Kizibo
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 3,871
- 8,380
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.
Kwa kiasi fulani uko sahihi, lkn swali linakuja, HADI SASA HATUNA MATATIZO YA KUTUFANYA TUTOKE NJE YA BOKSI KUFIKIRIA ZAIDI?? mtu anapata matatizo, badala atafute suruhusho anakimbilia kuombewa au kwa waganga au NASEMA NAMWACHIA MUNGU YEYE NDO ANAUEPANGA KILA KITU