6 vs sisiem | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

6 vs sisiem

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Far star, Nov 18, 2010.

 1. F

  Far star Senior Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama sitta uliweza kutetea hoja zako wakati wa hayati mwalimu na ukalambwa viboko pale ikulu wakati ukiwa mwanafunzi wa udsm,sasa unashindwa nini kuondoka ccm na kuonyesha misimamo yako? usogope kutetea ukweli na kusimamia haki kwa kuhofia kuonekana msaliti, tena wakati ule hapakuwa na vyama vingi wala mbadala wa ccm,sasa leo kuna mbadala na kama unaona umeonewa/ kuchakachuliwa na mafisadi unagonja nini kuhama na kuachana nao,maana mapinduzi yoyote yawe ya kiuchumi,kisiasa au kijamii yana gharama zake.Tafuta njia ya kweli katika utetea kile unacho kiamini na usipoteze muda kwa kuogopa lawama zisizo na msingi.amua kuwa fisadi au mwana mapinduzi wa kweli.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inawezekana Sita akawa na wazo la kuondoka ccm lakini je uhai wake utakuwa ktk hali ya usalama?
  Maana sita alikuwa ni kiongozi mkubwa na anazijua siri nyingi sana za ccm.
  Watamruhusu aondoke na siri zao?
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Far star+ndibalema, mbona siwaelewi?, hebu fafanueni. Kuna nini kati ya sita+ccm? Mnataka kusema amezibwa mdomo asitetee haki?, amezibwa na nani/kivipi?,. ACHENI UCHOCHEZI.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Sitta kuonyesha umeumizwa, usikubali kuingia kwenye baraza la mawaziri ni heri ubaki kama mbunge tu na kufanya kazi za Bunge tu kama Mbunge. Kuingia kwenye baraza la mawaziri ni sawa na kujishusha kwani mwanzo umekuwa kiongozi wa mhimili wa dola sasa unashuka na kukaa ndani ya muhimili mwingine wa dola na kuwa chini ya mkuu wa muhimili huo.

  Kwa nini usiige mfano wa Dr. William Shija jamani? Mwanzo nilikuambia usichukue fomu ya Uspika lakini hukusikia na kukimbilia fomu; sasa ninakuambia usikubali kuwa waziri kwa sababu wenzio akina Prof. Mbilinyi walichomekewa skendali na kuishia kujiuzulu sasa na wewe subiria skendali kwenye hiyo wizara utakayopewa na kuishia kujiuzulu au JK kufanya reshuffle na kukuacha katikati ya mbuga ya Mikumi usiku huku simba wakiunguruma, na JK hana joke kwenye kutoa kafara utaishia kama akina Mramba, Yona na Mgonja, Karamagi, Msabaha, na Eddo.

  Nafikiri hakuna kwenye historia ya Tanzania na haikubaliki kuwa Spika mstaafu kuwa waziri, naomba msaada kwenye hili kama historia hii ipo!
   
Loading...