Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,052
- 12,904
Kadri siku zinavyoenda lugha yetu adimu ya kiswahili inazidi kuchimbiwa kaburi.
Leo vijana wetu hawawezi kuongea kiswahili fasaha kwa dakika 5 mfululizo, lazima aweke na neno au maneno ya kingereza.
Kwa vijana wa kike hali ni mbaya zaidi, wao imefikia hatua sasa hata kuongea kiswahili wanaona aibu, wanaona kama wanadhalilika na kuona kua kingereza ndio hadhi yao.
Leo wakati Julius Malema anahutubia wafuasi wake amependekeza Afrika kua na lugha moja na akapendekeza Kiswahili kiwe lugha ya Afrika.
Cha ajabu njoo kwa watanzania, kiswahili kinazidi kupoteza mvuto kila kukicha, kuanzia kwa viongozi wakubwa hadi kwa wananchi. Kiongozi mkuu hawezi kuongea bila kutupia kingereza maneno mawili matatu.
Siku sio nyingi Tanzania tutakua kama Kenya, neo moja la kiswahili matano ya kingereza.
Ni lazima zifanyike jitihada za maksudi kuhusu hii lugha vinginevyo itapotea.