingefanyika kwenye eneo la tukio Dar es Salaam Tanzania na sio London, Uingereza.
3.Kwa vile Shares Acacia zina trade kwenye Soko la hisa la London na la Dar es Salaam, DSE, na lengo la Press Conference ile ni kutoa tuu reassurance kwa wanahisa wa Londo kuwa everything is OK interms of hisa zao ndio maana licha ya kuzuia kusafirishwa mchanga, bado wanapata faida ile ile na ndio maana wametoa gawio nono kwa wanahisa wao, ili tuu kuzuia mauzo ya hisa zao kuzidi kuporomoka, jee vipi wanahisa wa DSE?, wao hawastahili reassurance?.
4. Katika taarifa yao wamesema na hapa nina quote
" Since then, Acacia has continued to
co-operate with the second Presidential Committee, which was set up to examine economic and legal issues associated with historic exports of gold/copper concentrates".
Hapa wanamaanisha wanashirikiana hii kamati ya pili. Kwanini hawakushirikiana na kamati ya kwanza?!.
5. "We have provided extensive information to this committee and have provided access to each of our mine sites". Kwanini sasa ndio waprovide extensive information kwa kamati ya pili?!. Baada ya kamati ya kwanza kuyabaini tunaibiwa, jee sasa ndio yanajifanya ku provide extensive information ili kudhibitisha no stealing au kujikosha tuu?!.
6. "We believe that the second Committee is close to completing its work". Hii ni dalili ya watu kuwa compromised!. Kamati ni ya Rais wetu, inapaswa kuripoti kwa Rais wetu, iweje Ripoti ifike Acacia kuwa wanakaribia kumaliza, hii kamati inaripoti kwanza kwa nani kati ya kwa Rais wa JMT na Acacia?.
Hata kama Acacia wanao wasiri wao ndani ya kamati waliowapa siri kuwa wanakaribia kumaliza, kwa vile kamati ni ya Rais wa JMT, na sio ya Acacia, then hata kama walipata taarifa ya siri ya kukaribia kumaliza kazi walipaswa kujinyamazia kimya hadi Ripoti ifikie mwenye Ripoti yake. Huku kuropoka kwa Acacia ni kufuatia "ushirikiano mkubwa" walioutoa kwa kamati hivyo sasa inawezekana kamati inaripoti kwao kabla ya kwa aliyewatuma?!.
7. " following which we would welcome the opportunity to discuss the findings directly with the Government". Hapa Acacia wanaeleza wameishayajua matokeo ya kamati ya pili na wameisha yajua mapendekezo, kamati hiyo imependekeza Serikali na Acacia wakae meza moja kuyajadili matokeo hayo!.
Yaani tayari wameishajua wataitwa kwa majadiliano na hapa hata kabla Ripoti haijatoka, mapendekezo hayatolewa, wala hao Acacia hawajaitwa kwa majadiliano, tayari wameisha itika wito wa kuja kujadiliana na Serikali!. Rais wetu Magufuli kamwe usikubali kabisa uhuni huu, kama kuna chochote cha kujadiliana, tukutane mahakamani.
Bila kujua matokeo ya hiyo kamati, wamejuaje wataitwa kwa majadiliano?. Kitu usichokijua unakisubiria kwa wasiwasi maana hujui kama utafukuzwa, utashitakiwa au itakuwaje, lakini wenzetu hawa wameishajua kila kitu hadi wataitwa tukae mezeni kujadiliana nao?. Wanafikiri Magufuli ni Kikwete, kukaa meza moja na majizi kujadiliana jinsi ya kurejesha walichokwiba!. Sijui kwa Magufuli huyu!.
8. "We remain hopeful that we will be able to reach a resolution to the current situation with the Government so that we can continue to deliver strong performance from our mines for the benefit of all stakeholders".
Huyo walio m compromise amewaahidi hili litakwisha, hivyo hapa wanatoa assurance kwa wanahisa wao kuwa litakwisha na wataendelea kutuibia!. Nani amewapa assurance hii, who is so close to Magufuli amewaahidi hawa majizi kuwa hata hili litapita tuu na tutaendelea?.
9. Ikitokea matokeo ya Tume ya pili yakawa ni tofauti na yale ile Tume ya Mwanzo, Rais Magufuli usikubali, hakuna kukaa chini kujadiliana chochote na majizi haya, madini ni yetu, hata wakitishia kuondoka na kuhatarisha investment climate ya nchi yetu, then just let it be, let them pack and go!. Tujenge uwezo wa ndani, hadi watoto wetu na watoto wa watoto wetu ndio waje kuwa wawekezaji wa nchi yetu!.
10. Angalizo kuhusu Trend Reading ni kusoma dalili tuu kama ilivyo kwa dalili ya mvua ni mawingu, kunaweza kabisa kutokea wingu kubwa, zito na jeusi la dalili ya mvua kubwa lakini mvua inaweza kabisa isinyeshe.
Hivyo inawezekana kabisa hakuna yoyote aliye kuwa compromised, bali hizo details za Acacia kwenye hiyo press conference yao ya London sio any inside information za kamati bali ni just pre emptive moves za trende shapping ya mapendekezo ya kamati. Hivyo trends zote nilizowawekea humu zinaweza zisitokee.
Conclusion.
Kama hili limetokeo haitakuwa mara ya kwanza kwa possibility ya viongozi wetu hadi wakuu na maofisa wetu wa serikali kuwa compromised kwenye uvunaji wa rasilimali zetu kuanzia mikataba mibovu hadi cheating na mis representation za kilichomo.
Kwenye hili la mchanga niliwahi kushauri hivi hata kabla Tume hazijaundwa!.
Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!".
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Mbariki Rais Wetu Magufuli ili ayaweze yote katika YEYE.
Nawatakia Jumamosi Njema
Paskali