95% ya vijana wa sasa hawawezi kuongea kiswahili fasaha kwa dakika 5. Vijana wa kike hali ni mbaya zaidi.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,902
Kadri siku zinavyoenda lugha yetu adimu ya kiswahili inazidi kuchimbiwa kaburi.

Leo vijana wetu hawawezi kuongea kiswahili fasaha kwa dakika 5 mfululizo, lazima aweke na neno au maneno ya kingereza.

Kwa vijana wa kike hali ni mbaya zaidi, wao imefikia hatua sasa hata kuongea kiswahili wanaona aibu, wanaona kama wanadhalilika na kuona kua kingereza ndio hadhi yao.

Leo wakati Julius Malema anahutubia wafuasi wake amependekeza Afrika kua na lugha moja na akapendekeza Kiswahili kiwe lugha ya Afrika.

Cha ajabu njoo kwa watanzania, kiswahili kinazidi kupoteza mvuto kila kukicha, kuanzia kwa viongozi wakubwa hadi kwa wananchi. Kiongozi mkuu hawezi kuongea bila kutupia kingereza maneno mawili matatu.

Siku sio nyingi Tanzania tutakua kama Kenya, neo moja la kiswahili matano ya kingereza.

Ni lazima zifanyike jitihada za maksudi kuhusu hii lugha vinginevyo itapotea.

Julius Malema naye chenga kwa Afrika lugha yenye wazungumzaji wengi ni kiarabu sasa kivipi kichaguliwe kiswahili ambacho kimesambaa eneo dogo?
 
Nadhani kwa kuwa kiarabu kimefungamanisha na dini fulani ndio maana akapendekeza kiswahili.
 
Kadri siku zinavyoenda lugha yetu adimu ya kiswahili inazidi kuchimbiwa kaburi.

Leo vijana wetu hawawezi kuongea kiswahili fasaha kwa dakika 5 mfululizo, lazima aweke na neno au maneno ya kingereza.

Kwa vijana wa kike hali ni mbaya zaidi, wao imefikia hatua sasa hata kuongea kiswahili wanaona aibu, wanaona kama wanadhalilika na kuona kua kingereza ndio hadhi yao.

Leo wakati Julius Malema anahutubia wafuasi wake amependekeza Afrika kua na lugha moja na akapendekeza Kiswahili kiwe lugha ya Afrika.

Cha ajabu njoo kwa watanzania, kiswahili kinazidi kupoteza mvuto kila kukicha, kuanzia kwa viongozi wakubwa hadi kwa wananchi. Kiongozi mkuu hawezi kuongea bila kutupia kingereza maneno mawili matatu.

Siku sio nyingi Tanzania tutakua kama Kenya, neo moja la kiswahili matano ya kingereza.

Ni lazima zifanyike jitihada za maksudi kuhusu hii lugha vinginevyo itapotea.

Uko sawa kabisa. Yaani mtu kuongea kiswahili bila kuchanganya kiingereza hawezi na kuongea kiingereza bila kuchanganya kiswahili hawezi. Kwa hiyo mbumbumbu wa lugha zote mbili!
 
Wakuu hivi muundo wa lugha umezingatiwa hapa??
Naombeni mnijuze

"Nimefurahishwa kwa kutumia Kiswahili kukizungumza nchini Marekani"
Screenshot_2018-08-18-14-21-43.png
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom