500 Zimbabwean dollar sawa na 1USD, 2400 Tanzania Shilingi sawa na 1USD, Wazimbabwe wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao na sisi tunakwama wapi?

Apa ndugu yangu sijakuelewa kusema 2400 itafanya manunuzi mengi kuliko 500 si ni sawa kwa sababu 2400 ni zaid ya mara nne kwa 500 ,au sijaelewa wap
Nilivyoelewa Ni kwamba zote 2400/500 Ni dola 1 ya marekani..
Inatakiwa Kama 500 ya Zimbabwe inanunua lita moja ya petrol Basi na 2400 ya Tanzania inunue lita 1 ya petrol..
Lakini Kama lita 1 ya petrol huko Zimbabwe Ni 3000 ya Zimbabwe.. Basi hela ya Tanzania kwenye uhalisia itakuwa na thamani kuliko ya Zimbabwe
 
Mzee wa tozo Ni mchumi wakati huo Ni waziri wa fedha lakini sijawahi kusikia akiwa na mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu...
 
Hawajapandisha thamani Bali wametengeneza hela mpya yenye jina jengine.

Kuelewa zaidi chukulia mfano huu, hela yetu inaitwa Tanzanian shillings (TSh) kwa sasa 2400 Unapata Dola 1. Halafu serikali iamue wanatengeneza hela mpya, iitwe New Tanzanian shillings (NTsh) halafu hii hela mpya iwe na thamani Mara 4800 ya Hela ya zamani. Ina maana hapa NTsh 1 itakuwa sawa na Dola 2.

Wazimbabwe wametengeneza hela mpya inaitwa New Zimbabwean Dollar (ZWL) ambayo ni sawa na matrilioni ya Hela ya zamani, hela ya zamani ilikuwa na Noti hadi ya Trilioni 100.

Soma zaidi hapa
Same to Zambia kwacha walifanya hivyo
 
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

View attachment 1906061
Hawa wazimbabwe wameintroduce new currency as side effect za inflation
 
Zambia nao walifanya kupunguza sifuri kwenye Kwacha.

Kuna kitu nimeona kwenye hela ya Burundi, official exchange rate ya 1BIF=1.1Tzs.
Ila ukienda mpakani 1BIF=0.7Tzs
 
Mzee wa tozo Ni mchumi wakati huo Ni waziri wa fedha lakini sijawahi kusikia akiwa na mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu...
Kupanda Kwa thaman ya fedha hakuna mahusiano na ukuaji wa uchumi in contrary currency depreciation (kupunguza thaman ) ni Kwa ajili ya kukuza exportation ya bidhaa zinazozalishwa mfano mmoja rahisi ni huu kama wamarekan wananunua maparachichi 4 Kwa dola Moja Ili kuwafanya waweze kununua maparachichi mengi Kwa dola Moja Ile Ile unawapa maparachichi sita Ili wewe uuze sana na wasiende kununua maparachichi nchi ingine
 
Kuongeza thaman ya pesa unamaanisha kuwa hutaki uza sana bidhaa sana nje ya mipaka yako na sababu kubwa inaweza ikawa shortage ya bidhaa hio mfano kama Kenya Uganda Kuna njaa na mahitaji ya ndani ya mahindi ni tani 57000 na wewe wakati huo maybe una tan 61000 maana yake surplus ya mhindi ni ndogo therefore unatakiwa upandishe thaman ya pesa zako Ili hao majiran wasije nunua mahindi kwako
 
Back
Top Bottom