500 Zimbabwean dollar sawa na 1USD, 2400 Tanzania Shilingi sawa na 1USD, Wazimbabwe wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao na sisi tunakwama wapi?

Android

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
970
1,207
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

Screenshot_20210824-120516.png
 
Hawajapandisha thamani Bali wametengeneza hela mpya yenye jina jengine.

Kuelewa zaidi chukulia mfano huu, hela yetu inaitwa Tanzanian shillings (TSh) kwa sasa 2400 Unapata Dola 1. Halafu serikali iamue wanatengeneza hela mpya, iitwe New Tanzanian shillings (NTsh) halafu hii hela mpya iwe na thamani Mara 4800 ya Hela ya zamani. Ina maana hapa NTsh 1 itakuwa sawa na Dola 2.

Wazimbabwe wametengeneza hela mpya inaitwa New Zimbabwean Dollar (ZWL) ambayo ni sawa na matrilioni ya Hela ya zamani, hela ya zamani ilikuwa na Noti hadi ya Trilioni 100.

Soma zaidi hapa
 
Kwa level ya pesa ya Zimbabwe ilipofikia namna pekee ikawa kuresort kwenye barter trade.

Anyway, wakati nasoma ilikua rahisi sana ukiulizwa dola 100 ni sawa na sh ngapi as ilikua dola 1 ni 1000.

Serikali imeshindwa kuturudisha pale.

Nchi inatakiwa iwe na uwiano sawa kati ya bidhaa inazoagiza kutoka nje (import) na inazopeleka nje (export) na itapendeza zaidi kama export itaizidi import.

Tz tunaexport nini na nini? Tuna mpango wa kuexport nini na nini? Wizara ya kilimo na Wizara ya Madini nafikiri zilitakiwa ziwe mstari wa mbele katika exportation kwa kuwatafutia wakulima na wachimba madini soko.

Bahati mbaya serikali imefocus kwenye tozo na kodi ya jengo.
 
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

View attachment 1906061
Mkuu nami nimejionea, nadhani sisi wabongo tuna shida sehemu,

1629798852137.png

Wasalaam
 
Kwa level ya pesa ya Zimbabwe ilipofikia namna pekee ikawa kuresort kwenye barter trade.

Anyway, wakati nasoma ilikua rahisi sana ukiulizwa dola 100 ni sawa na sh ngapi as ilikua dola 1 ni 1000.

Serikali imeshindwa kuturudisha pale.

Nchi inatakiwa iwe na uwiano sawa kati ya bidhaa inazoagiza kutoka nje (import) na inazopeleka nje (export) na itapendeza zaidi kama export itaizidi import.

Tz tunaexport nini na nini? Tuna mpango wa kuexport nini na nini? Wizara ya kilimo na Wizara ya Madini nafikiri zilitakiwa ziwe mstari wa mbele katika exportation kwa kuwatafutia wakulima na wachimba madini soko.

Bahati mbaya serikali imefocus kwenye tozo na kodi ya jengo.
Kuna mada huwa tukijadili naishia kupata hasira tu maana kuna watu wanatufanyia kusudi serikalini tunafeli.
 
Miaka si mingi iliyopita, thamani ya 1USD ilikua ni sawa na matrilioni kadhaa ya pesa ya Zimbabwe. Lakin leo thamani ya 1USD ni sawa na 500ZWD tu.

Wakati huo thamani ya 1USD ikiwa matrilioni kadhaa nchini Tanzania 1USD ilikua 1600TZS lakin sasa ni 2400TZS.

Wamewazaje kupandisha thamani ya pesa yao kwa haraka hivyo? Na sisi tunakwama wapi?

View attachment 1906061
Mkuu hata wewe leo ukiamua unaweza kufanya currency denomination upya na ukaipeg pesa yako na pesa ya nchi nyingine let's say Dollar kwa hiyo pesa yako mpya itakua na ratio labda ya 1:1 yaani Dollar 1 sawa na JF shillings 1.

Sasa changamoto inakuja je kwenye soko kukoje? Mfumuko wa bei ukitokea ina maana noti yako ya 1 JF Shillings itahitajika ziwe nyingi ili ununue bidhaa moja. Hivyo basi muda unavyozidi kusonga ukipiga hesabu za purchasing power parity yaani uwezo wa pesa kufanya manunuzi kwa kulinganisha nchi utagundua nguvu ya Dollar 1 ya US ni kubwa mnoo kuzidi JF shillings kuliko TZS. So mwisho wa siku ndio unakuta kutoka ratio ya USD 1= 1 JF Shs inakua USD 1= 1000 JF Shs.

So kikubwa hapo usiangalie tu Dollar moja ya marekani inalingana vp na 500 Zim dollars bali angalia purchasing power parity utagundua bado ipo nyuma sana kulinganisha na maybe pesa ya Tanzania.

Yaani 2400 ya TZ unakuta ina fanya manunuzi mengi kuliko hyo 500 ya Zimbabwe.
 
Kwa level ya pesa ya Zimbabwe ilipofikia namna pekee ikawa kuresort kwenye barter trade.

Anyway, wakati nasoma ilikua rahisi sana ukiulizwa dola 100 ni sawa na sh ngapi as ilikua dola 1 ni 1000.

Serikali imeshindwa kuturudisha pale.

Nchi inatakiwa iwe na uwiano sawa kati ya bidhaa inazoagiza kutoka nje (import) na inazopeleka nje (export) na itapendeza zaidi kama export itaizidi import.

Tz tunaexport nini na nini? Tuna mpango wa kuexport nini na nini? Wizara ya kilimo na Wizara ya Madini nafikiri zilitakiwa ziwe mstari wa mbele katika exportation kwa kuwatafutia wakulima na wachimba madini soko.

Bahati mbaya serikali imefocus kwenye tozo na kodi ya jengo.
Changamoto yetu ni kwamba tunategemea Extractive industry mfano mazao au madini sasa bei ya bidhaa ikiporomoka duniani then sisi tunaumia na ndio maana mpango wa taifa ukagusia TZ ya Viwanda ili kuongeza thamani ya mazao/madini N.k ili tuuze kma BIDHAA na sio Raw material (nimekosa tafsiri) hii inalenga kuongeza pato la fedha za kigeni ili kuweka urari wa BOP yetu.

So tukifanikiwa kma "makaratasi" yanavyosema basi tusishangae USD 1 ikawa sawa na TZS 100.

Lakini........ Pesa kupanda thamani inaharibu uwekezaji unless muwe na soko kubwa la ndani otherwise inakua gharama watu kuja kununua bidhaa huku maana Dollar 1 itanunua vichache kuliko akienda say China au Uganda!!! So unaweza ona Tz kuwa na pesa imeshuka thamani lakini kwa jicho la kiuchumi kma tutakuwa exporters itatuletea shida.... Ila kma tutaendelea kuwa importers basi pesa kupanda thamani ndio itakua na faida.
 
Kiswahili chake ni malighafi.

Nakubaliana na wewe kwamba pesa kua na thamani ndogo kunaongeza sana exportation.

Idea ya viwanda ilikua sahihi lakini nafikiri hatukua tunajua tunataka viwanda gani, historically inaonyesha ili ufikie kwenye viwanda ni lazima kuwe na mapinduzi ya kilimo ambayo yataenda sambamba na elimu ya kukupa wataalamu.

Hiki kitu Shivji alikisema, nimesahau kitabu gani, sasa nini kilitokea kwa Tz wakati tunachagua dira ya viwanda? Ni ilikua tunataka kuruka huku hatujaagana na nyonga.
 
Back
Top Bottom