90 Minutes in raid on Entebbe: Tukio la ukombozi wa mateka wa Israel Nchini Uganda - THUNDERBOLT

90 minutes to entebe
Mkuu katika hivyo vita vya 6 days war Israeli iliishambulia Misri, Yordan na Syria na kuzishinda ndani ya siku sita. Mwazo vilikuwa ni vita kati ya Misri na Israeli baada ya mmisri kutwangwa na bila Yordan kujua kwamba Mmisri ametwangwa wakaingia kumsaidia Misri nao wakatwangwa. Siria nae akaingia kumsaidia Mmisri nae akatwangwa. Baada ya Israeli kuwashinda ndipo aliposhikilia na kukalia maeneo ya Sinai na Gaza strip kutoka misri na West bank kutoka Yordan na Golon heights kutoka Syria. Baadae ukisoma historia Israeli ilisaini mkataba wa amani na Misri na Israeli ikawarudishia Eneo la Sinai pia miaka ya karibuni Israeli ilisaini mkataba wa amani na Yordan wakaweka mipaka vizuri kati yao na kukubaluana kushirikiana katika baadhi ya mambo ikiwemo kufungua mipaka baina yao lakini bado west bank haikurudi Yordan. Mkuu hivyo vita nafikiri ndiyo ilikuwa chanzo cha kimoja wapo cha mgogoro kati ya wapalsstina na Israeli mpaka leo wapalestina wakitaka israeli iondoke katika maeneo yao waliokalia.offcourse kuna sababu zingine nyingi mojawapo ikiwa ni religious perspective ambapo Israeli wanaamini kwamba walipo ni katika ardhi takatifu walioahidiwa na Mungu kupitia Ibrahim na Isaka wakati waraabu nao wanaamini ni eneo lao walilopewa kupitia Kwa Ibrahimu na Ishmaeli. Mkuu nimekumegea tuu ....mengine utafute mwenyewe.
 
Wakuu kwema?
Samahani nimekua nikisikia tu story za kuwa israel waliwah kufanya operation kubwa kwenye uwanja wa ndege wa entebe,naomba kupewa fully details za nini kilichotokea na ulimwengu ulilichukuliaje hili tukio?
 
Imeandikwa na Josephat Keraryo Nyambeya

AMBATANA NA MIMI

Oparesheni Entebbe ni operesheni ya kuokoa mateka wa Kisrael waliotekwa na magaidi , oparesheni hii ilifanywa na makomando wa Israel (IDF) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe tarehe 4 July 1976, wiki moja kabla yaani tarehe 27 June ndege ya shirika la Air France ikiwa na abiria 248 ilitekwa na wanachama wawili wa chama cha vuguvugu a ukombozi wa Palestina (PFLP-EO) baada ya amri ya mtu aliyefahamika kama Wadie Haddad, pia katika utekaji huo kulikuwa na wanachama wawili wa vuguvugu za kimapinduzi huko Ujerumani.

Watekaji walikuwa wanadai Israel iwaachie huru wafungwa 40 na wengine 13 waliokuwa wamefungwa kwenye magereza mbalimbali nchini humo ili iwaachie mateka hao. Ndege hiyo iliyoanzia safari yake mjini Tel-Aviv nchini Israel ikiwa inatarajiwa kutua jijini Paris-Ufaransa ilibadilishwa uelekeo na kushuka jijini Athens-Ugiriki kwa ajili ya kujaza mafuta kabla haijapaa kuelekea Benghazi-Libya kasha Entebbe uwanja mkuu wa ndege nchini Uganda.

Serikali ya Uganda ilikuwa inawasapoti watekaji hao, na binafsi dikteta Idd Amin aliwakaribisha watekaji hao (huyu Idd Amin akili zake zilimtosha mwenyewe). Baada ya kuwaondoa mateka wote kutoka uwanjani na kuwapeleka kwenye jengo lililokuwa halitumiki hapo uwanjani, watekaji waliwatenganisha Waisrael na wasio Waisrael .

Siku mbili baadae mateka 148 ambao hawakuwa raia wa Israel waliachiwa na kurejea jijini Paris. Raia 94 wa Israel ikiwemo na wafanyakazi 12 wa shirika hilo la ndege waliachwa kama mateka na kutishiwa kuawawa .

Jeshi la Israel (IDF) lilizipata taarifa walizopewa na shirika la Ujasusi la nchi hiyo Mossad juu ya tishio la mateka hao kuuliwa kama Israel haitatii matakwa ya watekaji hao ambayo yalikuwa kuwaachia huru wafungwa wote wa Kipalestina waliokuwa kwenye magereza nchini humo. Kitisho hiki kilipelekea IDF kupanga misheni ya Uokozi, operesheni hii ilipangwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na Mapambano kutoka Jeshi la Uganda maana walijua fika kuwa endapo watafanikiwa kuingia Uwanja wa Entebbe kwa ajili ya uokoaji huo lazima wangekabiliana na upinzani kutoka jeshi la Idd Amini hivyo walijiandaa kwa ajili ya hilo.

Oparesheni ilifanyika usiku , Israel ilichukua ndege iliyobeba makomandoo 100 na kusafiri zaid ya Maili 2500 (Kilomita 4000) kuelekea Uganda kwa ajili ya uokozi. Oparesheni iliyochukua wiki nzima kuiandaa ilipangwa kuchukua dakika tisini tu kukamilika, Mateka 102 waliokolewa , makomando watano wa Israel walijeruhiwa, Kamanda aliyekuwa akiongoza Operesheni hiyo Lt. Kanali Yonathan Netanyahu aliuwawa. Watekaji wote, mateka watatu, na wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda waliuliwa . Pia ndege vita 11 za jeshi la Uganda ziliharibiwa.

Opareheni hii iliyopewa jina la fumbo (codename) la Oparesheni Thunderbolt, mara nyingine huitwa oparesheni Yonathan kama kumbukumbu ya Kiongozi aliyeiongoza oparesheni hii. Kiongozi wa oparesheni hii alikuwa kaka mkubwa Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa sasa wa Israel.

Katika uwanja wa ndege wa Entebbe watekaji wane waliungana na wenzao wanne wakiwa wanapewa sapoti na Jeshi la Uganda. Idd Amini alikuwa akiwatembelea mateka kila siku na kuwapa maendeleo ya mazungumzo juu ya kile kilichokuwa kikiendelea, na kuwaahidi kuachiwa huru kama maafikiano yatafikiwa. Tarehe 28 siku moja baada ya utekaji watekaji walidai fidia ya dollar Millioni 5 ili waiachie ndege na pia wapalestian 53 waliokuwa wamefungwa kwenye magereza ya Israel wachiiwe huru. Walidai kama madai yao hayatatekelezwa wataanza kuwaua mateka kuanzia tareh 1 July mwaka huo wa 1976.

Wiki hiyo Israel ilijaribu kutumia majukwaa ya kisiasa ili kuwaokoa mateka. Vyanzo vingi vinadai baraza la Mawaziri la Israel lilipanga na kukubaliana kuwaachia wafungwa hao wa Kipalestina ili kuokoa roho za waisrael hao waliotekwa. Burka bar-Lev afisa mstaafu wa jeshi la Israel alikuwa anamjua Idd Amin kwa mda mrefu alipewa jukumu la kumbembeleza Idd Amin ili awaachie mateka hao, Bar-lev alikuwa akimpigia simu mara nyingi Idd Amin kumuomba awaachie mateka bila mafanikio, Idd Amin hakuelewa somo. Israel iliomba Marekani kuongea na rais wa Misri Anwar Sadat aliyekuwa na mahusiano mazuri na Idd Amin kumuomba awaachie mateka bila mafanikio. Sadat alijaribu kuongea na PLO na seriakli ya Uganda , pia Mwenyekiti wa PLO wa kipindi hicho Yasser Arafat alituma ujumbe wake nchini Uganda kuongea na watekaji ila watekaji walikataa katakata kuonana na mjumbe huyo aliyetumwa.

Tarehe ya mwisho ilifika (yaani tarehe 1, July) na hapo baraza la mawaziri la Israel liliomba watekaji kusogeza mda hadi tareh 4 ili waweze kukubalina . Idd Amin pia aliwaomba wasogeze siku hadi tarehe hiyo hadi arudi kutoka kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika (Kipindi hicho OAU) alipokuwa anaenda kukabidi Uenyekiti wa mkuu mwingine wan nchi.

Kukubaliwa kwa ombi hili kuliwafanya Waisrael kujipanga zaidi jinsi ya kuifikia Entebbe. Tarehe 3 July saa 12:30 jioni Baraza la mawaziri la Israel lilibariki kufanyika kwa oparesheni hii, utekelezaji wa Oparesheni hii ukiwasilishwa na Meja Jenerali Yekutiel Kuti Adam na Brigedia Jenerali Dan Shomron mbele ya baraza hilo.

Mwanzoni operesheni ilipangwa kwa kuwadondosha makomando wa Kiyahudi ndani ya ziwa Vicktoria na kuwaacha watumie boti za mipira hadi kwenye ncha ya uwanja wa ndege wa Entebee ulipo pembezoni kabisa mwa Ziwa Vicktoria. Walipanga kuwauwa watekaji wote na kuwaokoa mateka, ila baadae Israel iliukaaa mpango huu kwa sababu ya kuwa walipata taarifa kuwa Ziwa Vicktoria lina mamba wengi hivyo ingekuwa hatari kwa mateka waliokolewa.

Wakati wakipanga oparesheni hiyo walijiuliza watajazia mafuta wapi kwenye ndege yao waliyopanga kuitumia kufika Entebbe, walikosa ndege ya kuweza kufika Entebbe na kurudi Israel bila kujazwa mafuta, hivyo kitu hicho kikawaumiza kichwa tena. Walipanga kuongea na moja ya mataifa ya Afrika ya Mashariki ili kuweza kuwaruhusu kutumia uwanja wao wa ndege kwa ajili ya ndege yao kutua na Kujaza mafuta. Katika kuitafuta nchi ambayo ingewakubalia ombi lao wakaamua kuichagua Kenya na kuwatuma mabalozi wake waliokuwepo nchini Kenya pamoja na wafanyabiashara wa Kiyahudi wenye ushawishi mkubwa nchini Kenya kwenda kuongea na Rais Jomo Kenyatta juu ya ombi lao hilo, msomaji naomba ufahamu kuwa Tanzania haikuwa na uhusiano mzuri na Israel kwa hiyo njia pekee iiyokuwepo ni kuitumia Kenya.

Oparesheni hii isingeweza kufanikiwa bila msaada wan chi yoyote ya Afrika Mashariki, waliotumwa kwa Kenyatta walibubujikwa na machozi ya furaha baada ya ombi lao la kuutumiwa uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kukubaliwa. Kenyatta pia aliwaruhusu MOSSAD kuitumia Kenya kama njia ya kukusanya taarifa za kiintalenjesia.

Mossad ilipata picha kamili ya mahali walipo mateka, idadi ya watekaji pia walizipata taarifa za juu ya uhusikaji wa Jeshi la taifa la Uganda kutoka kwa wale mateka walioachiwa na kurudi Paris (moja ya udhaifu wa watekaji hawa). Taarifa za mateka hao waliochiwa zililisaidia sana Jeshi la Israel na Mossad kujua idadi ya kikosi watakachokituma Entebbe.

Kama bahati ya mtende kuota Jangwani Mossad pia ilipata taarifa za kuwa kuwa Uwanja huo wa ndege wa Enttebe ulijengwa na kampuni moja la Kisrael mnamo mika ya sitini, hivyo iliwasiliana na kampuni hilo liitwalo Solel Boneh na kupata ramani kamli ya uwanja huo na majengo yaliyopo uwanjani hapo.

Kikosi kazi kikiwa na Makomandoo wapatao 100 na silaha nzito nzito walijindaa kuelekea Uganda. Kikosi kazi hizi kiligawanyika katika vitengo vitatu,

Moja, kamandi ya Ardhini iliyoongozwa na Brigedia dan Shomron na muwakilishi wa Kikosi cha anga Kanali Ami Ayalon, kikosi hiki kilikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha ulinzi unaimarishwa uwanjani hapo pamoja na kuyakata mawasiliano yote kutoka uwanjani hapo. Kikosi cha pli kikiongozwa na Kamanda kijana wa miaka 29 tu Luteni Kanali Yonathan Netanyahu kikosi hiki kilikuwa na makomando kutoka kambi ya Sayeret Matkal kilipewa kazi ya kuuteka uwanja wa ndege wa kuingia kwenye terminal na kuwaokoa mateka, Meja Betser alichukua nafasi ya kukiongoza kikosi hiki baada ya Yonathan kuuwawa kwa risasi. Kikosi kazi kingine kilipewa jukumu la kuzilinda njia za Kutulia ndege (runways-siko vizuri Kiswahili mnisamehe) na kulinda sehemu ya kujazia mafuta na kuhakikisha ndege za Israel zinajaza mafuta uwanjani hapo kabla ya kupaa (Yaani hii ni sawa na kuvamiwa na Majambazi ukiwa umelala na mkeo wewe unainamishwa nay eye anainamishwa mbele yako). Kikosi hiki kiliongozwa namakamanda watatu walikouwa na majukumu tofauti, kikosi hiki pia kilipewa jukumu la kuharibu ndege vita zote za jeshi la Uganda zilizokuwepo uwanjani hapo.

Kikosi hiki makini cha makomando wa kiyahudi kilipaa kutoka Sharm el-Sheikh ndege iliyowabeba makamanda hawa ikiwa inaruka umbali wa Mita 30 (futi 100) tu ili kuepuka kunaswa na Rada za Sudan, Misri na Saudi Arabia (kwa wataalamu wa RADAR nadhani watakubaliana na mimi) kilipita bahari ya shamu kuelekea Kusini na kasha kupita Djibouti kutoka huko walitua uwanja wa ndege jijini Nairobi, wakiwa na ndege mbili za Boeing 707 ndege moja ikiwa ikiwa imebeba madawa na vifaa tiba na ndege ya pili kikiwa imewabeba makamanda.

Jeshi la Israel lilitua uwanja wa Entebbe saa tano kamili usiku July 3, ndege ya mizigo ikiwa tayari imefunguliwa milango gari nyeusi aina ya Mercedes Benz iliyofanana na ile aliyokuwa anatembelea rais Idd Amin ilishuka kutoka kwenye ndege ikiwa imeambatana na Land Rovers kadhaa sawa na zile zilizokuwa zinampa Idd Amin eskoti, walizitumia hizi kupita check points zote za uwanjani hapo. Ndege ya pili iliyowabeba makamanda wa kazi ilitua dakika sita baadae na hapo hapo wakayadandia magari hayo kuelekea kwenye jengo walipo mateka wakiwa wanafanana sawa sawa kabisa na Idd Amin, wakiwa wamekaribia terminal ya pili Maaskari waliokuwa guard wakiwa wanatambua kabisa kuwa Idd Amin alikuwa siku chache zilizopita alikuwa kanunua Mercedes nyeupe na kuachana na ile nyeusi walisimamisha msafara huo, makomando hao waliwafiatulia risasi kwa kutumia bastola za sailensa lakini hawakuwaua lakini komando mmoja aliyekuwa kwenye rand Rover za msafara aliwamalizia kwa kutumia bunduki kubwa isiyotoa sauti.

Wakiwa wameingia kwenye jengo lililokuwa linawafuga mateka hawa makomando walipaza sauti kutumia Vipaza sauti wakisema kwa Kingereza na Kiebrania kuwa “KAA CHINI, KAA CHINI” sisi ni wanajeshi wa Israel , kijana wa Kiyahudi wa miaka 19 alijaribu kusimama na alipigwa risasi kwa kudhaniwa kuwa alikuwa mtekaji. Pia mzee wa miaka 52 aliuwawa kimakosa baada ya kujeruhiwa na risasi ya jeshi la nchi yake, pia mateka mmoja mwenye asili ya Urusi aliuuliwa kwa risasi ya watekaji.

Wakiwa wanaendelea na oparesheni hii makamanda wa kiyahudi waliwauliza mateka kwa kiebrania walipo watekaji wengine na waliwaonyesha kwa vidole kuwa watekaji hao wamejificha kwenye chumba kinachofuata, makomandoo walikibomoa chumba hicho kwa magruneti kabla ya kuingia ndani na kuwamiminia risasi watekaji hao wa Kipalestina.

Kipindi wakiendelea a zoezi hilo la uokozi ndege vita tatu aina ya C-130 zilitua uwanjani hapo ili kutoa ulinzi wa anga ikiwa pia na kuzilinda ndege za jeshi la israel zikiwa zinajaza mafuta uwanjani hapo, oparesheni ya kuwaokoa mateka pia ilienenda sambamba na kuziharibu ndege za jeshi la Uganda zilizokuwepo uwanjani hapo.

Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka kwenye ndege zao wanaeshi wa Uganda waliendelea kurusha risasi, wanajeshi hawa wa Uganda wakiwa wanarusha risasi kutoka mnara wa kuongozea ndege walifanikiwa kuwajeruhi makomando watano na kumuua Kiongozi mmoja wa oparesheni Luteni Kanali Yonathan Netanyahu, makomando wa Israel walirusha RPG (wanaojua dhana za kijeshi RPG siyo jina geni kwao) na kuuharibu kabisa mnara huo wa kuongozea ndege, kulingana na mmoja wa vijana wa Idd Amin askari aliyempiga risasi Yonathan Netanyahu aliuliwa katika majibizano hayo ya risasi.

Zoezi hili lilichukuwa dakika 53 pekee japo lilipangwa kuchukua dakika 90. Katika oparesheni hii jumla ya wanajeshi 45 wa Uganda waliuliwa, mateka wote wanane waliuliwa, komando mmoja wa Israel alikufa, pia makomando 5 kujeruhiwa, ndge vita 11 za jeshi la Uganda aina ya Mig-17s na Mig-21 zilliharibiwa, pia kati ya mateka 106 mateka 3 waliuwawa kama nilivyoelezea mwanzoni pia na mateka mmoja kikongwe wa miaka 75 alisahaulika Uganda kikongwe huyu alichukiliwa nakupelekwa hospitali ya taifa ya Uganda-Mulago ambapo aliuliwa na wanajeshi wa Uganda kesho yake akiwa kitandani .

Ni hayo tu kwa leo, sina mengi ya kueleza juu ya oparesheni hii ila hayo kiduchu ninaamini yamekufanya uipate picha juu ya kile kilichotokea miaka 40 iliyopita. Ninaweza nikawa sijaandika kwa mtiririko mzuri ila nadhani hoja yangu imefika na imeeleweka.

Unaweza wasiliana nami kupitia +255653737353 (WhatsApp) au nyambeya@yahoo.com
 
Hongera sana Mkuu,
Japo ile operesheni ilikuwa ni lazima waisraeli wamalize kirahisi,
Kwasababu MOSSAD na IDF ni taasisi kubwa sana hapa duniani.
Idd Amin asingekuwa na uwezo wa kuwafanya lolote.
 
Duh! Kuna MTU kanihadithia hii story Leo. Nikaona wacha nije kuutafuta ukweli Jf
 
huwa navutiwa na sana na habari/stori hizi mngekua mnataja na movies zake zinazoelezea tukio husika ingekua safi

asante
 
Wakuu kwema?
Samahani nimekua nikisikia tu story za kuwa israel waliwah kufanya operation kubwa kwenye uwanja wa ndege wa entebe,naomba kupewa fully details za nini kilichotokea na ulimwengu ulilichukuliaje hili tukio?
Kuna kitabu kinaitwa [HASHTAG]#ninety[/HASHTAG] minutes at Entebe ni vizuri ukakitafuta na kukisoma kama wewe nimsomaji mzuri wa vitabu
 
Back
Top Bottom