95% ya watu duniani wameathirika na soul viruses(virusi vya nafsi)

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Soul viruses

Ni dhahiri kuwa moja Kati ya janga kubwa ni uwepo wa virusi vya ukimwi(HIV) ambavyo vikiingia kwenye mfumo wa damu vinaenda kuharibu kinga ya mwili.
Virusi vya ukimwi huenezwa kwa njia mbali mbali lakini njia kuu ikiwa ni ngono isiyo salama, maambukizi kutoka kwa mama aliyeathirika kwenda kwa mtoto,Nk

Hivyo humpelekea mtu kupatwa magonjwa ya kila aina..Mara utasikia kifua kikuu, kuharisha,mkanda wa jeshi sijui mapele na madonda ya kutosha! Ili mradi kila gonjwa linalokuja halipati pingamizi na hata kupelekea vifo vingi sana.
Ila siku hizi kuna dawa za kurefusha maisha na humfanya muathirika aishi kwa MATUMAINI.

Vivyo hivyo kwenye mfumo wetu wa nafsi(astral body) pia huwa kuna virusi vinavyoingia na kuharibu kinga ya nafsi zetu.
Virusi hivyo huingia kwa njia ya milango mitano ya fahamu na kupeleka taarifa kwenye ubongo.
Virusi hivyo huenda na kuharibu mifumo yetu ya kiakili(mind) ivyo kupelekea kinga ya nafsi ambayo ni fikra kuwa affected na viruses.

Madhara ya kinga ya nafsi kupungua(soul CD4) hupelekea magonjwa mengi kuibuka na kuanza kudhoofisha nafsi zetu na kujikuta tukisumbuliwa na magonjwa Kama Chuki,uzinzi,ulevi,kukata tamaa, msongo wa mawazo,kujikataa na mengine mengi.

Kibaya zaidi virusi hivi hushambulia hadi nguvu yetu ya maamuzi(will power) na tunashindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi au kutofanya maamuzi kabisa!
Hii Hali hupelekea vifo vingi maana watu wengi hujinyonga,overdose ya madawa ya kulevya,ajali,kuvunjika kwa mahusiano hata kujitoa mhanga.

Nadhani 95% ya watu wengi duniani tumeathirika na virusi vya nafsi ambavyo vinaendelea kushambulia kinga yetu(fikra) kwa Hali ya juu Sana.

Kibaya zaidi hatuhangaiki kutafuta ufumbuzi wa kumaliza hili janga la virusi vya nafsi,hatutaki hata kuliongelea kama janga la ukimwi linavyoongelewa.

Lakini ipo dawa itakayotuponesha kabisa, itakayotuweka huru na kuturudishia kinga zetu za nafsi.
Dawa ni Yesu Kristo,tumpokee,tuishi kwa MATUMAINI ya kumtumainia yeye.
Be blessed.
 
Back
Top Bottom