CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,250
- 12,868
Good morning Ladies under Gentlemen (Sosi: Idd Amin)
Natumaini hamjamboni nyote hapa jukwaani, kwa wale wagonjwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye .
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha miaka mitano (5) nikiwa hapa kwa Mkoloni, si jambo rahisi kufikisha miaka mitano, kuna ambao walipata redundancy, kuna ambao waliacha kwa mapenzi yao na kuna ambao walitangulia mbele za haki. Ila mimi bado nipo, ni jambo la kushukuru kwa kweli.
Pili napenda kumshukuru Mama yangu mzazi kwa kunitia moyo, asikwambie mtu katika kazi kuna changamoto nyingi sana, isingekuwa mama yangu aisee ningeacha kazi na kurudi Ushagoo kulima. I LOVE YOU MUMMY Kama mjuavyo Majungu, wivu, fitina na kijicho ni Unkwepable katika kazi. Hivyo basi nilipitia katika kipindi kigumu sana katika hii kazi. Kuna Mtumishi mmoja wa Shetani alitaka kuniharibia, ila kwa mkono ulio hodari wa Mwenyezi Mungu alishindwa na nawaambia yale mabaya yote alikuwa kuwa akinifanyia yalimrudia. Mungu ni mwema na nimeuona mkono wake jamani .
Tatu napenda kuwashukuru WANAJAMIIFORUM woooote kwa kunitia moyo kwa namna moja ama nyingine, nimekuwa nikisoma post za watu waliopitia changamoto zinazofanana na zangu na jinsi gani wamekuwa wakizikabili. Mmekuwa msaada kwangu kimawazo, pia hata katika kupunguza stress hasa jukwaa la picha na Jokes. Huwa nafarijika sana kwa kupita majukwaa hayo ili kupunguza stress za kazi. Daddy angu watu8 na Mzee Mtambuzi hamkuwa nyuma kunitia moyo, hakika mawazo na ushauri wenu umenijenga sana. Mbarikiwe saaaaaaaana, mnaweza msijue ni kwa namna gani mmenifanya nimekuwa strong katika kazi ila napenda kuwaambia ushauri wenu ni mkubwa sana na sitawasahau.
Mwisho napenda mjumuike name katika kuadhimisha miaka mitano (5) hapa kwa mkoloni .
Humbled
CL

Last edited by a moderator: