A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Hitajiko la malighafi na nguvu kazi huko kwao ndio chachu iliyowapelekea kuja Africa .wakati sisi hatukuwa na mahitaji hayo kwa kiasi kikubwa hivyo tako zetu zililia bwata. Kama ilivyo mchukue mtoto wa masaki na uwanja wa fisi uwapambanishe basi utapata majibu.. n.b wazungu walianza kutawalana na kutumikishana wenyewe kwa wenyewe na kutokana na hali ngumu za kimazingira na kimaisha kiujumla mfumo wao ulikuwa strongest to survive hivyo waligaa gaa sana kutafuta ukuu ili wazidi kujiimarisha wakati sisi tukilewa neema ambayo wenzetu hawakuwa nayo
Nimeelewa sasa
 
Hitajiko la malighafi na nguvu kazi huko kwao ndio chachu iliyowapelekea kuja Africa .wakati sisi hatukuwa na mahitaji hayo kwa kiasi kikubwa hivyo tako zetu zililia bwata. Kama ilivyo mchukue mtoto wa masaki na uwanja wa fisi uwapambanishe basi utapata majibu..
thanks. umenena@
 
Unamaanisha nini kwa hii statement yako?
Habari nzima ya "mtu mweusi" na "mtu mweupe" ni hadithi ya kutungwa na watu ili waweze kubaguana vizuri.

Kwamba, hizi catwgory za rangi za watu hazipo,na hata rangi zilizopo hazina ukomo maalum wala wa kueleweka kisayansi.

Kwamba, huu ni mfumo arbitrary watu wamejitungia tu.

Kisayansi, hakuna significant difference kati ya watu inayotokana na rangi ya ngozi ya mtu.

Na hao wengi wanaofikiriwa jwamba ni weupe wana mchanganyiko mwingi sana na na wanaofikiriwa juwa ni weusi.

Msome James Baldwin utaona kaandika hata mambo miaka mingi sana, racw us a made up thing.

Nimetoka kusoma " Between The World And Me" cha Ta-Nehisi Coates, anazungumzia sana hii hadithi ya "watu weusi" na "watu weupe".
 
Sidhani kama waafrika tuna akili tofauti na watu weupe au wazungu. Nachoona ni wenzetu waliwahi kustaarabika na kuendelea kabla yetu na waliweza kugundua vingi kabla yetu hivi hapo ndipo walipotuzidi.

Ila kama ubaguzi usipokuwepo kabisa duniani na mtoto wa kiafrika na kizungu akakuzwa katika mazingira sawa utakuta akili zao zinafanya kazi sawa. Mfano ni mashirika kama FBI ambapo kuna watu weupe na weusi na wote wanapiga mzigo sawa sema kutokana na ubaguzi mweupe atafanywa awe kiongozi wa mweusi
Kustaarabika ni kitu gani na kwa aina gani.. Unaweza sema ushoga ni ustaarabu..
 
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.
Jibu zuri sana mkuu
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom