_Mrejesho_,haya ndio majibu ya mama mkwe nilipomfata make wangu kumuomba msamaha.

Mr mgeni

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
1,222
804
Habari za mda huu wanaJf,.
Ni safari ndefu kidogo nilisafiri,nilitumia siku mbili kumfuata mke wangu kipenzi na mwanangu kumuomba samahani kwa niliyo mkosea.Daahh!! Kweli wanawake wana moyo wa huruma sikutegemea kama ataweza kunisamehe lakini alinisamehe kwa yote,alilia na kutokwa na machozi mengi sana kuonesha machungu alionayo juu yangu na kudai ananipenda sana hakutegemea kama anaweza kunipata tens.kidogo afya ya mtoto ilidhoofika kidogo.Hapo nilipokuwa Mimi na yeye mke wangu tukamaliza.Ilikuwa shughuli pevu pale nilipoanza kujieleza kwa wakwe;kiukweli hawakunielewa hata kidogo.Mama mkwe alinichukia sana na kuniambia maneno ambayo sipendi kuyataja humu,.na kusema "yamekushinda ndo umemfata mwanangu'wanawake wengine huwaoni?mwanangu haondoki popote hapa kama ni haja ya mtoto wako mchukue"ndivyo alivyomaliza na kuendelea na shuguli zake zingine.Nami sikujivunga niliondoka zangu.Sasa wife anataka atoroke aje kwake Je nikimkubalia nitakua nipo sahihi?au ni ache naye mzazi wake arizike?naombeni ushauri na mawazo ya kina.Ahsanteni nikipata majibu mazuri.
 
Wewe muache aje tu hapo ni kwake.unafikiri atakaa kwa wazazi wake hadi lini? Akishakaa sana hapo itakuwa tabu tena bora tu arudi kama nyie wawili mmesameheana.mapenzi ni ya wawili hao wakwe watulie.ila usimkwaze tena mkeo hatokuamini tena.
 
Tafuta wazazi wa pande mbili wakae huenda wao wakapatana juu ya swala lako. Kama tujuavyo kuwa kwa watu wazima hakuharibiki jambo. Usije ukakubali mke wako atoroke aje muishi wote hiyo ni hatari sana kwan mzazi wake hakuridhia suala hilo na Je! Akipata tatizo we utakuwa mgeni wa nani???
 
Iko hivi, kwakuwa mkeo kakusamehe kabisa haina shida mruhusu aje kwako.Ila zingatia hay a:

1.Tambua kuwa mama mkwe na wewe bado hamjahafikiana.

2.Tambua mama mkwe wako hayupo tayari mkeo arudi kwenye ndoa yake.

3.Tambua kuwa mkeo anatoroka bila ridhaa ya mama yake.

4. Hivyo tambua kuwa mkeo teyari nae atakuwa kamkosea mama yake, hivyo nyote mtakuwa maadui kwake.

MATOKEO IKIWA UTAPUUZIA HAYO.
-Ukirudia tena kumfanyia ukatili mkeo, ambao hadi wewe umekiri kuwa hukutegemea kusamehewa kwa ukatili uliyomtendea. Basi hapa utakuwa umeharibu mwelekeo wa mkeo kabisa.

KWANINI?

-Kwasababu mkeo amekuthamini sana wewe kuriko ndugu zake hasa mama yake. Hivyo wewe ndio utabaki kuwa sehemu ya furaha na amani kwake.

NB. Ukiishi nae kwa upendo, amani na furaha basi tambua mama mkwe atakusamehe na kuwa upande wenu mda si mrefu. Ila ukiharibu tena utambue kuwa mkeo kwao atarudi kwa fedheha na kunyanyasika sana kwa kitendo cha kutoka bila ridhaa ya mama yake.

MKEO KAKIHESHIMU NA KUKITHAMINI SANA KILE KILICHO KUSUKUMA HADI UKAENDA KUMWOMBA MSAMAHA. HIVYO NAWEWE YAKUPASA UTHAMINI KILE KILICHO MFANYA AKUSAMEHE.

.............KILA LA HERI...................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom