93% Ya Watanzamia wanaamini Ushirikina

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,980
3,578
Habarini wanajumvi
Katika tafiti iliyofanywa na asasi ya Washington DC inayoitwa PEW Research Center matokeo yanaonyesha kuwa
93% ya watanzania wanaamini katika masuala ya ushirikina.
Ilihali wenzetu Uganda ni 29% na Kenya 27%.

Matokeo haya yana mtizamo gani?
Je Tanzania tuna idadi ndogo ya wasomi kuliko Kenya na Uganda?

Je ni kwa nini watanzania wanaamini zaidi katika ushirikina??

Idadi ya Misikiti na Makanisa kuna umuhimu ikaongezwa zaidi?

Imani ya watanzania katika ushirikina ina uhusiano na maendeleo au umaskini uliopo kwa sasa?
NAWAZA TU BILA KUPATA MAJIBU.
 
Washington DC ndio walifanya utafiti! makubwa hayo: haya ngoja nikae pembeni nisubiri kusoma comments za wenzangu
 
Aiseee! Inawezekana lakini maana hata humu jamvini kuna wadau kadhaa wanajihusisha na mambo ya "ndumba nangai "
 
Habarini wanajumvi
Katika tafiti iliyofanywa na asasi ya Washington DC inayoitwa PEW Research Center matokeo yanaonyesha kuwa
93% ya watanzania wanaamini katika masuala ya ushirikina.
Ilihali wenzetu Uganda ni 29% na Kenya 27%.

Matokeo haya yana mtizamo gani?
Je Tanzania tuna idadi ndogo ya wasomi kuliko Kenya na Uganda?

Je ni kwa nini watanzania wanaamini zaidi katika ushirikina??

Idadi ya Misikiti na Makanisa kuna umuhimu ikaongezwa zaidi?

Imani ya watanzania katika ushirikina ina uhusiano na maendeleo au umaskini uliopo kwa sasa?
NAWAZA TU BILA KUPATA MAJIBU.
Hii kitu ni kweli kabisa kama unabisha anglia viongozi wetu. Juzi kunakiongozi kasema ataloga watu kutumia albadil
 
Kipindi cha vuguvugu la uchaguzi mkuu mauaji ya Albino na watu kunyofolewa viungo yanashamiri sana
 
Tanzania si waliosoma wala wasiosoma,wote kwa pamoja wanamini ushirikina.

Imefikia hatua hata kufanikiwa kwa baadhi ya watu,kunahusishwa na ulozi,na si vigezo vingine vyenye mantiki zaidi.
 
Kama unamuamini Mungu na Biblia ntakushangaa utakapokataa uwepo wa nguvu za giza,unategemea shetani anaoperate vipi?
 
Kuamini ushirikina ni kitu kimoja, kufuata ushirikina ni kitu kingine!!!
 
Hizi tafiti nyingine za wazungu ni za ajabu sana unapoongelea ushirikina manake ni full package
Sisi bado sana kwenye ishu za ushirikina
Huko kwao wamefika mbali mpaka kuwa na vyuo na taasisi rasmi za kishirikina wana majarida vipindi vya tv na hata makongamano
ba0b70ae777adb55ab59862da9d3a692.jpg
c5dab0efd5ffb9e8cfed4d685d4b884c.jpg
ce0f97d8f1260c9e5ed8e51f1c821565.jpg
2fc9ef725abb62cc41b1fbc203fcc060.jpg
sisi bado sana hatuna hata chuo kimoja cha uchawi kinachotambulika rasmi
 
Ushirikina,Ukristo na Uislam vyote ni kitu kile kile,ni imani tu

Kuamini uchawi unaofanyika makaburini,

Na kuamini miujiza inayofanyika makanisani zote ni imani za kishirikina

Thereby,huko kulipofanyika utafiti ndio kuna ongoza kwa ushirika kwasababu makao makuu ya makanisa mengi yapo huko
 
Habarini wanajumvi
Katika tafiti iliyofanywa na asasi ya Washington DC inayoitwa PEW Research Center matokeo yanaonyesha kuwa
93% ya watanzania wanaamini katika masuala ya ushirikina.
Ilihali wenzetu Uganda ni 29% na Kenya 27%.

Matokeo haya yana mtizamo gani?
Je Tanzania tuna idadi ndogo ya wasomi kuliko Kenya na Uganda?

Je ni kwa nini Watanzania wanaamini zaidi katika ushirikina??

Idadi ya Misikiti na Makanisa kuna umuhimu ikaongezwa zaidi?

Imani ya watanzania katika ushirikina ina uhusiano na maendeleo au umaskini uliopo kwa sasa?
NAWAZA TU BILA KUPATA MAJIBU.

Tafiti hiyo inaacha maswali mengi. Moja matokeo hayo ni ya ki-Majimbo, kiBara ama ki-Dunia? Zipo nchi zinaizidi Tanzania kwa hilo hapa Afrika na hata ulimwenguni? Je waliuliza maswali gani kwa walengwa? Waliuliza swali kama "unadhani uchawi upo?" Ama waliuliza: "wewe unaamini katika uchawi?" Ama waliuliza: Unaamini uchawi upo? Kwa mfano India kuna dini inayoamini kuna miungu milioni 30. Katika dini hiyo kila kitu chaweza kuwa Mungu na Mungu yupo katika kila kitu. "Panatheism" na "Pantheism" kwa kiingereza. Ushirikina ninayoulewa mimi ni kushirikiana na mambo ya kichawi katika upana na uwingi wake kwa kina ama kwa uchache tu. Kiingereza neno linalotumika kujumuisha hayo yote in "occult." Biblia inautaja ushirikina kama upo. Je huko ni kuamini katika huo? Tena Biblia inautaja ushirikina katika upana wake (Kumb 18 : 9 - 14).

9Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. * 10Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, * 11wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. * 12Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. * 13Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. * 14Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.

Biblia ni mfano tu wa haraka nilioutumia. Uchawi unatajwa mahali pengi katika Biblia. Yaani, Biblia inatambua uchawi upo.Je kimekuwa kitabu cha uchawi kwa sababu hiyo? nadhani wangekuwa na vipengele vya kufuatilia ukweli wa kushamiri jambo hili kwa kutazama pia kama kuna dini ambazo zipo nchini zilizojumuisha ushirikina na Ukristo (kwa mfano) katika Ibada zao. Hili lipo sana Visiwa vya Karibeani. Utakuta huko upo Ukristo ambao umeingiza ushirikina kabisa. Haiti lipo dhehebu la kikatoliki ambalo limechanganya na ushirikina.Niliona huko Brazil dini ambazo zimesheheni taratibu za kishirikina kama vile dini ya "Umbanda."

Kwangu mimi kipimo kingekuwa kuwa na miungu mingi ya kigeni miongoni mwa wananchi, na kuwepo na dini (taasisi za kiimani) ambazo rasmi kabisa zimeshindwa kujitenga na ushirikina na kuujumuisha katika ibada zao. Kutegemea mirejesho tu toka kwa waaminio ndio utoe matamko kama hayo ni kutowatendea haki WaTanzania. Tungeweza kuwa pia na mifumo ya serikali ambayo inaendekeza ushirikina. Kwa asilimia hizo walizotoa walipaswa kutoonyesha jinsi ambavyo ushirikina umepenya hata serikalini maana waliomo serikalini ni WaTanzania wanaodaiwa kuwa washirikina zaidi. Kwa mfano zipo bendera za mataifa fulani Marekani ya Kusini zinaashiria miungu mikuu inayoabudiwa na asilimia kubwa ya wananchi hasa mungu jua "Ra". Naomba nisitaje nchi hizo hapa. Nao wametuzidi ikiwa walijumuishwa katika utafiti huo?

Kwa uelewa wangu, vielelezo vya kuwa WaTanzania ni washirikina vingeonekana hata katika maeneo mengine ya maisha ya WaTanzania. Miji yetu ingejaa sanamu za miungu wa kishirikina kama vile Paulo alivyoona Athene (Mdo 17: 22-23). Viongozi wetu wangevaa kijadi na kupepea usinga kwenye matukio ya kiserikali. Zingekuwepo siku maalumu za kutambika kitaifa kwa ajili ya nchi kama vile katika nchi moja kusini mwa Afrika ambapo mtawala mkuu huenda likizo kutambika kitaifa kila mwisho wa mwaka. Nilitembelea huko na wenzangu mwaka fulani tukataka kutembelea mheshimiwa huyo tukaambiwa: "Hamtaweza kumwona kwani huu ni mwezi wa matambiko ya [kiongozi]" huyo. Hawa nao wametuzidi kwa ushirikina jamani!

Hatuwezi kuwa washirikina asilimia 93 na tusiwe washirikina kwa vitendo na kwa dhahiri kama ilivyo katika nchi zingine zilizosheheni ushirikina kutuzidi; ingawa watafiti sampuli hiyo hawataki kuchimba zaidi na kutuletea matokeo halisi. WaTanzania wanaelewa ukweli kwamba ushirikina upo katika jamii yao hata kama wao wenyewe baadhi yao hawahusiki nao. Kama swali litaulizwa kiujumla kisha useme anaamini katika huo, hiyo tafiti si kweli kimatokeo. Kuna haja ya kuona proposal ya tafiti hiyo na maswali yaliyoulizwa ili kupima kama yalilenga kupata majibu yaliyotolewa ama yametafsiriwa vibaya kwa faida ya mtafiti. Mtafiti alifikaje kwenye hitimisho lake nayo ni muhimu kujua.Napinga matokeo ya utafiti huo kwa vigezo nilivyovitoa. Nahitaji kusoma kwa kina taarifa ya utafiti huo.

 
Back
Top Bottom