500 Zimbabwean dollar sawa na 1USD, 2400 Tanzania Shilingi sawa na 1USD, Wazimbabwe wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao na sisi tunakwama wapi?

Hawajapandisha thamani Bali wametengeneza hela mpya yenye jina jengine.

Kuelewa zaidi chukulia mfano huu, hela yetu inaitwa Tanzanian shillings (TSh) kwa sasa 2400 Unapata Dola 1. Halafu serikali iamue wanatengeneza hela mpya, iitwe New Tanzanian shillings (NTsh) halafu hii hela mpya iwe na thamani Mara 4800 ya Hela ya zamani. Ina maana hapa NTsh 1 itakuwa sawa na Dola 2.

Wazimbabwe wametengeneza hela mpya inaitwa New Zimbabwean Dollar (ZWL) ambayo ni sawa na matrilioni ya Hela ya zamani, hela ya zamani ilikuwa na Noti hadi ya Trilioni 100.

Soma zaidi hapa
Mimi siyo mchumi na bado somo halijaingia kichwani, sasa kama hiyo ndo suluhu si nchi zote zingenetengeza hela mpya ili kupandisha hela zao, naamini mmerekani asingekubali hela yake kuzidiwa na currency yoyote duniani.
 
Hela kuwa na thamani si kigezo cha uchumi mkubwa, inatakiwa tu hela iwe stable. Na hela mpya haipandishi thamani inapunguza tu sifuri
 
Mimi siyo mchumi na bado somo halijaingia kichwani, sasa kama hiyo ndo suluhu si nchi zote zingenetengeza hela mpya ili kupandisha hela zao, naamini mmerekani asingekubali hela yake kuzidiwa na currency yoyote duniani.
kwa hiyo unaamini currency ya usa haizidiwi na yoyote duniani!
 
Hawajapandisha thamani Bali wametengeneza hela mpya yenye jina jengine.

Kuelewa zaidi chukulia mfano huu, hela yetu inaitwa Tanzanian shillings (TSh) kwa sasa 2400 Unapata Dola 1. Halafu serikali iamue wanatengeneza hela mpya, iitwe New Tanzanian shillings (NTsh) halafu hii hela mpya iwe na thamani Mara 4800 ya Hela ya zamani. Ina maana hapa NTsh 1 itakuwa sawa na Dola 2.

Wazimbabwe wametengeneza hela mpya inaitwa New Zimbabwean Dollar (ZWL) ambayo ni sawa na matrilioni ya Hela ya zamani, hela ya zamani ilikuwa na Noti hadi ya Trilioni 100.

Soma zaidi hapa

Fafanua vizuri
Tunataka tufkke tulikotoka 1Tz shiling =1 dollar
 
Mkuu hata wewe leo ukiamua unaweza kufanya currency denomination upya na ukaipeg pesa yako na pesa ya nchi nyingine let's say Dollar kwa hiyo pesa yako mpya itakua na ratio labda ya 1:1 yaani Dollar 1 sawa na JF shillings 1.

Sasa changamoto inakuja je kwenye soko kukoje? Mfumuko wa bei ukitokea ina maana noti yako ya 1 JF Shillings itahitajika ziwe nyingi ili ununue bidhaa moja. Hivyo basi muda unavyozidi kusonga ukipiga hesabu za purchasing power parity yaani uwezo wa pesa kufanya manunuzi kwa kulinganisha nchi utagundua nguvu ya Dollar 1 ya US ni kubwa mnoo kuzidi JF shillings kuliko TZS. So mwisho wa siku ndio unakuta kutoka ratio ya USD 1= 1 JF Shs inakua USD 1= 1000 JF Shs.

So kikubwa hapo usiangalie tu Dollar moja ya marekani inalingana vp na 500 Zim dollars bali angalia purchasing power parity utagundua bado ipo nyuma sana kulinganisha na maybe pesa ya Tanzania.

Yaani 2400 ya TZ unakuta ina fanya manunuzi mengi kuliko hyo 500 ya Zimbabwe.
Apa ndugu yangu sijakuelewa kusema 2400 itafanya manunuzi mengi kuliko 500 si ni sawa kwa sababu 2400 ni zaid ya mara nne kwa 500 ,au sijaelewa wap
 
Hakuna cha thamani wala nini ni wizi wa mataifa makubwa kuwaibia mataifa madogo wasiokuwa na interest nayo. Zimbabwe kuna mabeberu wengi walibaki wanamiradi na mashamba makubwa aambamba na adrika kusini na kenya hakuna cha vigezo vya uchumi wala nini yameamua tuu kutunyanyapaa
 
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

View attachment 1906061
Hii kitu hata Zambia walifanya hivyohivyo. Walifanya rebase.
 
Dogo huyu
tendai1_0.jpg

Matoroli haya
Man-carrying-money-in-wheelbarrow.jpg
😂 😂 😂
 
Apa ndugu yangu sijakuelewa kusema 2400 itafanya manunuzi mengi kuliko 500 si ni sawa kwa sababu 2400 ni zaid ya mara nne kwa 500 ,au sijaelewa wap
''500'' ya Kenya inafanya manunuzi kuliko elfu 10 ya Tanzania.... I hope unalijua hilo. Kwahyo sio issue sana eti kuwa na hela yenye shillingi 1-1000 basi eti una uchumi mzuri kuliko mwenye noti ya elfu 50. Kikubwa ni jinsi gani pesa yako ina nguvu kulinganisha na dollar.

Mfano 500 hyo ya zimbabwe tumeambiwa ni sawa na Dollar 1. Ila Tanzania 2400 ndio sawa na Dollar 1. Lakini ukiangalia nguvu ya manunuzi/purchasing power parity unaweza kuta 2400 ya Tanzania inanunua vitu vingi kuliko hyo 500 ya Zimbabwe sababu vitu vingi kma supply ya bidhaa ama mfumuko wa bei.

Na ndio maana hta wakipiga hesabu za pato la taifa siku hizi wana factor in Purchasing Power Parity ili kupima je dollar moja ukiwa nayo mfano Tanzania utanunua vitu vingapi kuliko ukiwa na dollar moja zimbabwe??? Sasa ukishajua tofauti ndio utaona hela ya nani ina thamani.

Kuna nchi watu wanalipwa dollar 100 kwa siku ila maisha magumu sababu money supply ni kubwa so vitu vinapanda bei kila siku unakuta mtu hafaidi hiyo dollar 100 anaishia kununua msosi tu. Lakini hyo dollar 100 kwa Dar unaweza nunua msosi pekee?? So haya masuala ya pesa ni vzuri tuangalie kwa umakini maana sio necessarily eti mia 500 ya zimbabwe italingana thamani na 2400 yetu kwa kigezo tu kwamba zote ni sawa na dollar 1 ya US.
 
Cha kushangaza kwenye miaka ya 1970's Dola 1 ya Kimarekani ilikua ni sawa na Shilingi 5 tu za Kitanzania, kiasi cha kusababisha magari ya kubebea abiria Jiji Dar es salaam kuitwa Dala dala!!

Baada ya hapo, imebakia historia! Ukiwauliza Wachumi sababu za kuporomoka kwa thamani ya Shilingi yetu, utajikuta unatoka kapa! Kutokana na maelezo yao ya kwenye vitabu.
 
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

View attachment 1906061

Mkuu unajua kuwa:

Japan, Yen 110 ni 1 USD wakati pia
Kenya, Shs 110 ni 1 USD

Labda kama unataka kusema karibu mnaowaita k*nya land karibu wanawa overtake wa Jap.

Uwanja huu nao mkuu mpana tu kama ule wa Corona na kina Gwajiboy.

Vinginevyo inakuwa kelele tu.
 
Mimi siyo mchumi na bado somo halijaingia kichwani, sasa kama hiyo ndo suluhu si nchi zote zingenetengeza hela mpya ili kupandisha hela zao, naamini mmerekani asingekubali hela yake kuzidiwa na currency yoyote duniani.

Unajua kuwa 1USD = 0.85 EURO
 
Unajua kuwa 1USD = 0.85 EURO
Jifunze kusoma ukaelewa Jambo ndo ukachangia soma tena nilichokiandika nazijua currency zoote za dunia hii. Rudi soma, rudia, rudia utaelewa yawezekana darasani wewe ni wale ambao huwa wanaelewa kesho yake baada ya mwalimu kutoka darasani
 
Tsh against USD haijafika 2,400 Sasa hv hela yetu imeongeza nguvu kidogo tupo 2,314 nafikiri export ya Chakula to Kenya and Sudan ndo imebust kidogo japo kitu Kama mahindi tungeyasaga na kuuza Kama unga saiz sisi na wakenya ingekuwa Ksh 1= Tsh 15 au chini yake
Screenshot_20210826-083142.png
Screenshot_20210826-083219.png
 
Haya mambo ya GDP sijui na Purchase Parity ni balaa!

Kwenye kusoma tuliambiwa “Balance of trade” ndio suluhu ila sasa sioni hao wenye mamlaka wakipambana na hilo zaidi ya kutengeneza mazingira ya kupokea mishahara na posho tu! Ina maana akina mwigulu hawaoni haja ya kutatua changamoto ya balance of trade ili tuweze kuwa na export kubwa dhidi ya Imports?

Binafsi naona tuna nafasi kubwa tu ya kupandisha thamani ya pesa yetu ila ni kama vile hamna cordination ya wale tuliowapa dhamana! Mazao yangetusaidia sana maana janja ya technology hatuna nashindwa kuelewa tumeshindwaje hata kualika wajapan wafungue viwanda sio vya kuuzia humu ndani bali ku export nchi washirika za Africa these minor and matured technologies za computers,simu,cars wich are branded as made in Tanzania sidhani kama watakataa! Mabalozi wanafanya kazi gani huko?
 
Back
Top Bottom