A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors | Africa Wake Up

Mkuu samahani nina swali kidogo, umesema original ya ukristo ni Middle East and specifically Israel, swali linakuja itakuaje sehemu yenye chimbuko la ukristo yani Israel ndio kuwe na idadi ndogo sana ya watu wakristo? Yani Israel ata waislam ni wengi kuliko wakristo, katika population yote ya Israel wakristo ni 2% na Muslim 6% na zilizobaki ni wayahudi

Sasa imekuaje kwenye chimbuko la ukristo wao hawautaki ukristo ila katika maeneo ambayo sio chimbuko ndipo kuna idadi kubwa ya wakristo mfano Africa
Maswali yako ni kuntu na ni biblical.Ningekupa maandiko kutoka kwenye Biblia, lakini kwa vile inaelekea hujui maandiko,nadhani ni busara kukupa maelezo tu.

Ni hivii,Bwana Yesu (a re-incarnation of God),ambaye ndiye mwanzilishi wa Ukristo,amezaliwa Israel.Huyu Bwana Yesu,alichagua wanafunzi wake 12,ambao ndio waliokuwa msingi wa kwanza wa Ukristo Israel.

Kwa nini waumini wa Ukristo ni wachache Israel.It is a Godly plan.Through their denial of Jesus Christ,non-Iraelis(ambao Biblia inawaita Wamataifa), wamepata wokovu.The Bible makes it very clear that because of this, "true" Israelis will be saved as a nation.Hii inaweza kuwa ngumu kwako kuelewa,lakini ndio ukweli according to the Bible.
 
BOOK SUMMARY: WHITE POISON

(A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors..Africa Wake Up !)

MWANDISHI: Kayemb “Uriël” Nawej

MCHAMBUZI: Ghost Writer()

inaendelea..

Kabla ya ujio wa wakoloni Watu weusi walikuwa wakiabudu miungu( Polytheism) lakini baada ya ujio wa hawa wazungu mambo yakaanza kubalika baada ya kuanzisha imani ya Mungu mmoja( Monotheism) kwa kusema Miungo tuliyokuwa tunaiabudu ni imani potofu kwani kuna Mungu mmoja tu ambaye yuko juu.

Kabla ya ujio wao, watu weusi walikuwa na zaidi ya lugha 7 ambazo walikuwa wakiongea na kuzitumia kuandika baadhi ya maandiko yao mbalimbali. Kulikuwa na Yoruba, Nsibidi, Gicandi, Mende, Vai, Loma, Ge'ez, Bete na Bamum

Yoruba ilikuwa ikiongewa baadhi ya sehemu ikiwepo Nigeria, Ghana, Benin, Togo na Ivory Coast

Nsibidi ilikuwa ikiongelewa sana Nigeria na Cameroon

Gicandi ilikuwa ikiongelewa Nchini Kenya tu hapo kwa jirani zetu ambayo sahv nadhani niyo wanaita Kikuyu

Mende
ilikuwa ikitumika zaidi Sierra Leone na Liberia

Vai ilitumika sana Liberia na Sierra Leone pia

Loma ilitumika Liberia, Guinea na sehemu zingine

Ge' ez ilikuwa ikitumika Nchini Ethiopia

Bete nayo ilikuwa ikitumika Nchini Ivory Coast

Lakini pia Bamum ilikuwa na yenyewe inatumia Cameroon n.k

Na katika Maandiko hayo yote yaliyoandikwa na watu weusi kabla ya ujio wa wazungu yalikuwa yakigusa sehemu mbalimbali ikiwepo sayansi, sanaa, ushairi n.k lakini wengi wetu tumekuwa tukijua kwamba wazungu ndio walitufundisha kusoma na kuandika kwani walitukuta hatujui kusoma wala kuandika( Illiterate)

Kwa lugha ya Lingala, kusoma ni Kotanga na kuandika ni Kokoma

Kwa lugha ya Bambara, kusoma ni Kalan na kuandika wanaita Sebe

Kwa lugha ya Fulani, kusoma wanaita Janguigol na kuandika ni Windugol

Kwa lugha ya Yoruba, kusoma ni Kika na kuandika ni Kiko.

Tumeona kwamba bila ata ya ujio wa Waarabu na Wazungu tayari Africa ilikuwa na lugha zake , Swali la kujiuliza ni inawezekanaje Africa iwe na maneno yanayomaanisha KUSOMA na KUANDIKA ikiwa hawajui kusoma na kuandika!!?

Hivyo basi, Wazungu walikuja kutubadilishia mfumo wetu na kutufundisha mfumo wao ila sio kwamba walitukuta hatujui Kusoma na Kuandika.

Tukirudi nyuma kidogo tukamuangalia Mwanahistoria wa kigiriki ya kale 'Deodorus of sicily' katika nyakati za Julius Caesar ni kwamba maandiko ya kigiriki( Hellenic writing) ambayo ndiyo yalizaa maandiko ya Kirumi na Latin yalikuwa yakifundishwa na Mtu mweusi aliyekuwa anaitwa Cadmos kutoka Misri ya kale. (Tutalizungumzia hili kiundani katika maandiko yanayofuata na uthibitisho kadri inavyowezekana).

Je unajua kwamba viongozi waa kikristo sana sana Papa wamekuwa wakiunga mkono biashara za utumwa!?

Je umekuwa ukijua kuwa wamekuwa wakisema kwa muda mrefu kwamba watu weusi hawana nafsi!?

Je unajua kuwa babu zetu walibadili dini na kuwa wakristo kwa kulazimishwa, kunyanyaswa, kuteswa na mauaji ya halaiki!?

Hivi unafikiri Babu zetu wanajiskiaje huko walipo wakiwa wanatuangalia kwamba kunaipenda dini ya wale waliowatesa na kuwauwa!?

Kwa miaka mingi zaidi ya waafrica 15,000,000 wanaume, wanawake kwa watoto wamekuwa wakichukuliwa kama punda( Beast of burden) kwa kubebeshwa mizigo kama watumwa huku wakidanganya na maneno potofu kwamba "Mpende Jirani yako kama nafsi yako"(Mathayo 22:39) lakini wao walikuwa wanawapenda jirani zao ambao wamewafanya kuwa watumwa!?

Usilolijua wale wafalme watatu Melchior, Gasper na Balthasar waliokwenda kumuhani Yesu baada ya kuzaliwa mmoja wapo alikuwa ni Mtu mweusi. Melchior ambaye alikuwa mfalme wa Persia, Gasper alikuwa mfalme wa india na Balthasar alikuwa mfalme wa Arabia ama ukipenda Ethiopia.

Picha ya Bikira Maria( Cult of the virgin Mary) haikuwepo wakati wa ukristo mwanzoni ila baada ya mwaka 431 ndio walianza kuitumia kanisani

Mfumo wa Kuabudu sanamu za Mitume na Malaika ( Veneration) haukuepo mpaka mwaka 609 ndio walianza kuweka sanamu za mitume na malaika kwenye Makanisa yao. Lakini pia walianza kuziweka picha za mitume hao Makanisani kuanzia mwaka 787

Mfumo wa Utawa( Celibacy) ulipitishwa kwa Mapadri na viongozi wengine Mwaka 1074 ila huko nyuma haukuwepo na Mitume wote walioa isipokuwa Yohana na Paulo.

Mfumo wa kuvaa Taji la kristo ( Crown of christ) ulianzishwa mwaka 1090

Utoaji wa sakramenti( The sacrament of Penitence) ulianzishwa mwaka 1213

Matumizi ya Mkate( wafer) kama mwili wa kristo yalianza mwaka 1215

Matumizi ya Mvinyo( wine) kama damu ya kristo yalianza mwaka 1415

Na imani hii ya kutumia Mkate na Mvinyo( Transubstantiation) kama ishara ya mwili na damu ya kristo ulithibitishwa kutumika rasmi mwaka 1551 wakati wa mikutano ya Council of Trent ikiendelea

Na mengine mengi ikiwemo imani ya Immaculate conception iliyowekwa bayana mwaka 1854 na Amri ya Papal infallibility iliyotolewa kwenye First Vatican Council mwaka 1870

Unaweza kuona mambo yote haya yaliyoanzishwa baada ya kuondoka kwa Yesu kristo lakini hakuna ata kimoja alichokianzisha yeye kati ya hivo.

itaendelea!!
(Ghost..)
Tisha sana Mwamba..
 
Maswali yako ni kuntu na ni biblical.Ningekupa maandiko kutoka kwenye Biblia lakini kwa vile inaelekea hujui maandiko,nadhani ni busara kukupa maelezo tu.

Ni hivii,Bwana Yesu (a re-incarnation of God),ambaye ndiye mwanzilishi wa Ukristo,amezaliwa Israel.Huyu Bwana Yesu alichagua wanafunzi wake 12 ambao ndio waliokuwa msingi wa kwanza wa Ukristo Isrthis,

Kwa nini waumini wa Ukristo ni wachache Israel.It is a Godly plan.Through their denial of Jesus Christ,non-Iraelis(ambao Biblia inawaita Wamataifa), wamepata wokovu.The Bible makes it very clear that because of this, true Israelis will be saved as a nation.Hii inaweza kuwa ngumu kwako kuelewa,lakini ndio ukweli according to the Bible.
Shukrani mkuu
 
Asante kwa kushukuru,ila wewe je,huoni kwamba ingekuwa busara kuingia kwenye huu mpango mkubwa wa Mungu wa kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye hukumu ya milele aliyoandaliwa Shetani na wale wasiomtii Mungu?
These things are too complicated brother, ila tuko pamoja, unachofanya ni sahihi hivo endelea kusambaza injili
 
These things are too complicated brother, ila tuko pamoja, unachofanya ni sahihi hivo endelea kusambaza injili
Sio complicated mkuu,ni swala la wewe kukubali kuwa on-board and God will facilitate the rest through His Holy Spirit.
 
Sio complicated mkuu,ni swala la wewe kukubali kuwa on-board and God will facilitate the rest through His Holy Spirit.
Ni complicated mkuu ndio kama hivo unaambiwa wayahudi ni taifa teule kivipi? Baada ya Mungu kuwapa adhabu binadamu kutokana na matendo yao kama vile kuchoma moto kipindi cha sodoma na kushusha gharika kipindi cha nuhu, akasema hatoangamiza tena watu wake ispokuwa amewapa freewill kila mmoja kwa utashi wake aamue maisha yake ataishi vipi ili adhabu iwe siku ya mwisho, sasa kwa maana hiyo huoni kama Mungu hajaweka usawa, iweje wayahudi ata waibe, wadhini, waseme uongo, waue wao teyari ni teule na wengine tuadhibiwe huoni kama hakuna usawa?

Unahis ni kweli tumepewa freewill au tumepewa uoga? Kwa namna moja au ingine me naona watu wanafanya ibada kutokana na ile fear tuliyonayo moyoni, kuwa nisiposali kuna moto, nisiposali sipati baraka, nisiposali kitatokea hiki na hiki kwanini kusali sio enjoyable? Narudi kule kule kwanini alipozaliwa yesu ndio kuna namba ndogo ya wakristo? Ikiwa jamii yao ndio ina history ya yesu original huisi kama wao ndio walitakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kumkubali na kumpokea mwana wa Mungu?

Kwanini ukristo imekuwa ni ngumu sana kuingia na kuenea bana la Asia kuliko Africa? Sie tuna uspecial upi tofauti na wenzetu wachina /wahindi /wathai hadi iwe rahisi sana kuliko kwao? Kutokana na population yao na level ya maisha waliyonayo wengi me naamini ingekuwa rahisi sana kuwa manipulated na kukubali hizi dini ila kwanini imekuwa kazi ngumu sana kuwabadili msimamo wao, je Mungu amewazira au hana mpango wa kuwakomboa kwa kuwapelekea injili?
. Unahisi wanakosa nini ambacho sie tunacho kwa kutoamini katika ukristo?
 
Mlokole uchwara akikujibu haya maswali nitag .
 
Eti usioe au kuolewa ili ufanye kazi ya Mungu! Ni Mungu yupi?? Ni utumwa uliotukuka kwani mtu unavizia wanawake kwa kujificha ili usionekane ,huo ni utumwa!

IMG_0114.jpg
 
Kimbaguism ni dini ya asili iliyoanzishwa na Simon Kimbagu huko Congo mwaka 1921

Tukija kwenye suala la Ubuddha sio kwamba ni lazima iwe imeanzishwa/ ni utamaduni wa Mtu mweusi ila mwandishi alichokuwa anamaanisha ni bora kufuata imani ya kibuddha ya kuabudu miungu kuliko kuamini katika ukristo( Monotheism)
Kimbaguism sio dini asili ya kongo!! Ni ukristo wenye kufit na tamaduni za kikongo! Yaan mixture humo humo ukristo pamoja na yale yanayozuiliwa na ukristo!! Kimbangu hakuukata ukristo ila alitaka tamaduni za kikongo ziongezwe kwenye ukristo, mfano wake wengi, tiba asili, ngoma, etc rejea hata "antonian movement" iloongozwa na kimpa vita huko kongo 1700s
 
BOOK SUMMARY: WHITE POISON

(A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors..Africa Wake Up !)
Sasa najiuliza hao Wakristo wa Ethiopia waliofuata Ukristo wao tangu miaka 1700 walimsaliti nani? au nini?
Yaani unaleta nukuu ya Kenyatta ambaye ni Gikuyu na tunajua Wagikuyu walikuwa na dini yao kabla ya wamisionari wakisali kwa Kirinyaga (Mlima Kenya). Ila wakati Waethiopia walikuwa Wakristo tayari, Wagikuyu hawakuwepo bado. Inajulikana kwamba walihamia sehemu ya Mlima Kenya kutoka kaskazini. Kwa hiyo kusali kwa Kirinyaga haikuwa dini ya mababu yao. Ila kabla ya mababu hao Waethiopia walikuwa tayari Wakristo.
Kwa hiyo naomba msaada kuhusu hicho kusaliti . . .
 
Kumbe, kimya ? Samahani kama swali lilikuwa ngumu kidogo. Sikutaka kumtisha mtu yeyote. Samahani tena!
 
Back
Top Bottom