60 computers have been stolen at Sokoine University | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

60 computers have been stolen at Sokoine University

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Masanilo, Oct 27, 2008.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  I have been informed that more than 60 used computers which were donated by donors to Sokoine University in August this year to help in teaching and training at different faculties and institutes within the university have been stollen from Mazimbu campus last week. The stollen computers were Compaq, Dell and IBM machines Pentium III and Pentium IV.

  I am really worried, this computers were received in early August, surplisingly were not distributed to the lecturers for almost two months now, with no strong reasons. Nina wasi wasi na mchezo mchafu umefanyika hapa, this will be a big shame to donors and funders to support SUA in future.

  My take

  This is another ufisadi which is a common problem at SUA, teaching and living conditions of both lecturers and students are very poor, while administrators are living like kings in heavens.

  Ushi Wa Rombo
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni michezo ya kuigiza tu!

  Kama zilitolewa Agosti hadi zinaibiwa walengwa hawajafikishiwa utaaminije kama hapo SUA kwenyewe zilifika. Hii ni michezo ya kipuuzi tunayochezewa Watz. Lakini tukimaliza kazi ya kuikomboa nchi, haya mambo ya kitoto yatakuwa yamefika mwisho, once and for all!!
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  DC , unadhani hadi nchi ikombolewe ndio haya mengine yaishe, by the time yatakuwa yameota mizizi na itachukua muongoa mwingine kuyamaliza!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  As per my signature!
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Bado wanatumia hizi?
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Maaama......hapo itakuwa haijakombolewa!! ....Tutakuwa bado kwenye enzi za usanii.

  Nchi hii ikikombolewa kadri ya ndoto zangu ni kwamba tutaongozwa na kichaa. Huyu kichaa atavaa kofia za ninja. Kwa maana hiyo atamtia kitanzi babake, mama, dada, kaka n.k endapo anafanya mambo yanayoinajisi jamii. Kwa hiyo muda huo wa kutiana vitanzi ukifika, huu ujinga wote huwezi tena kuuona. Ila kwa hali ya sasa ambapo kila kiongozi amekuwa kama mbuni aliyeficha kichwa kwenye mchanga ili asione adui yake, hatuwezi kwenda kokote. Kwa hawa wasanii wetu nani atamfunga paka kengele??
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu pale wanahata Pentium I, na word perfect 3.1 bado inatamba, kumbuka huu ulikuwa msaada waliokuwa wameusubiria kwa muda mrefu sasa wajanja wameamua kuzikomba....

  Ushi
   
 8. M

  Mama JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  yaani najizuia kucheka nashindwa.....let me burst.. kwi kwi kwi kwiiiiii
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Jamani tusicheke!

  Hizo pentium III na IV tungeweza kuzifikisha hadi kijijini tungepiga hatua kubwa ya maendeleo! Mnajua kuna watu hawajawahi kuiona kompyuta inafananaje? Kama ina umbo la kitunguu, kiazi au boga! Na watu wa kuonea huruma ni hawa vijana watakaosoma shule za kata hadi kidato cha 6. Watakaobahatika wataona kompyuta kwa mara ya kwanza wakati wa kujiunga na chuo kikuu. Sasa kama hao tungeweza hata kuwapelekea key board tu, tungekuwa tumewasaidia sana. Shida niliyonayo hata hizo zitaibiwa!
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  he he he heee, sicheki furaha jamani...hata msibani watu hucheka kwa uchungu baada ya kulia sana.

  .....halafu tunasema elimu imefanya nini hapa Tanzania, halafu chuo cha kilimo, na kilimo ndio uti wa mgongo. Sijui hao maafisa ugani wanakuwa competent kiasi gani kama mwalimu anayewafundisha ndio yuko hoi kiasi hicho,
   
 11. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Yo Yo;
  Sisi ni WaTanzania, hata hiyo Pentium III kuwa nayo nyumbani bado ni ishu.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani mfadhili anayeleta msaada wa Computers ambazo ni obsolete, naye inabidi amulikwe..naona hii ni kama kuifanya Tz ni disposition area..Afterall sijui kama tuna recycle systems nzuri au methods zozote ambazo ni hazard-free hapa Tz..

  Au mnasemaje wandugu?
   
 13. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #13
  Oct 28, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Absolute kwa mataifa ya magharibi lakini kwa Tanzania hizi computer zinatufaa kabisa, tena sana. Ni heri kuwa nazo kuliko kutokuwa nazo. Kujifunza computer sio lazima utumie software za Bill Gates zenye demand ya capacity kubwa. Kuna software ambazo zinatufaa na zinaweza zikatumika kwenye pentium III na IV bila matatizo. Hata ukiangalia internet cafe zetu nyingi zinatumia computer hizi hizi isitoshe hata hizi shule zetu za kujifunzia computer ni hivyo hivyo. Tunatakiwa tuwa encourage donors waendelee kutoa misaada ya computer ambazo hazitumiki huko zije kuwapa angalau mwanga na uelewa kidogo wanafunzi wetu hapa bongo.

  La kusikitisha ni huo mchezo mchafu uliochezwa wa kuzikwapua hizo computer na hapo wafadhili watakaposikia na kusitisha hii misaada.

  .
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Well said Nyumbu, tupo ukurasa mmoja! Kufundishia hatuhitaji kabisa Pentium M ama zenye core duo, hata window vista. Tuliosoma zamani bongo watakubaliana nami, nilianza kuona computer na kuitumia nikiwa second year university, kulikuwa na sheria ile mbaya ie kuvua viatu usile kitu computer lab utasababisha virus etc etc etc. Ninalaani kwa nguvu zote wizi huu wa computer hata kama ni obselete, bado zingefaa kwa wanafunzi na wallimu wao

  Respect

  ushi
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hizo P3 SPARE ZAKE HAKUNA SASA HIVI KWAHIYO ZINGKUWA HAPO SOKOINE GHARAMA ZA KUZITUNZA ZINGKUWA KUBWA SANA , NENDA MFANO UDSM KATIKA CAFE ZAO WANA P3 NYINGI SANA WANASHINDWA KUZITUNZA KUTOKANA NA VIFAA VYAKE KUWA GHALI
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo ni heri wasiwe nazo kabisa? hao walioiba spare wataizoa wapi? ama mzee ni umeshiriki wizi huo, maana jana kulikuwa na thread ikionyesha wewe hujihusisha na hayo mambo?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  P.1; P2; P3; kwa chuo kikuu? jamani this is a joke hata kama ni msaada. Mhhh.
  Mi nimeona shule za primary katika mji mmoja wa mkoa mmoja wa kanda ya ziwa shule ikipewa msaada na hao wafadhili. Komputa ni Pentium M, tena mpya kabisa. Zilikuwa kama 50.
  Sasa University?! inapewa P.3?
  Ndiyo sababu hawakuzijali kuziwekea ulinzi hadi kuibiwa.

  Ni kweli kuna cafe za aina hii lakini mimi sikubali katika ulimwengu wa leo hii kukaa katika cafe ya namna hii maana najua nitasumbuka kupata speed ya kutosha na hata wakati mwingine mashini itakuwa ina stack kila wakati. Nimeliona hili mara nyingi.
  Wafanya biashara makini wa cafes siku hizi wameachana na vikomputa hivyo vya bei bure. Kama UDSM wanazo ndio wale wale! wapenda vya bure kila kukicha


  Tunatakiwa tuwa encourage donors waendelee kutoa misaada ya computer ambazo ni za kisasa kidogo si kuturundikia vitu walivyokosa mahali pa kutupa.
  Nani alisema kama ni msaada lazima tupewe kitu ovyo vyo? Huoni magari wanayotupa msaada wanayaagiza special toka Japan? hakuna vigari vya mtumba au vilivyokwisha wanavyotupatia kama msaada.
   
 18. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Mzee unakuza mambo.
  Vifaa gani unavyozungumzia, RAM? Ninafahamu donors wanaotoa RAM za ziada wakipeleka misaada ya Computer.

  Submarine cable system itakuwa tayari mwaka 2010. Jaribu kufikiri itakuwaje ikiwa hatuna uwezo wa kuweka hata PIII kwenye zahanati au mashule. Nani atumie hiyo bandwidth? Huyu mwanafunzi wa chuo ndio tunamtegemea akatoe mafunzo kwa manesi; au hilo wafanye donors pia?
  .
   
 19. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Sikatai kwamba hakuna computer za ovyo ovyo zinaletwa kama 'misaada'. Kuna kundi la wasanii na wengi ni wenzetu wanaofanya haya ili kujipatia cheap popularity.


  Kama Ushirombo alivyosema, hizi ni IBM computers sio zile wanaziita CLONE.
  Computer zilizo cafe ziko slow kwa sababu kadhaa, mojawapo ni virus au ni clone PC (zile zisizo hata na brand name)
  .
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Lazy dog mimi nipo sokoni kwahiyo najua jinsi hivyo vitu vinavyotumika kuuzwa na kadhalika hapo p3 mfano memory yake ya 256 sdr kwanza huzipati ni duka moja tu wanauza tena kvd bei yake ni kuanzia alfu 50 wakati ungekuwa na duo core kwa hiyo alfu 60 unapata 1gb ya ram ddr2 , p3 mainboard zake hakuna sasa hivi , ukija katika duo board zake zinaanzia alfu 60 mpaka laki moja inategemea unataka aina gani , ukija katika hdd hizo za duo nyingi wanatumia sata harddrive ya sata ni alfu 40 mpaka 50 kwa 80 gb wakati ide ambayo ndio hiyo p3 kwanza hazipo sana kama ukipata ni kuanzia alfu 60 kwa 40 gb tena nyingi zimetumika

  nenda sokoni ukaone mambo sio unaongea tu ulimradi

  kwahiyo hao watu wanaotoa misaada kama hiyo siku nyingine wapigwe marufuku kutuletea mizigo hiyo halafu unakuta wanaweka operating system ambayo sio genuine -- sasa hizo computer 60 waaamue kununua genuine operating system
   
Loading...