90% ya 'Antibiotic' zinatumika kutibu wanyama badala ya Chanjo Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,098
Serikali imetahadharisha matumizi mabaya ya dawa za antibiotiki ambazo zinasababisha usugu wa vimelea dhidi ya dawa, ikionya hatari ya kutokea madhara makubwa hasa kifo kwa watumiaji.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema jijini Dar es Salaam kuwa takwimu zinaonesha asilimia 92 ya antibiotiki zinatumika nchini zimesababisha usugu kwa asilimia 59.8.

Amesema eneo lililoathrika zaidi ni la uvuvi na ufugaji ambapo asilimia 90 ya dawa hizo hutumika kutibu wanyama badala ya chanjo.

“Tumetengeneza mpango kazi mpya wa kitaifa kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa,” amesema Profesa Nagu. “Tunategemea kupokea taarifa ya utekelezaji ya mpango kazi wa taifa wa mwaka 2017-2022.”
Tanzania inakabiliwa na usugu wa vimelea dhidi ya dawa, tatizo ambalo limeendelea kushamiri katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara.

HABARI LEO
 
Kama wameligundua Hilo n jukumu la serikali kutoa ruzuku kwenye hizo chanjo ziuzwe kwa Bei ambayo mkulima anaweza kuimudu i.e 2500/=


Na siyo kupiga tu kelele bila kuchukua hatua

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kama wameligundua Hilo n jukumu la serikali kutoa ruzuku kwenye hizo chanjo ziuzwe kwa Bei ambayo mkulima anaweza kuimudu i.e 2500/=


Na siyo kupiga tu kelele bila kuchukua hatua

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sasa shida hata hizo chanjo zenyewe hazipatikani kabisaaa mimi nilipatwa na goat pox nilifilisika kabisa
 
Back
Top Bottom