⅞ Comfort Zone ni nini? Kwanini huwezi kuendelea ukiwa kwenye Comfort Zone?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,820
Kwa Kiswahili lugha yetu adhimu tuite ukanda wa raha.

Ukanda wa Raha Ni nini?
Ni eneo la hisia linalokupa faraja. Tuseme, huna kazi, unaishi kwa baba, na anakupa pocket money.

Hapo uko rahani. Hudaiwi Kodi, utakula, utalala, na bado atakupa pocket money ambayo utapata msichana na utakunywa.

Kufanikiwa, au kutoboa kwenye hali hii ni vigumu sana kwa sababu changamoto yoyote utakayokutana nayo, tayari iko solved.

Kwanini wanaoanza kujitegemea mapema wanafanikiwa zaidi?

Kwa sababu Wana majukumu, anawaza atalipaje Kodi, ataishije, atajiendelezaje nk.

Hivyo huwa na bidii, huwa na nidhamu ya fedha na huwa na mipango mashubuti.

Comfort Zone yaweza kuwa mitandao ya kijamii, ukawa busy na Instagram, Facebook, WhatsApp, JF etc, ulevi wa pombe, mihadarati nk kuondoa mawazo, lakini kaa ukijua kuwa ulimwengu unaendelea, unakupita na kukuacha kwa kasi, ukija kushtuka mvi zinaonekana huku na kule.

Hosea 7:9

Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom