98% hawamtaki JK na CCM

drgeorge

Member
Jun 22, 2009
99
23
Utafiti binafsi: 98% ya watu ninaokutana nao na kuzungumza nao habari za siasa au wakiwa wanazungumza habari za siasa hueleza kutoitaka CCM na JK. hii ni pamoja na nyumbani, chuoni, hospitalini, hotelini, kwenye migahawa, dukani, sokoni, kwenye foleni za benki, kwenye daladala, kwenye taxi, kwenyevituo vya daladala, na kwenye vijiwe vyangu ninavyopendelea kukaa.

Wengi husema rais wao ni Dr Slaa. kwa mfano katika hospitali ilikuwa ni ndani ya chumba cha upasuaji (Thietre), hii inaonesha ukubwa wa tatizo.

Naomba member wa JF, hebu niambieni kwa upande wenu hali ikoje? maana isijekuwa ni mimi ninayewasikia vibaya au wanasema wanaponiona tu, maana na mimi rais wangu ni Dr W. Slaa
 

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
974
Yaliyonipata juzi nilidhamiri niyaandika lakini wewe naona umeni-time.

Mimi ni naipenda CHADEMA lakini ukifuatilia thread zangu utaona nilivyochukizwa na watanzania tulivyozembea kuacha Tume ijumlishe kituo kwa kituo wakati tulitakiwa kuwa na matokeo ya vituo vyote tujumlishe wenyewe ili tuwasakame vizuri tume.


Humu JF nimeliongelea sana, na wa kunipinga kabisa hawakuwemo. Baadhi wamekiri na kunikubalia kuwa 2015 hatutafanya uzembe ule. Ninafurahi kuwa JF wamenielewa.

Kunielewa huko JF kukanivimbisha kichwa nikaipeleka mada hii ofisini ambako kweli siku hizi u-CHADEMA na u-CCM umechukua nafasi ya SIMBA na YANGA.

Nikadhani kule nako nitapata kuheshimiwa kama nilivyoheshimiwa humu JF. KUmbe sivyo. Ile kutaja tu kwamba watanzania na wanaCHADEMA tumefanya uzembe aisee kila mmoja alikuja juu kwa ubishi mkali.

Mwisho mmoja akaishiwa uvumilivu na kunitamia "Wewe tukikupekua tunaweza kukuta na kadi ya CCM".

Sina hakika kama hadi leo jamaa zangu hawa wananiamini maana wananiita mwana-CCM.

Je, unatathmini nini hali hii? Kumbuka hapo ni ofisini.

Zamani, na wala si zamani sana, juzi tu kabla Dr. Sla hajajitokeza kwenye urais hali ilikuwa tofauti. Pale ofisini kwetu hakukuwa na ushabiki wowote wa kisiasa licha ya kelele ndogondogo za mtu mmojammoja.

Binafsi napenda msuala ya kisiasa na hivyo nilkuwa nakosa kabisa mtu wa kujadili naye kwanza kumugopa mwajiri akigundua tunajadili siasa au chama chochote.

Waajiri wetu wengi tunajua ni wafanyabiashara baadhi yao ni walioitikia ule wito wa kwamba ukitaka biashara zako zikunyookee njoo CCM. Baadhi ni watu wenye share kweny ajira nyingi.

Hivyo moyoni mwangu nimekuwa mwoga sana kuongea siasa ofisini na hata nikimsikia mtu anaongea najua labda katumwa tu huyo kujua tunawazaje na hivyo ilikuwa namkwepa.

Alipojitokeza Shyrose nikajua huko NMB aliko kunaweza kuse na matatizo sana lakini vilevile nikajiuliza ni nani kwenye ajira anaweza kujitokeza akagombee CHADEMA halafu aendelee kubaki. Achilia kugombea je, ni nani humu ofisini anayweza kutamka hadharani kuwa anaipenda CHADEMA kwa dhati kama Shyrose alivyofanya kule NMB na kama nilivysikoa jamaa wa CRDB kwenye jimbo fulani!

Ukweli ni kwamba ilikuwa ni kama laana ukisema unaipenda waziwazi CHADEMA kwenye maeneo ya ofisini hasa ofisi nilizowahi kufanyia kazi. Huko hata magazeti litaletwa la MTANZANIA lakini TANZANIA DAIMA haliletwi.

Nilianza kuona dalili wiki baada Dr. Slaa amechukua formu za uraisi na bbosi wa idara moja akanikutiliza nasoma makala ya Joseph Mihangwa kwenye gazeti la RAI. Aliniuliza kwa mshangao "Wee unasoma RAI, inabidi tukufuatilie". Nilijua ni utani.

Upepo wa Dr. Slaa ulipozidi uoga maofisini ukaisha. Watu sasa wakawa haogopi si kuongea kuhusu Dr. Slaa bali email za wazawazi zikawa zinatembea ofisi zote tena email za kazi si zile za yahoo na hotmail. Eail zikitaja waziwazi tumchague Dr. Slaa.

Kumbe hata ofisi zingine nchi hali ilikuwa hivyohivyo. Unapata email toka kwa rafiki yako lakini ukiangalia chain unaona humo walibadilishana ndani ya shirika au kampuni. Waliojiamini zaidi ni wapenzi wa CHADEMA.

Ule woga na aibu ya kujulikana kama mpenzi wa CHADEMA sasa imekuwa kinyume. Zamani ukipenda upinzani na uko kazini ukiwa na jambo unaangalia kulia na kushoto kuona ni nani yuko karibu na humuamini. Ukiona hali mbaya unamvuta pembeni mwenzako.

Siku hizi aibu ile ninaona dhahiri inawapata wapenzi wa CCM. Wametangazwa na tume kushinda uchaguzi lakini sijui ni lini watazoea mazingira ya kuzungukwa na CHADEMA wengi maofisini.

Ndiyo hali ile iliyonipata nimeieleza mwanzo kwamba ilibidi wenzangu ofisini waniulize "wanahisi nina kadi ya CCM". Jibu ambalo humu JF sijaliata lakini ofisini nimelipata tena si mara moja.

Anayeamua kutoniamini shauri yake lakini nausema huu ukweli nilioushuhudia kwa macho na masikio.

Wapenzi wa CHADEMA wanatembea kifua mbele kana kwamba wao ndiyo wamekamata dola. Wanaongea kwa kujiamini, bila woga tena. Ninakifananisha kabisa kama ninavyoona humu JF. Tena afadhali humu JF tunaficha ID zetu na hivyo CCM wanachomokachomoka mmojammoja lakini huko maofisini social climate si nzuri kwao.

Ilifika mahala pale ofisin nikamuuliza mwenzagu mmoja wa idara nyingine kwamba: "Hivi CCM ikiamua kwa hasira na kuamua kuwatuma kisiri waajiri wote nchini na kuwaashawishi wawafukuze kazi hata kwa mbinu wapenzi wote wa CHADEMA hali itakuwaje hapa taasisini kwetu"

Jamaa alinijibu hakika taasisi tunayofanyia kazi atabaki na watu kumi tu! NIkamuuliza na kwa taasisi zingine ambazo wenye share au wamiliki wakiamua kufukuza vile. Akanijibu kwamba kama wana share basi shareholders wenzake watamuambia aondoe share zake maana anataka kuua shirika au kampuni kwani wafanyakazi wataisha wote.

Hii maana yake ni nini. Maana yake ni kwamba hali ya kutopendwa CCM ni kubwa kuliko tunavyojua. Mpenzi wa CCM wakati mwingine unamhurumia maana baadh yao hawataki kuongea kabisa siasa sasa hivi na lakini wanashindwa kuzuia moto uliolipuka wa wapenzi wa CHADEMA maofisini.

Kabla ya June mwaka huu ilikuwa ni wazi kuwa ukitaka ubunge wewe nenda kagombee ndani ya CCM uhakikishe unashinda kura za maoni. Juzi nimemuasa rafiki yangu kwamba sasa hivi ukitaka kugombea ubunge au kuwekeza kwenye siasa kwa vijana kama sisi basi ingia moja kwa moja na waziwazi CHADEMA leo hii. Utapata misukosuko sanasana miaka hii minne lakini pale 2015 hutakuwa mwenzetu tena.

Nashauri kwamba viongozi wa CHADEMA wasahau machungu ya uchaguzi huu kwani wana kambi kubwa maofisini. Wengi hata mimi hatukujutayarisha mwaka huu na hivyo tulianza moto siku Dr. Slaa alipojitokeza.

Slaa alijitokeza Julai uchaguzi ni October. Hivyo tulikuwa na miezi mitatu tu kujiandaa na kisiasa haitoshi. Sasa muda wa kujiandaa ni mkubwa zaidi yaani miaka mitano.

Makamba ameijua hali hii na ndiyo maana amesema "Watanzania tutasahau na tutaichagua CCM". Nashukuru ameifahamu lakini afahamu kuwa tunajiandaa vilivyo.

Na kwa wingi huo CHADEMA nawahurumia kwa sababu kuna wengi wanataka kuwasaidia kimyakimya bila kujulikana. Wakubalini hao na mtunze siri zao. Lakini wapo watakaotaka kutoa ushauri. Hapo ni pagumu kwa sababu mamluki pia waweza kuwa wengi.

Hivyo, mleta mada, hata kama kiwango cha asilimia ulicholeta cha upenzi wa CHADEMA hujakifanyia utafiti, mimi nakuunga kwa kusema kimapenzi hali ya CCM ni taabani kama vile mke na mme walionunia a wanasubiri kero ndogo itokee wapate mwanya wa kukoromeana.

Hivyo hapa tulipo ndipo kwa mtizamo wangu kwamba sasa siasa zimeanza. Miaka hii mitano tujikite na mengi lakini tu-exahaust mbinu zote za uchakachuaji za dunia hii. Mimi nitaendelea kulia na ileile kwamba ikifika Januari 2015 tuanze kukumbushana madai ya kuletewa idadi ya kura za wagombe kituo kwa kituo. Ikifanyika hivyo utanisikilizia hofu itakayojengeka kwa wanapoenda kura zilizojumlishwa na Tume kana kwamba kuna kifungu cha sheria kimekataza magazeti yasitangaze matokeo ya vituoni.

Na wasiozijua sheria waanze lkuzisoma leo nikiamini ndani ya miaka mitano tutalinagana uelwa na hatutababaishwa.
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,396
58,208
well said, nadhani hata watoto wadogo wanampenda Dr wa ukweli,hivi wamama wetu wajawazito washaanza kupewa mabajaji yao?
 

RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,369
1,516
Tutabaki tunalalamika tu humu jamvini bila bila action wakati muda unaenda. We need to take action, viongozi wa Chadema inawezekana wanasubiri pressure group kutoka kwa wanachama watiifu kama wewe na mimi hapa jamvini tujitoe na kuonyesha muongozo. Hivyo basi, tunaweza kuandika historia mpyaa kama tutajitoa hata kwa kutoa walaka mzito kwenda kwa viongozi wetu, wananchi na sehemu zingine husika.

Chadema ni yetu sote siyo ya Dr Slaa au Mbowe au Mtei, wote tumechangia vijisenti vyetu wakati wa uchaguzi, wakati mwingine tumelazimika kutembea umbali mzrefu ili tuweze kuchangia hizo mia mia au mia mbili au elfu moja au hata zaidi kuona Dr Slaa anashinda. Hivyo, naimani kila mtanzania anauchungu kuibiwa kura yake na mtu anayeitwa rais wakati si kwa matakwa ya wananchi.

Maoni yangu:
Tutoe tamko letu kama wanajamvi hapa, tunaopenda mabadiliko katika nchi yetu. Tunaweza kutumia ID zetu hizi ili kuupeleka kwa viongozi wetu wa Chadema kuchukua hatua kali zaidi.

Naimani sote hapa tunapenda kuona watu/watanzania wote wakiishi katika maisha yenye amani, haki ikitendeka, na watu wakiishi bila kubaguana wala katika misingi udini au ukabila.
 

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
399
Utafiti makini ukifanywa utaonyesha jinsi Chadema inapendwa na watanzania wengi. Hivi sasa ukiongelea ccm hadharani utaishia kusonywa tu. Binafsi nilifanya hivyo nikiwa kwenye basi kutoka DSM kuelekea Dodoma ghafla karibu abiria wote walinigeukia na kuniangalia kwa jicho kali. Wasio na uvumilivu walisonya. Jamaa mmoja akalipuka na kusema 'ngoja 2015 tutaonana tu hatutakubali ushindi uende tena kwa vibaka'. Hakika ccm ina kibarua kigumu.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom