90% ya Madudu ya IPTL Yanatokana na Utawala wa Mkapa!!

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,496
29,843
Kwanza tuweke kumbukumbu sawa sawa manake kutokana na muda mrefu kupita watu wameshasahau origin ya IPTL. Aliyesaini Mkataba wa IPTL hakuwa JK bali William Shija!!

Bado haijafahamika ni nani hasa aliileta IPTL lakini taarifa mbalimbali zinadai Mechmar Holding Malaysia (largest shareholder wa IPTL) ililetwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM; Marehemu Horace Kolimba mnamo July 1994.

JK wakati akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini alishiriki katika hatua za mwanzo! Ni yeye ndie aliletewa proposal ya IPTL ili wazalishe na kutuuzia umeme.

Hata hivyo, ushiriki wa JK haukufika mbali sana kwa sababu miezi michache baadae, November 1994, Rais Ally Hassan Mwinyi alivunja Baraza la Mawaziri. JK akahamishiwa Wizara ya Fedha na William Shija akaletwa Nishati na Madini!!

Kwa mara ya kwanza, proposal ya IPTL ilifika Baraza la Mawaziri (Technical Committee) mwezi January 1995 na aliyeifikisha alikuwa waziri mwenye dhamana... William Shija!!!

Technical Committee wakaipiga chini Proposal ya IPTL na wakatoa sababu. Kutokana na hilo, TANESCO wakampa kazi Mtalaamu kutoka UK ili kuitathimini Proposal ya IPTL na kutoa ushauri wa nini cha kufanyika!

February mwaka 1995 Rais Mwinyi akamtimua kazi Augustino Lyatonga Mrema aliyekuwa Waziri wa Kazi na Vijana. Mrema alitimuliwa baada ya kukiuka kiapo cha Baraza la Mawaziri ambapo alitofautiana na serikali yake hadharani... Bungeni chini ya Chavda Scandal!!!

Hata hivyo Mrema alifanya hilo kwa makusudi!!! Alishakusudia kutoka CCM lakini alikuwa anatafuta namna ya kutoka kwa kishindo! Bahati ikawa upande wake likaja suala la Chavda na Mrema akalitumia.

Kwahiyo Mrema alitoka CCM as a HERO! Muda mfupi baada ya kutoka CCM, akaingia NCCR-Mageuzi!!!

REMEMBER, Mrema alikuja upinzani wakati upinzani ukiwa hauna nguvu kabisa kwa sababu ulikuwa umeanza takribani miaka 3 tu iliyopita!! Hiki ni kipindi ambacho Watanzania wengi waliamini kuchagua upinzani ni kuleta vita nchini! Hiyo ndiyo Proganda ya CCM iiyokuwa inatumika kuwatisha wananchi!!!

Kinyume chake, Mrema alipoingia NCCR Mageuzi upepo wa kisiasa nchini ulibadilika kabisa! Mrema alionekana wazi kwamba ni mwiba mchungu kwa CCM!!! Hata Baba wa Taifa alionekana wazi kumuogopa Mrema kiasi cha kufikia kumwaga povu hadharani pale aliposema "...I will never let my country go to the dogs!" (Please, hiyo ni idiom kwahiyo msitafsiri neno kwa neno msije mkapotosha!)

Huyo ndie Mrema wa 1995! Alikuwa hakamatiki wala hazuiliki!!! Watu walipigwa mabomu kila kona kwa ajili ya Mrema! Umaarufu wa Mtikila ulianza kupotea pale alipotoka London na kuingia tu Bongo akaanza kumponda Mrema ambae ndo kwanza alikuwa MPYA!

Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho ilikuwa ni Haramu kumsema vibaya Augustino Mrema!!! Hata baba wa Taifa alikuwa kila wakati akikumbwa na kejeli kwa ajili ya Mrema!!! Kejeli maarufu kabisa ni ile ya kumwambia kuhoji Mwalimu amesahau nini Ikulu ili watu wakamchukulie na aachane na siasa za Tanzania!

Hata idiom hiyo hapo juu niliyosema msiitafiri neno kwa neno msije mkapotosha watu kwa makusudi waliitafsiri neno kwa neno ili mradi tu kumchafua Mwalimu!! Wakadai Mwalimu amemwita Mrema mbwa... kwamba, eti amesea hawezi kuiacha nchi yake iende kwa mbwa!!!

Kwangu mimi hajatokea mwingine kama Mrema!!! Bado nakumbuka tukiwa school tulipomzomea Mkapa (Mgombea wa CCM) aliyejaribu kutupungia mkono watoto wa shule wakati habari ya mjini ilikuwa ni Mrema!!!

Huyo ndo Mrema wa 1995!

Si kwamba nimetoka nje ya mada kuzungumzia suala la Mrema hapa ... la hasha!! Sasa turudi kwenye IPTL.

Kama nilivyosema hapo awali, Proposal ya IPTL ilipigwa chini na Baraza la Mawaziri (Technical Committee). TANESCO nao wakaomba ushauri toka kampuni ya kigeni!

Bila kupepesa macho, kampuni ile ya London ikasema wazi kwamba IPTL itakuwa ni burden kwa taifa kwahiyo kaeni mbali nayo!!!!

May 1995, chini ya miezi 3 tangia Mrema aingie NCCR na kuanza kuitia pressure CCM, Waziri wa Maji, Nishati na Madini akaipeleka tena ile Proposal ya IPTL kwenye Baraza la Mawaziri... Technical Committee!

Ingawaje Ushauri wa Kitalaamu ulishasema IPTL ni bomu kwa taifa lakini safari hii Baraza la Mawaziri (Technical Committee) likaridhia proposal ya IPTL!!

Sasa kwanini nimemleta Mrema kwenye mlolongo wa IPTL?!

In short nashawishika kuamini kwamba CCM na serikali yake walihitaji pesa za haraka haraka ili waweze kumdhibiti Mrema!! Watanzania walishajitoa kufa kwa ajili ya Mrema hivyo CCM na serikali yake walihitaji nguvu ya ziada kupambana nae! Nguvu hii si nyingine bali ni pesa kwa sababu mabomu ya machozi yalisha-prove failure!!!

Tena CCM na serikali yake ili kujihakikisha wanapata pesa za rushwa kutoka IPTL, naamini waliwaahidi IPTL mambo mazuri zaidi!!! Tutayaona just by speculation!!!

Mkataba na IPTL ukasainiwa haraka haraka May 1995. Mkataba huu uliwataka IPTL kusimika mitambo ya Slow Speed Diesel Engines. Aidha hapo ilisainiwa Power Purchase Agreement (PPA) ya miaka 20 ambayo mkataba wa kununua umeme ungeisha mwaka 2015 !!!

Keep the dates above... mkataba ungeisha mwaka 2015 !!!!

Hujuma ya wazi ya IPTL ilianza 1997. Wakati kwenye mkataba waliambiwa wasimike Slow Speed Diesel turbines ambayo kimsingi ilikuwa ndiyo yenye viwango, IPTL wakasimika Medium Speed Diesel turbines kwa bei ile ile ya Slow Speed Diesel turbines. Hii medium speed haikuwa na ubora kama wa slow speed engines!

Habari zikavuja. Rais Mkapa akajifanya ufanyike uchunguzi kuhusu IPTL kukiuka mkataba juu ya mitambo ya kusimika!

Cha ajabu, mwezi mmoja tu baadae serikali ya yule yule aliyeitisha uchunguzi ikaridhia mitambo hiyo hiyo isiyo na viwango kutumimika!!!

Ni Dr. Abdallah Kigoda aliyekuwa Waziri wa Nishati ndie alihalalisha hujuma hiyo ya wazi!!!

Kufuatia suala la IPTL kusimika mitambo ya hovyo, TANESCO wakakimbilia ICSID!!! Hata hivyo, kama ilivyo kesi za TANESCO kwa IPTL, hiyo ikawa ndiyo kesi ya kwanza TANESCO kuangukia pua kwa maelezo kwamba, hiyo mitambo isiyo na viwango ilisimikwa mbele ya macho yao!!!!

Hapo juu nilisema "keep the dates above!"

PPA ilisainiwa mwaka 1995 na kwamba mkataba wa kuuziana umeme ungeisha mwaka 2015!

Katika hali ya ajabu kabisa, ilipofika mwaka 2002 PPA ikauhishwa... ikaanza tena upya! Ule mkataba wa 1995 ukapigwa chini na badala yake ukasainiwa mkataba mwingine mwaka 2002 ambao nao ungedumu hadi mwaka 2022... miaka 20!!!! Yaani walifanya kama ambavyo walifanya TICTS ambayo mkataba wake wa miaka 10 ukaongezewa miaka mingine 15 kabla ya ile 10 haijaisha!!

Kutokana na ukweli huo ndio maana nashawishika kuamini kwamba, ile 1995 CCM walihitaji pesa za kupambana na Mrema na ndio maana wakapuuza ripoti ya kitalaamu iliyosema wazi kwamba IPTL ni kimeo!

Na ndio maana nashawishika kuamini kwamba CCM na serikali yake wali-offer something bigger kwa IPTL... kwamba, PPA isingeanza 1995 kama mkataba unavyosema bali ingeanza pale IPTL watakapoanza kuuza umeme! So, badala ya kuanza 1995 ukaanza mwaka 2002 ili waendelee kututafuna hadi 2022 !!!

Na CCM na serikali yake wana historia ya kufanya ufisadi kila unapokaribia uchaguzi mkuu!! Uchaguzi wa mwaka 2005 waliifisidi EPA!

Aidha, ni huo mwaka 2002 ndipo ilipoanza sintofahamu kati ya VIP ya Ruge na Mechmar ya wa-Malay!!

Baada ya hizo sinema hapo juu ndipo ikazaliwa Escrow ambayo nayo inahitaji mdadala wa peke yake!!!

UPDATES:

Naona watu wanazungumzia suala la Simba Trust!!!

In short, tracing ya Simba Trust ni ngumu si kidogo. Kuna baadhi ya info hata ukisema ulipie bado ni ngumu kuzipata... hususani linapokuja suala la trustees.

But all in all, haya ndo machache kuhusu Simba Trust but still DIGGING:

Simba Trust ilikuwa registered Australia July 01, 2000 na ilikuwa active hadi December 31, 2000.

December 31, 2000 ikawa cancelled.

Ilipofika January 16, 2002 ikabadilika kutoka Simba TRust to THE Simba Trust!

Ilipofika Octoba 2, 2002 ikabadilika tena kutoka The Simba Trust na kuwa The Trustees for The Simba Trust!!!

Inapatikana Perth... address tuweke kapuni kwanza! Nilipokuja kuchoka ni pale nilipokuta wanajihusisha na Real Estate... nikashindwa kuunganisha dots!!

Itoshe tu kusema kwamba, kama hii nayo ni kampuni ya upigaji basi wapigaji wapo very smart! Nilipata jina moja au mawili. Nilihangaika sana kutafuta connection zao na Tanzania lakini ndo kwanza connection zinanielekeza London! Nikaachia hapo!!!!

Kwahiyo kuna kila dalili leo hii ukienda kuitafuta Simba Trust hutaikuta bali The Trustees For The Simba Trust!!!!
 
Mkapa kwa kweli inabidi akamatwe, yule mtu alipiga deal sana katika utawala wake. Mkewe Mama Anna kwao ni mafukara, ila baada ya Mkapa kuchukua nchi alinunua eneo kule Mbezi na kujenga majumba ya kifahari kupangisha maexpatriates, hizi hela alizitoa wapi? Mkapa na JK wote wakamatwe na kunyongwa ili heshima irudi.
 
Mkuu wa nchi ameshasema wazee hawapaswi kutajwa!!! Tena nadhani anatamani itungwe sheria kabisa ili mtu akiwataja wazee kwa ubaya tu, hapo hapo akamatwe!
 
CCM wote ni wapiga dili sema kila mtu anatumia njia tofautitofauti na staili ya peke yake ila Magufuli nae akimaliza muda wake watu hawataamini japo wachache washafahamu ni nini kinaendelea...ndipo ule usemi usemao "hata wewe"..utatimia
 
mkapa hakukosea kutuita yale majina pale jangwani,,,na kweli sisi ni hivohivo alivotuita,,kwa sababu hatatufanyiwe nini hatujielewi,,ata wafanye nini hatujielew,,,hata kenya ilishatuita hivyo sembushe baba yetu,,,,,kazi kulia ndanindani na kushikilia ushabiki wa kupuuzi,,,maneno yetu ya mwisho kama kimeuma sana ni tunamwachia mungu,,,,hate these coward words
 
uliyeandika huu uzi tafadhali andika na mengine angalau wanaopenda kusoma tujisomee tuzidi kupata ufahamu,,,wengine wakiona uzi mrefu wanabweka kama mbwa kaona uchawi kisa hawapendi kusoma,,,,tunatakiwa tusome katiba na baadhi ya sheria ili tujue haki zetu na kuheshimu sheria jameni,,tofauti tutaonewa sana na kupoteza haki
 
Kwanza tuweke kumbukumbu sawa sawa manake kutokana na muda mrefu kupita watu wameshasahau origin ya IPTL. Aliyesaini Mkataba wa IPTL hakuwa JK bali William Shija!!

Bado haijafahamika ni nani hasa aliileta IPTL lakini taarifa mbalimbali zinadai Mechmar Holding Malaysia (largest shareholder wa IPTL) ililetwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM; Marehemu Horace Kolimba mnamo July 1994.

JK wakati akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini alishiriki katika hatua za mwanzo! Ni yeye ndie aliletewa proposal ya IPTL ili wazalishe na kutuuzia umeme.

Hata hivyo, ushiriki wa JK haukufika mbali sana kwa sababu miezi michache baadae, November 1994, Rais Ally Hassan Mwinyi alivunja Baraza la Mawaziri. JK akahamishiwa Wizara ya Fedha na William Shija akaletwa Nishati na Madini!!

Kwa mara ya kwanza, proposal ya IPTL ilifika Baraza la Mawaziri (Technical Committee) mwezi January 1995 na aliyeifikisha alikuwa waziri mwenye dhamana... William Shija!!!

Technical Committee wakaipiga chini Proposal ya IPTL na wakatoa sababu. Kutokana na hilo, TANESCO wakampa kazi Mtalaamu kutoka UK ili kuitathimini Proposal ya IPTL na kutoa ushauri wa nini cha kufanyika!

February mwaka 1995 Rais Mwinyi akamtimua kazi Augustino Lyatonga Mrema aliyekuwa Waziri wa Kazi na Vijana. Mrema alitimuliwa baada ya kukiuka kiapo cha Baraza la Mawaziri ambapo alitofautiana na serikali yake hadharani... Bungeni chini ya Chavda Scandal!!!

Hata hivyo Mrema alifanya hilo kwa makusudi!!! Alishakusudia kutoka CCM lakini alikuwa anatafuta namna ya kutoka kwa kishindo! Bahati ikawa upande wake likaja suala la Chavda na Mrema akalitumia.

Kwahiyo Mrema alitoka CCM as a HERO! Muda mfupi baada ya kutoka CCM, akaingia NCCR-Mageuzi!!!

REMEMBER, Mrema alikuja upinzani wakati upinzani ukiwa hauna nguvu kabisa kwa sababu ulikuwa umeanza takribani miaka 3 tu iliyopita!! Hiki ni kipindi ambacho Watanzania wengi waliamini kuchagua upinzani ni kuleta vita nchini! Hiyo ndiyo Proganda ya CCM iiyokuwa inatumika kuwatisha wananchi!!!

Kinyume chake, Mrema alipoingia NCCR Mageuzi upepo wa kisiasa nchini ulibadilika kabisa! Mrema alionekana wazi kwamba ni mwiba mchungu kwa CCM!!! Hata Baba wa Taifa alionekana wazi kumuogopa Mrema kiasi cha kufikia kumwaga povu hadharani pale aliposema "...I will never let my country go to the dogs!" (Please, hiyo ni idiom kwahiyo msitafsiri neno kwa neno msije mkapotosha!)

Huyo ndie Mrema wa 1995! Alikuwa hakamatiki wala hazuiliki!!! Watu walipigwa mabomu kila kona kwa ajili ya Mrema! Umaarufu wa Mtikila ulianza kupotea pale alipotoka London na kuingia tu Bongo akaanza kumponda Mrema ambae ndo kwanza alikuwa MPYA!

Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho ilikuwa ni Haramu kumsema vibaya Augustino Mrema!!! Hata baba wa Taifa alikuwa kila wakati akikumbwa na kejeli kwa ajili ya Mrema!!! Kejeli maarufu kabisa ni ile ya kumwambia kuhoji Mwalimu amesahau nini Ikulu ili watu wakamchukulie na aachane na siasa za Tanzania!

Hata idiom hiyo hapo juu niliyosema msiitafiri neno kwa neno msije mkapotosha watu kwa makusudi waliitafsiri neno kwa neno ili mradi tu kumchafua Mwalimu!! Wakadai Mwalimu amemwita Mrema mbwa... kwamba, eti amesea hawezi kuiacha nchi yake iende kwa mbwa!!!

Kwangu mimi hajatokea mwingine kama Mrema!!! Bado nakumbuka tukiwa school tulipomzomea Mkapa (Mgombea wa CCM) aliyejaribu kutupungia mkono watoto wa shule wakati habari ya mjini ilikuwa ni Mrema!!!

Huyo ndo Mrema wa 1995!

Si kwamba nimetoka nje ya mada kuzungumzia suala la Mrema hapa ... la hasha!! Sasa turudi kwenye IPTL.

Kama nilivyosema hapo awali, Proposal ya IPTL ilipigwa chini na Baraza la Mawaziri (Technical Committee). TANESCO nao wakaomba ushauri toka kampuni ya kigeni!

Bila kupepesa macho, kampuni ile ya London ikasema wazi kwamba IPTL itakuwa ni burden kwa taifa kwahiyo kaeni mbali nayo!!!!

May 1995, chini ya miezi 3 tangia Mrema aingie NCCR na kuanza kuitia pressure CCM, Waziri wa Maji, Nishati na Madini akaipeleka tena ile Proposal ya IPTL kwenye Baraza la Mawaziri... Technical Committee!

Ingawaje Ushauri wa Kitalaamu ulishasema IPTL ni bomu kwa taifa lakini safari hii Baraza la Mawaziri (Technical Committee) likaridhia proposal ya IPTL!!

Sasa kwanini nimemleta Mrema kwenye mlolongo wa IPTL?!

In short nashawishika kuamini kwamba CCM na serikali yake walihitaji pesa za haraka haraka ili waweze kumdhibiti Mrema!! Watanzania walishajitoa kufa kwa ajili ya Mrema hivyo CCM na serikali yake walihitaji nguvu ya ziada kupambana nae! Nguvu hii si nyingine bali ni pesa kwa sababu mabomu ya machozi yalisha-prove failure!!!

Tena CCM na serikali yake ili kujihakikisha wanapata pesa za rushwa kutoka IPTL, naamini waliwaahidi IPTL mambo mazuri zaidi!!! Tutayaona just by speculation!!!

Mkataba na IPTL ukasainiwa haraka haraka May 1995. Mkataba huu uliwataka IPTL kusimika mitambo ya Slow Speed Diesel Engines. Aidha hapo ilisainiwa Power Purchase Agreement (PPA) ya miaka 20 ambayo mkataba wa kununua umeme ungeisha mwaka 2015 !!!

Keep the dates above... mkataba ungeisha mwaka 2015 !!!!

Hujuma ya wazi ya IPTL ilianza 1997. Wakati kwenye mkataba waliambiwa wasimike Slow Speed Diesel turbines ambayo kimsingi ilikuwa ndiyo yenye viwango, IPTL wakasimika Medium Speed Diesel turbines kwa bei ile ile ya Slow Speed Diesel turbines. Hii medium speed haikuwa na ubora kama wa slow speed engines!

Habari zikavuja. Rais Mkapa akajifanya ufanyike uchunguzi kuhusu IPTL kukiuka mkataba juu ya mitambo ya kusimika!

Cha ajabu, mwezi mmoja tu baadae serikali ya yule yule aliyeitisha uchunguzi ikaridhia mitambo hiyo hiyo isiyo na viwango kutumimika!!!

Ni Dr. Abdallah Kigoda aliyekuwa Waziri wa Nishati ndie alihalalisha hujuma hiyo ya wazi!!!

Kufuatia suala la IPTL kusimika mitambo ya hovyo, TANESCO wakakimbilia ICSID!!! Hata hivyo, kama ilivyo kesi za TANESCO kwa IPTL, hiyo ikawa ndiyo kesi ya kwanza TANESCO kuangukia pua kwa maelezo kwamba, hiyo mitambo isiyo na viwango ilisimikwa mbele ya macho yao!!!!

Hapo juu nilisema "keep the dates above!"

PPA ilisainiwa mwaka 1995 na kwamba mkataba wa kuuziana umeme ungeisha mwaka 2015!

Katika hali ya ajabu kabisa, ilipofika mwaka 2002 PPA ikauhishwa... ikaanza tena upya! Ule mkataba wa 1995 ukapigwa chini na badala yake ukasainiwa mkataba mwingine mwaka 2002 ambao nao ungedumu hadi mwaka 2022... miaka 20!!!! Yaani walifanya kama ambavyo walifanya TICTS ambayo mkataba wake wa miaka 10 ukaongezewa miaka mingine 15 kabla ya ile 10 haijaisha!!

Kutokana na ukweli huo ndio maana nashawishika kuamini kwamba, ile 1995 CCM walihitaji pesa za kupambana na Mrema na ndio maana wakapuuza ripoti ya kitalaamu iliyosema wazi kwamba IPTL ni kimeo!

Na ndio maana nashawishika kuamini kwamba CCM na serikali yake wali-offer something bigger kwa IPTL... kwamba, PPA isingeanza 1995 kama mkataba unavyosema bali ingeanza pale IPTL watakapoanza kuuza umeme! So, badala ya kuanza 1995 ukaanza mwaka 2002 ili waendelee kututafuna hadi 2022 !!!

Na CCM na serikali yake wana historia ya kufanya ufisadi kila unapokaribia uchaguzi mkuu!! Uchaguzi wa mwaka 2005 waliifisidi EPA!

Aidha, ni huo mwaka 2002 ndipo ilipoanza sintofahamu kati ya VIP ya Ruge na Mechmar ya wa-Malay!!

Baada ya hizo sinema hapo juu ndipo ikazaliwa Escrow ambayo nayo inahitaji mdadala wa peke yake!!!
Mkataba wa iptl ulisainiwa kipindi Cha Mzee Ruksa Na ulikuwa initially wa miaka 10 Na ulikuwa Na kifungu kwamba tukivunja mkataba tunalipa $100m.
Sema utejekezaji wa huo mkataba ulifanyika kipindi Cha Mkapa, ndio watu Kama Mwanasheria Mkuu Na Waziri wa Madini Na Nishati wa kipindi Cha Mkapa nao wakaingia dimbani Na kuweka hizo nyongeza zingine Za mkataba uwe wa 20 years etc etc . Ya Mrema nayaweka kando ili mjadala wa Hilo dude uwende vizuri .
 
Mleta mada kuna kitu unataka kupindisha. La msingi hapa kwa faida ya nani, mbona huu unaotaka kuwaaminisha watu, haukutolewa mapema? M msingi wake ni nini?
 
Back
Top Bottom